Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Malaysia

H.  10 Jumada II 1441 Na: HTM 1441 / 06
M.  Jumanne, 04 Februari 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ewe JAIS! Je Uhalifu na Uovu wote huko Selangor Umemalizika Hadi sasa Unawaendea Walinganizi kama Wahalifu?

Bila kujihisi na hatia, bila ya aibu na bila kumuogopa Mwenyezi Mungu (swt), Kitengo cha Dini ya Kiislamu cha Selangor (JAIS) kimewashtaki Dada watatu wa Hizb ut Tahrir, pamoja na wengine wawili, katika Mahakama ya Chini ya Shariah ya Shah Alam mnamo 29/01/2020 kwa kosa la ‘kuwatukana viongozi wa kidini’. Wanne wao walikamatwa 28/07/2019 katika msako wa JAIS kwenye duka huko Shah Alam PKNS Complex, na mwengine mmoja alikamatwa t31/07/2019 wakati akihudhuria makao makuu ya JAIS kutoa taarifa. Walioshtakiwa walikuwa ni Kalsom Binti Abu, miaka 65, Norliahani Binti Abdul Basir, miaka 43 na Nor Hazan Binti Bachok, miaka 41. Wengine wawili walikuwa watoto wa mwenye duka, Nur Afiqah Fatnin Binti Mohd Latif, miaka 26, na Muhammad Arfan Firas Bin Mohd Latif, miaka 20 ambao walikuwa wakitunza duka wakati huo kwani wazazi wao walikuwa wameenda Hajj. Wao wote walishtakiwa chini ya Kifungu 12 (c) cha makosa ya jinai ya sheria ya (Selangor) iliyotungwa mwaka 1995, isipokuwa Kalsom Binti Abu ambaye pia alishtakiwa chini ya Kifungu 12 (b) cha sheria ile ile, ambacho kinabeba faini ya mwisho kabisa ya RM 3,000 au kifungo cha miaka miwili au zote mbili, juu ya kupatikana na hatia.

Licha ya kuwa aghlabu tumekuwa tukiikumbusha JAIS juu ya fatwa ya kashfa dhidi ya Hizb ut Tahrir iliyopelekea mashtaka haya, kama inavyotarajiwa, JAIS iliendelea na vitendo vyake. Huo ndio mtazamo wa JAIS ambao huupa mgongo ukumbusho na haimuogopi Mwenyezi Mungu (swt) kwa ukatili wao! Katika kukamatwa na kushtakiwa Muslimah wa Hizb ut Tahrir, JAIS ilikuwa tangu mwanzo, ikikiuka Hukm (Sheria ya Wahyi) wakati ilipotuma wapelelezi wake kupenyeza katika mpango huo kabla ya msako. Kitendo hiki cha kupeleleza (Tajassus) ni ukiukaji wa wazi wa sheria ya Mwenyezi Mungu (swt) katika Surah Al-Hujurat (49) aya ya 12. Kuwapeleleza Waislamu ni wazi kuwa imekatazwa na Mwenyezi Mungu (swt) na hili ndilo lililofanywa na JAIS, bila kuhisi hatia yoyote!

Kwa kuongezea, JAIS ilitekeleza zaidi ya mamlaka yake na kukiuka sheria wakati walipozichukua simu za Norliahani na Nor Hazan katika kipindi cha mchakato wa kuchukua taarifa. Uchunguzi wa maafisa wa JAIS pia walifanya vitendo vya kinyama kwa kuzungumza kwa ukali, kunyanyua sauti zao na kuwatishia akina Dada wa Hizb ut Tahrir wakati wakichukua taarifa.

Kwa kuongezea, mmoja wa Maafisa wa uchunguzi aliwatuhumu Dada wa Hizb ut Tahrir kama "wahalifu", tuhuma nzito sana, zilizotupiwa mtu ambaye bado hajapatikaniwa na hatia!!! Je chama kama hicho kinaweza kutarajiwa kusimamisha sheria!? Je chama kama hicho kinaweza kutarajiwa kusimamisha hukmu!? Je chama kama hicho kinaweza kuwakilisha Bodi ya kulazimisha sheria za kislamu!?  Kwa jinsi walivyotenda tangu mwanzo, haishangazi kuwa JAIS iko makini sana na imepoteza hofu yoyote ya kumuogopa Mwenyezi Mungu (swt) katika kushtaki Dada wa Hizb ut Tahrir.

JAIS hadi sasa imewasukuma ndugu saba wa Hizb ut Tahrir katika Mahakama ya sheria kwa kosa la kuwatukana viongozi wa kidini. Pamoja na shtaka la hivi karibuni juu ya Dada watatu wa Hizb ut Tahrir na wengine wawili, na kuifanya idadi hiyo kuwa kumi na mbili, walikamatwa na kushtakiwa mahakamani kama matokeo ya fatwa za kiongo zilizotolewa na Kamati ya Selangor Fatwa juu ya Hizb ut Tahrir. Kwa hakika, JAIS imepoteza aibu yake na kutomuogopa Mwenyezi Mungu (swt) kwa kuwasukuma walinganizi (Daie) mahakamani kwa makosa ya uongo! Ilikuwa ni kama hakuna uhalifu tena na wahalifu huko Selangor hadi JAIS inawafuatilia walinganizi na kuwafanya wahalifu! Wakati kiwanda kikubwa cha pombe bado kimesimama imara huko Selangor; wakati vikundi vya ukombozi huzidi hamu ya kutoa taarifa za uongo na kupanga mipango mbali mbali ya kueneza mafundisho na ushawishi wao;  wakati majanga ya kijamii yanazidi kuwa mabaya; wakati sauti za Makafiri zinaongezeka juu zaidi katika chuki zao za Uislamu; wakati wanasiasa wakizidi kuutenga Uislamu kutoka katika utawala wao – badala ya kufanyakazi kupigana na kubadili haya, JAIS badala yake inawinda Walinganizi kuwafanya wao wahalifu!

Mwisho, tungependa kueleza kuwa, kama JAIS inafikiria kuwa kuwakamata na kuwashtaki wanachama wetu itadhoofisha na kuizuia Hizb ut Tahrir kubeba Da’wah, JAIS imefanya kosa kubwa. Hakika, Da’wah hii ni ya Mwenyezi Mungu (swt) na yeye ndiye atakayeilinda. Atawalinda wale ambao wanaubeba Ulinganizi huu kwa dhati katika njia yake na yeye ndiye atakayehakikisha Ulinganizi huu unaendelea. Kila ulinganizi katika njia yake ukipata vizuizi zaidi, ndio unapanuka zaidi kwa mapenzi yake na nguvu zake. Hii ndio Sunnah ya Mwenyezi Mungu. Tayari ashampa ushindi Mtume wake (saw) na vizazi vya mapema licha ya juhudi kubwa za maadui wake kuusimamisha Ulinganizi, na ni Yeye, ambaye kwa mara nyingine tena, atakipa kizazi hichi cha sasa ushindi mkubwa bila kujali kiasi gani cha juhudi kimefanyika kuzuia Ulinganizi. Tofauti pekee ni kwamba, mwanzoni, Ulinganizi ulizuiliwa na Makafiri, lakini sasa hivi unazuiliwa na wale ambao wanadai kuwa wao ni Waislamu na wanadai kufuata muongozo wa Uislamu! La hawla wa la quwwata illa billah!

Abdul Hakim Othman
Msemaji wa Hizb ut Tahrir Malaysia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Malaysia
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu