Afisi ya Habari
Malaysia
H. 28 Safar 1442 | Na: HTM 1442 / 01 |
M. Alhamisi, 15 Oktoba 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Shambulizi Ovu la Uzushi Dhidi ya Hizb ut Tahrir Ladhihirisha Ufisadi wa Kifikra wa Pande Zinazohusika
Kwa karibu wiki moja, Hizb ut Tahrir imekuwa ikishambuliwa kila wakati na kila aina ya kashfa mbaya na vyombo vya habari kufuatia mikutano ya waandishi wa habari iliyofanywa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maswala ya Dini ya Kiislamu ya Johor (mnamo 30/09/2020) na Mkuu wa Polisi wa Johor (mnamo 01/10/2020). Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Maswala ya Dini ya Kiisilamu ya Johor na Mkuu huyo wa Polisi wa Johor walikuwa wakizungumza kuhusu fatwa juu ya Hizb ut Tahrir, iliyotolewa na Kamati ya Johor ambayo ilikuwa imechapishwa katika gazeti rasmi la serikali mnamo 15/07/2019; fatwa ambayo ni mbaya kuliko fatwa kama hiyo iliyochapishwa katika gazeti rasmi la serikali na Selangor na Sabah. Fatwa hii miongoni mwa nyengine inasema kwamba Hizb ut Tahrir inaruhusu kubusu wanawake wa kando (wasio mahram), kwamba kutazama filamu ya ngono inaruhusiwa na kwamba Hizb ut Tahrir inatishia utulivu na usalama wa kitaifa. Mkuu wa Polisi wa Johor, katika mkutano wake na waandishi wa habari aliongeza kuwa Hizb ut Tahrir imeitaja serikali ya Malaysia kama ya kikafiri ambayo lazima ing'olewe kwa nguvu.
Vyanzo kadhaa vya habari, iwe ni runinga au magazeti, viliripoti mikutano ya waandishi wa habari (na fatwa hiyo) na idadi kadhaa yao vinaonekana kupatiliza fursa ya hali hiyo kwa kuongeza kashfa zingine ambazo hazijasemwa katika fatwa hiyo, vikiituhumu Hizb ut Tahrir kusema kwamba swala na zaka sio lazima mpaka Khilafah itakapo simamishwa, kwamba Waislamu wasiokuwa katika Hizb ut Tahrir wamepotoka, kwamba al-Qadha wa al-Qadar haziwezi kuaminiwa na kadhalika. Hali inazidi kuwa mbaya wakati wakuu wengine wa polisi, akiwemo Mkuu wa Polisi wa Malaysia mwenyewe, wamesukumwa na vyombo vya habari kujibu maswali juu ya Hizb ut Tahrir ambayo imetuhumiwa kuwa na kifungu katika rasimu ya katiba yake inayowalazimisha watoto wote wa kiume wa Kiislamu ambao wamefikia umri wa miaka 15 kuhudhuria mafunzo ya kisilaha.
Msemaji wa Hizb ut Tahrir / Malaysia amefanya mikutano miwili ya waandishi wa habari mtandaoni akijibu baadhi ya uzushi huo katika fatwa hizo, wa Mkuu wa Polisi wa Johor na pia vyombo vya habari. Kwa kuongezea, tunataka kurudia, na kusisitiza kama ifuatavyo:
1. Vyombo vya habari ni lazima viwe na utaalamu na viwe na uadilifu katika kuripoti. vilipaswa pia kuripoti majibu kamili kutoka kwa Msemaji wa Hizb ut Tahrir / Malaysia na sio tu kuripoti upande mmoja wa hadithi;
2. Licha ya kuhisi kuwa Kamati ya Fatwa ya Johor haitaondoa fatwa ya uzushi, bado tunataka fatwa hiyo iliyosemwa iondolewe, kwa faida yao wenyewe, haswa kesho Akhera;
3. Hizb ut Tahrir ni chama cha kisiasa cha kimataifa cha Kiislamu ambacho kimekuwa kikifanya kazi ndani ya Ummah huu tangu 1953 na kila mtu mwenye akili razini anajua kuwa kazi ya Hizb ut Tahrir ni ya kisiasa na ya kifkra na Hizb ut Tahrir inataka kuunganisha Ummah huu chini ya Khilafah na Hizb ut Tahrir kamwe haijihusishi na vurugu katika amali zake zozote, kinyume na kile kilichoelezwa katika fatwa hiyo na mkutano wa waandishi wa habari uliotajwa hapo juu.
Tunataka kuieleza vikali na bila ya kusuasua Kamati ya Fatwa ya Johor, kama tulivyo sema katika majibu yetu kwa Kamati ya Fatwa ya Selangor na Baraza la Fatwa la Sabah, kwamba fatwa hii dhidi ya Hizb ut Tahrir ni 'fatwa ya kisiasa' ili kuchafua taswira ya Hizb ut Tahrir na kusitisha Da'wah ya Hizb ut Tahrir ndani ya Ummah huu. Ajenda ya kuchafua sura ya Hizb ut Tahrir ili kuzuia Da'wah inayobebwa na Hizb ut Tahrir ni mfano wa ajenda ya kisiasa ya Makafiri wa Kimagharibi, kwani wanajua vizuri mno kuwa Khilafah ambayo Hizb ut Tahrir inaifanyia kazi, hivi karibuni itasimamishwa na itamaliza uongozi wao potofu wa kifikra, na ushawishi kwa Ummah huu. Kwa kushindwa kuikabili Hizb ut Tahrir kimfumo, wanageukia njama ovu, uzushi na kutunga hadithi za urongo kuhusu Hizb ut Tahrir. Mawakala wao miongoni mwa watawala wa Waislamu kisha wanafuata nyayo, wakiwa na matumaini kwamba Umma utaachana na Hizb ut Tahrir na fikra ya Khilafah.
Hadithi zote za urongo zilizobuniwa na mashambulizi maovu ya uzushi dhidi ya Hizb ut Tahrir ambayo yanafanyika kote ulimwenguni yanaonyesha ufisadi wa kifikra wa washambuliaji hawa katika kukabiliana na fikra na Da’wah ya Hizb ut Tahrir. Wanatarajia kuwa pamoja na njama zao ovu, uzushi na tuhma, Hizb ut Tahrir atasitisha Da'wah yake, kama vile Maqureishi Makafiri walivyotarajia na kumfanyia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Lakini wamesahau jambo moja ... kwamba Da’wah iliyo katika njia sahihi kamwe haiwezi kusimamishwa, badala yake, itaendelea kukua zaidi ya vile wanavyoweza kufikiria, mpaka Mwenyezi Mungu (swt) awape nusra yake wabebaji wake.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Malaysia
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Malaysia |
Address & Website Tel: |