Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Malaysia

H.  23 Rabi' I 1443 Na: HTM 1443 / 02
M.  Jumamosi, 30 Oktoba 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

JHEAINS Inatenda kwa Kupitiliza Kuliko Idara Nyinginezo za Kidini kwa Kumueka Kizuizini Mwanachama wa Hizb ut Tahrir, Mkewe na Familia yake!

(Imetafsiriwa)

Idara ya Masuala ya Dini ya Kiislamu ya Negeri Sembilan (JHEAINS) ilimkamata mke na wanafamilia wa Shab wa Hizb ut Tahrir / Malaysia (HTM) huko Seremban, mnamo saa tano usiku Jumanne iliyopita. Kabla ya kukamatwa, nyumba yao ilipekuliwa na timu ya maafisa wa polisi wa JHEAINS katika operesheni ya pamoja na Polisi wa Royal Malaysian (PDRM) ambapo baadhi ya vitabu vilichukuliwa. Katika tukio hilo, Shab huyo hakuwepo nyumbani na alipigiwa simu na mkewe ambaye alieleza kilichotokea. Kupitia simu hiyo hiyo, aliombwa na afisa wa JHEAINS kurudi nyumbani mara moja. Mbali na mkewe, 45, na bintiye, 22, pia waliowekwa kizuizini ni wafanyikazi wake wawili, mmoja wao ni mpwa wake. Wale wote waliozuiliwa walipelekwa katika Kituo cha Da'wah ya Kiislamu, Paroi, kwa ajili ya kuhojiwa.

HTM Shab, Ndugu Jamaluddin Maidin Syed, 45, alipigiwa simu tena na kutakiwa kufika katika Kituo cha Da’wah ya Kiislamu. Kwa hiyo, alienda Kituoni huko mwendo wa saa nane unusu usiku na akawekwa kizuizini na JHEAINS mara moja. Wote walituhumiwa kutenda kosa chini ya Kifungu cha 50 cha Sheria ya Jinai ya Negeri Sembilan Shariah 1992 - "kutusi, kupuuza, n.k. Dini ya Kiislamu" ambayo inawajibika kulipa faini isiyozidi shilingi elfu tano au kifungo cha muda usiozidi miaka mitatu au vyote kwa pamoja inapopatikana hatia. Wote walihojiwa usiku na asubuhi na hawakuruhusiwa kulala. Baya zaidi, ombi la mkewe na bintiye la kuswali swala ya Isha lilikataliwa hadi saa kumi na moja unusu alfajiri. Mnamo saa kumi alfajiri, wafanyikazi wake wote waliachiliwa, huku mahojiano ya Jamaluddin Maidin Syed, mkewe na binti yake yakiendelea hadi jioni ya tarehe 27 Oktoba. Watatu hao baadaye waliachiliwa mwendo wa kumi na moja unusu kwa dhamana ya RM 2,500 kila mmoja na Mahakama Kuu ya Shariah ya Seremban.

Enyi JHEAINS! Hakika mumekiuka waziwazi sheria ya Kiislamu kwa kuvunja na kuingia nyumba ya mtu na kuchukua mali yake bila ya ruhusa. Mlijaribu kuwakosea heshima na kuwatisha wakaaji na kitendo chenu hicho hakika kilitokana na uongo usio na msingi. Je, mnajua kwamba makafiri wa Kiquraishi walipoizingira nyumba ya Mtume (saw) hawakuingia ndani ya nyumba yake (saw) kwa sababu bado walikuwa wanaiheshimu nyumba hiyo na wakaaji wake? Bado walikuwa na heshima na aibu. Walingoja nje ya nyumba hadi asubuhi kwa sababu heshima yao iliwakataza kuvunja na kuingia nyumba ya mtu kwa nguvu. Hata hivyo, hamna tena utu na aibu hiyo, kuvunja na kuingia nyumba ya watu wengine, kuchukua mali na kuwatisha mke na watoto wa wakaaji!

Sisi, Hizb ut Tahrir / Malaysia tunapinga vikali kukamatwa kwa mwanachama wetu na familia yake, na usakaji na unyang'anyi wa JHEAINS. Kwa hakika, ukamataji na unyang'anyi huu ni ukatili wa wazi na ukiukaji wa sio tu sheria za Kiislamu, bali pia sheria walizotunga wao wenyewe. Tuhuma za kuwa wanachama wetu wanaukashifu Uislamu chini ya kifungu cha 50 ni za kipuuzi kiasi kwamba hata mlima ungepasuka kwa kusikia uongo huo!

Huku akiwa hakutosheka na ukamataji huo, Mufti wa Negeri Sembilan katika maoni yake kwenye Gazeti la Harian Metro kuhusu kukamatwa kwa watu hao, alisema kwamba mafundisho ya Hizb ut Tahrir ni ya kupindukia na yanapingana na Ahlu Sunnah Wal Jamaah, na kusababisha mgawanyiko na kuathiri usalama wa taifa. Kwa hakika hatushangazwi na kauli hii kwani ni masimulizi na shutuma zile zile zinazotolewa na mamlaka za kidini katika majimbo mengine pia, ambazo tayari zimejibiwa na sisi na hakuna hata mmoja wao anayeweza kutoa jibu hilo na kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu (swt), hawataweza kulijibu mpaka Siku ya Kiyama, kwa sababu yale waliyoyatoa ni uzushi tu na uongo dhidi ya Hizb ut Tahrir.

Tunataka kusisitiza kwamba hatua ya JHEAINS imepitiliza zaidi kuliko hatua iliyochukuliwa na Idara ya Kidini ya majimbo mengine. JHEAINS ilikuwa imemkamata sio tu Shab wa Hizb ut Tahrir ambaye hakutenda kosa lolote, bali pia walimkamata mkewe, binti yake na wafanyakazi wawili. Tuhuma za JHEAINS kwamba mwanachama wa HTM na familia yake wameukashifu Uislamu pia ni shutuma kali. Kwa hakika, kumkamata mhubiri na kumchukulia mhubiri kama mhalifu, chenyewe ni kitendo kilichopitiliza cha mamlaka za kidini, bila kusahau katika hali ambayo upotovu na dhambi nyingi nchini zinapuuzwa na mamlaka za kidini.

Kuyatangaza mafundisho ya Hizb ut Tahrir kuwa ya misimamo mikali ni masimulizi tu yanayoenezwa na nchi za Magharibi ambazo sasa hivi ziko katika hofu ya miito ya Hizb ut Tahrir ya kusimamisha tena Shariah na Dola ya Khilafah, kwani mwito huu unaitikiwa na Waislamu wengi zaidi kote Duniani. Magharibi inajua kwamba njama zake zote mbaya na utawala wake juu ya ulimwengu wa Kiislamu utafikia mwisho na watapata somo linalostahiki kutoka kwa Khalifa wakati Khilafah itakaposimamishwa hivi karibuni. Kwa msingi huo, wanazuia kwa nguvu zote wito wa Hizb ut Tahrir, wakiwahamasiha vibaraka wao wote katika ulimwengu wa Kiislamu kuipiga vita  Hizb ut Tahrir, kwa kueneza uzushi, tuhma na uongo mbalimbali dhidi ya Hizb ut Tahrir, zikiwemo tuhuma za kuwa na siasa kali, misimamo mikali na ugaidi. Wakati huo huo, Magharibi inaendelea kuwasifu wenye msimamo wa wastani, maliberali, wana LGBT, wahubiri wa demokrasia, na hata watawala madhalimu katika ulimwengu wote wa Kiislamu; kwa sababu wote wako sambamba na maadili na maslahi ya Kimagharibi.

Tunapenda kusisitiza kwamba kukamatwa kwa wanachama wa Hizb ut Tahrir hakukufanyika isipokuwa kwa fatwa ya kisiasa iliyojaa kashfa na uzushi dhidi ya Hizb ut Tahrir. Kwa mara ya kumi na moja, tunapenda kuwakumbusha wakuu wa dini msije mkadhani kwamba kwa kukamatwa, kukashifiwa, uongo na ukatili wote mliowafanyia wanachama wa Hizb ut Tahrir, kutasimamisha au kupunguza kasi ya Da'wah yetu, badala yake, Da ́wah yetu itaendelea kuongezeka kwa vile tunaifanya ili tu kupata radhi za  Mwenyezi Mungu (swt), sio kupata radhi za mwanadamu. Tunatekeleza jukumu la kusimamisha Dini ya Mwenyezi Mungu (swt) hapa duniani macho yetu yakitazama raha za Akhera tu, tofauti na nyinyi mnaofanya kazi ya kuharamisha Daawah huku macho yenu yakitazama starehe za dunia pekee!

Enyi mamlaka za kidini! Kwa kuwa bado tunakutakieni kheri, hivyo tungependa kumalizia taarifa hii kwa vyombo vya habari kwa kipande cha ukumbusho, iwapo bado muna kipande cha ikhlasi na khofu ya Mwenyezi Mungu (swt):

 [إِنَّ الَّذِينَ فَتَنُوا الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ثُمَّ لَمْ يَتُوبُوا فَلَهُمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمْ عَذَابُ الْحَرِيقِ]

“Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua.” [Al-Buruj: 10].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Malaysia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Malaysia
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu