Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Malaysia

H.  19 Jumada I 1441 Na: HTM 1441 / 05
M.  Jumanne, 14 Januari 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Sasa Ni Zamu ya Johor Kuituhumu Hizb ut Tahrir!

Mamlaka kadhaa za kidini nchini humu zinaonekana kupoteza muelekeo na taaluma katika kutekeleza uaminifu uliowekwa mabegani mwao. Lengo lao, linaonekana sasa ni kuzichochea harakati za Kiislamu ambazo hawakubaliani nazo, kutafuta kosa lolote kwa harakati hiyo, na ikiwa hawakuweza kupata kosa lolote, wanapanga njama ya kuichafua harakati hiyo. Hivi ndivyo viongozi wa kidini wa Johor wameifanyia Hizb ut Tahrir.  Baada ya majimbo mawili, Selangor na Sabah kutoa amri (fatwa) ya kuichafua Hizb ut Tahrir, sasa ni zamu ya Johor kufanya vivyo hivyo, wakifanya vibaya zaidi kuliko majimbo hayo mawili.  La hawla wa la quwwata illa billah.

Inasikitisha sana kwamba Kitengo cha Dini ya Kiislamu cha Jimbo la Johor (JAINJ) kilikuwa tayari kutumia misikiti yote kupitia Johor kama mahali pakueneza tuhuma na uongo juu ya Hizb ut Tahrir. Nyumba ya Mwenyezi Mungu (swt) ambayo usafi na heshima inapaswa kuhifadhiwa, imechafuliwa na JAINJ pamoja na tuhuma na uongo mbaya ambao kwamba umenasibishwa na Hizb ut Tahrir.  Inasikitisha sana wakati JAINJ ilikuwa tayari ishakumbushwa kuachana na khutbah kabla ya hapo, kupitia kumbukumbu ya maandamano na mkutano wa amani uliofanywa na Hizb ut Tahrir kwenye makao makuu yao, hata hivyo wanasisitiza, kana kwamba misikiti ni yao na wanaweza kufanya chochote ndani yake, pamoja na kuichafua! Minbari ya ijumaa, ambayo inastahili kutumiwa kuelimisha na kuhamasisha umma, ilitumiwa na JAINJ kama jukwaa la kisiasa kuwachafua wale ambao kwamba hawakubaliani nao.

Kwa kuongezea kuiga fatwa za kirongo za Selangor na Sabah, khutbah iliyotolewa siku ya Ijumaa, 10/1/2020 yenye kichwa, “Epuka mafundisho ya Hizb ut Tahrir” iliyokusanya maovu mingi na nukta za kipuuzi. Imetajwa katika khutbah kuwa nukta zote zinazohusiana na Hizb ut Tahrir zimetokamana na fatwa zilizotolewa na kamati ya fatwa ya Johor. Hili kwa kweli limetushitua sana, yawezekanaje bodi inayotarajiwa kujaa wanachuoni, iliweza kutoa kashfa na uongo dhidi ya Hiz ut Tahrir, bila kuthibitisha mwanzo au kukutana na Hizb ut Tahrir!? Je hivi ndivyo kamati ya fatwaa inavyotowa fatwa – bila uthibitisho, bila kufafanua uhalisi wa ukweli, bila kukutana na bila kushauriana na chama ambacho kinatakikana kutolewa fatwa juu yake? Je haingekuwa bora ikiwa kamati ya Johor Fatwa ingelituita mapema, kwa amani, kuuliza au kujadili juu ya mawazo na mafundisho yetu.

Miongoni mwa tuhuma ambazo Kamati ya Johor Fatwa na JAINJ walitoa kwenye khutbah hizo ni maoni ya Hizb ut Tahrir juu ya adhabu ya kaburi; Hizb ut Tahrir wanaamini kuwa Qadaa' na Qadar zilichukuliwa kutoka kwa falsafa ya Ugiriki na kuwa matendo ya mwanadamu hayana mahusiano yoyote na Qadaa' na Qadar ya Mwenyezi Mungu (swt); kuwa uongofu na upotevu hautoki kwa Mwenyezi Mungu (swt) bali ni kutoka kwa mwanadamu; kukataa Ta’wil ya aya za Mutashabihat; na kusema kuwa mtu yeyote anaweza kufanya ijtihadi; wanume na wanawake wako huru kupeana mikono na inaruhusiwa (Mubah) kubusu wanawake wasiokuwa-mahram bila kukusudia kufanya zinaa!!!

Kulingana na tuhuma zilizotolewa katika khutbha, ni wazi kuwa Kamati ya Johor Fatwa haikufanikiwa tu kufanya uchambuzi, na lau hata ingelikuwa imefanya, ilikuwa ni nusu, lakini pia walichukua uongo wa muda mrefu ambao umekuwepo katika dunia ya mitandao, iliyoundwa na wale wanaoichukia Hizb ut Tahrir. Kamati ya Johor Fatwa Ilipaswa kuja na kujadiliana na Hizb ut Tahrir badala ya kuchukua rasilimali kutoka kwa wale ambao ni maadui wa Hizb ut Tahrir! Hakika, Kamati ya Johor Fatwa inajuwa vizuri kuwa Afisi ya Hizb ut Tahrir iko wazi daima na kuwa wanachama wa Hizb ut Tahrir daima wako tayari kukutana nao, na kuwa wanaweza kuja wakati wowote ikiwa wanatafuta ukweli (haki), lakini kwa bahati mbaya, walichagua kufuata uongo (Batili).

Kana kwamba haitoshi, kupitia khutba Hizb ut Tahrir inatuhumiwa pia kuwa tishio kwa umoja wa umma na pia kwa amani na usalama wa kitaifa. Je hii ni aina gani ya dhana mbovu? Kwa kweli inatushangaza inawezekanaje kwa fatwa kutolewa kwa kutegemea dhana kama hii!? Mbali na kuwa ni uongo, pia ni kinyume na ukweli! Kwa zaidi ya miaka 20 tangu kuweko kwa Hizb ut Tahrir nchini Malaysia, tunashangaa ni wakati gani Kamati ya Johor Fatwa ilishudia kwamba nchi imekuwa katika msukosuko na machafuko yaliyosababishwa na Hizb ut Tahrir!

Kana kwamba haitoshi, maandishi ya khutbah hiyo yanaendelea na tuhuma na uongo kwa kuituhumu Hizb ut Tahrir kwa kusema kuwa lazima vita vitangazwe kwa watawala ambao hawatekelezi hukmu za Kiislamu. Kamati ya Johor Fatwa na vile vile JAINJ wanaonekana kupoteza fahamu wakati wa kutoa tuhuma hizo za kuchekesha. Madai haya yaonyesha wazi imani yao mbaya kwa Hizb ut Tahrir. Ikiwa tungeuliza ushahidi ikiwa kuna mtawala yeyote katika Johor, huko Malaysia au ulimwenguni kote, ambaye Hizb ut Tahrir wametangaza vita naye, au kuuliwa na Hizb ut Tahrir kwa sababu hawaku tekeleza hukmu za Kiislamu, basi hakika Kamati ya Johor Fatwa na JAINJ hawatoweza kutoa hata ushahidi mmoja, na hata wakikusanya wanadamu wote na majini kufanya hivyo!

Kwa wale Makhatibu ambao hawakuitoa khutbaH, tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu (swt) awalipe na awabariki na awape ujasiri wa kusimama imara kwa ajili ya ukweli. Kwa wale walioitoa khutbah kwa sababu yoyote ile, tunawaombea msamaha. Kwa Kamati ya Johor Fatwa, ambayo wanachama wake wanatakikana kuwa wasomi wa kweli na wataalamu, tunawashauri kuiondoa fatwa ili tuhuma hiyo isienee duniani ambayo mwishowe itarudi kwa bwana wake. Kwa hakika, tuhuma hiyo na uongo ambao umetolewa hautoleta wema wowote, si ulimwenguni, wala ahkera. Wacha tukapate furaha katika Akhera kwa kukutana na Mwenyezi Mungu (swt) bila kubeba dhambi za wale tuliowazulia uongo.

Abdul Hakim Othman
Msemaji wa Hizb ut Tahrir Malaysia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Malaysia
Address & Website
Khilafah Centre, 47-1, Jalan 7/7A, Seksyen 7, 43650 Bandar Baru Bangi, Selangor
Tel: 03-8920 1614
www.mykhilafah.com
Fax: 03-8920 1614
E-Mail: htm@mykhilafah.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu