Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
H. 12 Jumada I 1445 | Na: H.T.L 1445 / 08 |
M. Jumapili, 26 Novemba 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Lebanon cha Andaa Semina ndani ya Wigo wa Amali ya Wanawake ya Kiulimwengu kwa ajili ya Palestina
(Imetafsiriwa)
Kitengo cha wanawake cha Hizb ut Tahrir katika wilayah ya Lebanon, leo, Jumapili, kilifanya semina katika mji mkuu, Beirut, ndani ya wigo wa siku ya kufanya kazi ya wanawake ulimwenguni kwa ajili ya Palestina kuyalingania majeshi ya Waislamu kuwaokoa wanawake wa Gaza na watoto wake na kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina), mbele ya uhudhuriaji wa wanawake.
Ambapo semina hiyo ilianza kwa kusomwa Aya za Qur'an Tukufu kutoka Surat Muhammad, kisha Dada Rana Mustafa, Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, akawasilisha kwa niaba ya Dkt Nizreen Nawaz, Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, hotuba yenye kichwa: "Ukombozi Kamili wa Palestina uko Mikononi mwa Majeshi ya Waislamu wao Pekee ndio wenye Uwezo wa Kumaliza Mauaji ya Halaiki! Hotuba hiyo ilizungumzia ndani yake uwezo na rasilimali za Umma ambazo zinaidhinisha majeshi yake kutaharaki kuikomboa Palestina na kwamba hili haliwezekani kutokea kwa kuzingatia serikali zilizoko sasa, bali hapana budi kuweko na mchungaji ambaye watu watapigana nyuma yake, mwenye ikhlasi kwa Umma wake mlinzi wa maslahi yake, na akayaelekea majeshi kwa hotuba hiyo ili yataharaki na kuwaokoa watu wetu mjini Gaza.
Na baada ya hotuba hiyo, kelele za takbira na shangwe zilitolewa kunusuru Gaza na watu wake, na kisha video yenye kichwa: "Gaza iko chini ya Moto, taharakini, enyi Majeshi, hadi mupate Heshima na Muifute Aibu" ikaonyeshwa.
Hotuba ya pili ilitolewa na Dada Ihsan Muhammad, na ilikuwa kwa kichwa: "Je! Bado mungali Kambini Mwenu?", ambayo ilituma jumbe nne; wa kwanza wake kwa wenye mamlaka kumuogopa Mwenyezi Mungu, na kumcha, na wakomeshe usaliti, na wa pili kwa watawala, na wa tatu kwa majeshi kuchukua dori yao katika kuwatetea watu wa Palestina, ama ujumbe wa nne, ulikuwa ni kwa wanawake juu ya umuhimu wa dori yao na umuhimu wa kusema neno la haki lenye athari kubwa, na akahitimisha hotuba yake kwa mapendekezo ya kivitendo kwa waliohudhuria katika kubeba ulinganizi, na kuchochea majeshi na kutokata tamaa na Nusra ya Mwenyezi Mungu. Kisha hotuba hiyo ilifuatiwa na shangwe na video yenye kubeba wito kwa wanajeshi wa Umma.
Ama hotuba ya tatu na ya mwisho, ilitolewa na dada Reem Mohsen, yenye kichwa: "Maumivu na Matumaini!" ambayo ilizungumzia juu ya matumaini yaliyozaliwa baada ya Vita vya Gaza, pamoja na kutofaulu kwa mipango ya Magharibi ya kuutengua Umma na kufuta kadhia ya Palestina kutoka kwa kumbukumbu, na vilevile watu kusilimu baada ya kuona uthabiti wa Gaza na watu wake.
Hitimisho la semina hiyo lilikuwa dua kutoka kwa dada Khadija Akash, ambayo alimuomba Mwenyezi Mungu kukubali na kutia tawfiq na kutuondolea mapungufu yetu maovu na uzembe kutoka kwetu kuelekea watu wa Gaza, na atufungulie nyoyo za majeshi na kuwaimarisha katika Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu, na kututunuku Dola ya Khilafah katika njia ya Utume.
Semina hiyo ilimalizika na mahojiano kadhaa na wazungumzaji na waliohudhuria kuhusiana na suluhisho la kadhia ya Gaza.
Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon
Sehemu ya Amali ya Semina ya Wanawake iliofanyika jijini Beirut ndani ya wigo wa "Siku ya Kiulimwenguni ya Wanawake Kuchukua Hatua kwa ajili ya Palestina" iliyoandaliwa na Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
- Hotuba kwa kichwa: Mauaji ya Halaiki Hayatakwisha isipokuwa tu kwa Ukombozi Kamili wa Palestina Mikononi mwa Majeshi ya Waislamu -
Iliyowasilishwa na Ustadha Rana Mustafa kwa Niaba ya Dkt. Nizreen Nawaz
- Hotuba kwa Anwani: Je! Bado mungali Kambini Mwenu?" -
Iliyowasilishwa na Ustadha Ihsan Muhammad
- Hotuba kwa Anwani: Maumivu na Matumaini -
Iliyowasilishwa na Ustadha Reem Mohsen
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
https://hizbut-tahrir.info/sw/index.php/taarifa-kwa-vyombo-vya-habari/lebanon/3594.html#sigProIdcf8423234e
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Lebanon |
Address & Website Tel: |