Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 7 Rajab 1446 | Na: H 1446 / 070 |
M. Jumanne, 07 Januari 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kuganda Baridini hadi Kufa kwa Watoto Wachanga, na Njaa na Uuaji wa Watoto Hayatoshi Kukomesha Mauaji ya Halaiki huko Gaza!
(Imetafsiriwa)
Mnamo tarehe 30 Disemba, iliripotiwa kuwa mtoto wa 6 waliganda hadi kufa mjini Gaza ndani ya wiki mbili kutokana na hali ya baridi inayovumiliwa na wakimbizi wa Kipalestina katika mahema ya muda, waliohamishwa kutoka kwa nyumba zao kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara ya Ukanda huo na uvamizi wa Kiyahudi. Ali al-Batran mwenye umri wa mwezi mmoja alifariki siku moja baada ya kaka yake pacha, Jumaa al-Batran, huko Deir el-Balah. Baba yao, Yahya Muhammad al-Batran, alisema kuwa Jumaa alipatikana kichwa chake kikiwa kama “donge la barafu”. Nariman, mama wa Sila Mahmoud al-Fassih mwenye umri wa siku 20, ambaye pia alifariki kutokana na kupungua kwa joto la mwili, alielezea kumkuta mtoto wake akiwa rangi ya bluu na kuuma ulimi wake huku damu ikimtoka mdomoni. Zaidi ya watu milioni 1.6 wa Gaza wamelazimishwa kuingia kwenye makaazi ya muda, wakiishi katika mahema hafifu ambayo hayatoi ulinzi kutokana na hali ya hewa ya baridi kali. Zaidi ya hayo, kikwazo cha kikatili cha umbile la Kiyahudi cha Ukanda huo, kikizuia kuingia kwa nguo za baridi, blanketi na mafuta; kukatwa kwa umeme; na uharibifu wa miundombinu mingi ya umeme ya Gaza imeongeza hali mbaya ya maisha ya watu. Watoto wachanga pia wametolewa kwenye mashini za kuotamia mapema kutokana na ukosefu wa uwezo, uhaba wa mafuta na uharibifu wa hospitali. Haya yote ni pamoja na viwango vibaya vya njaa vinavyowatesa watoto wa Gaza kutokana na kuzuiwa kwa chakula na mahitaji mengine muhimu. Utafiti uliochapishwa mnamo Disemba 2023 uliofadhiliwa na War Child Alliance Charity, uligundua kuwa 96% ya watoto mjini Gaza wanahisi kwamba kifo kiko karibu, na karibu nusu yao walitamani kufa kutokana na viwango visivyofikirika vya kiwewe ambavyo wamevumilia. Zaidi ya watoto 17,400 wameuawa mjini Gaza tangu Oktoba 7, 2023 - sawa na mtoto 1 kuuawa kila dakika 30. Bragi Gudbrandsson, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Haki za Mtoto, alisema, “Vifo vya watoto vinakaribia kuwa vya kipekee kihistoria. Hapa ni mahali pa giza sana katika historia ... sidhani kama tulishawahi kuona kabla ukiukaji ambao ni mkubwa sana kama tulivyoona mjini Gaza.”
Enyi Waislamu! Je, hamuoni kwamba hata kiwango hiki cha kihistoria cha mateso na mauaji ya watoto wa Gaza hakitoshi kutikisa dhamiri ya serikali hata moja chini ya mfumo huu wa sasa wa dunia kukomesha mauaji haya ya halaiki? Je, haiko wazi kwamba leo hakuna dola ambayo inajali kwa dhati utakatifu wa maisha ya Waislamu au yenye dhamira ya kisiasa ya kusimama kwa ajili ya maslahi ya Waislamu na kuwatetea? Je, hamuoni kwamba kila sheria na mkataba wa haki za binadamu, haki za wanawake na haki za watoto umefanywa kuwa hauna maana kuhusiana na kuwalinda wanawake na watoto wa Gaza, ndani ya mfumo tasa wa ulimwengu ambao dola kubwa ziliwezesha umbile la mauaji la Kiyahudi kufanya kila uhalifu unaofikiriwa bila kuadhibiwa na bila kizuizi!? Je, hamuna hasira na tawala zenu zinazosimama tii huku watoto wa Kipalestina wakifa njaa, kuganda na kuchinjwa?!!
Enyi Majeshi ya Waislamu! Hakuna hata moja kati ya maovu haya mnayoyashuhudia mjini Gaza yatakayokwisha mpaka muchukue msimamo na musimame kwenye wajibu wenu wa kuulinda Ummah wenu na mutoe Nusrah yenu (msaada wa kimada) kwa ajili ya kusimamisha dola ya Khilafah kwa njia ya Utume ambayo Mtume wenu (saw) aliitaja kuwa ni mlinzi na ngao ya Waislamu, kwani ndiyo dola pekee yenye utashi wa kisiasa wa kulikusanya jeshi lake kukomboa kila shubiri ya Palestina kutokana na uvamizi huu wa kikatili. Kukomesha mauaji haya ya halaiki ni juu yenu! Na kila siku munapochelewa kutekeleza wajibu wenu wa Kiislamu wa kutoa nusra yenu kusimamishwa Khilafah, mateso ya watoto wa Gaza yanazidi tu! Kwa hivyo ufanyeni mwezi huu wa Rajab ambao Al-Quds ilikombolewa ndani yake na Salahuddin al-Ayyubi kutoka kwa uvamizi wa vita vya msalaba, kuwa chanzo cha msukumo kwenu kuiga ushindi huu mkubwa kwa kutoa nusra kuasisiwa Khilafah Rashida ya pili na kuikomboa Palestina kutokana na uvamizi huu wa Kiyahudi! Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[وَمَا لَكُمْ لاَ تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللّهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاء وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَـذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا]
“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako.” [An-Nisa: 75].
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info |