Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  2 Rabi' II 1444 Na: 1444/02
M.  Alhamisi, 27 Oktoba 2022

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Harakati Ili Kubadilisha Utawala au Kubadilisha Rais Wake?

Mgogoro wa Misri uko kwenye Utawala Unaoitawala, Sio Rais Wake Tu  
(Imetafsiriwa)

Migogoro ambayo Misri inakumbwa nayo si mipya wala si matokeo ya sadfa. Badala yake, ni mkusanyiko wa migogoro, baadhi yake ikiburuza mengine, iliyosababishwa na urasilimali ulioitawala Misri kwa miongo kadhaa, na zana zake, wasaliti vibaraka. Kwa kukithiri kwa migogoro inayosababishwa na mfumo huo, ima kwanza kwa kuwepo kwake na kanuni na sheria batili inazozitunga au maamuzi ya watekelezaji wake, ambayo yanafuja mabaki ya mali za watu na kula mapato na juhudi zao. na kutokuwa na uwezo wa kupata suluhu zozote za kuiondoa nchi katika majanga yake. Bali, masuluhisho yake yote yamekuwa yakiwalemea watu kwa mizigo na migogoro zaidi, mpaka subira ya wale waliobakia katika watu wa Misri ikamalizika kwa mateso ya mfumo huu.

Kwa hivyo miito ya harakati mpya na endelevu انزل_11_11_حرر_بلدك#[Jitokeze 11/11 Ikomboe Nchi Yako], na kufanya damu itiririke katika mishipa ya mapinduzi yanaipa uhai mitaa ya Misri na kuondoa majivu kutoka juu ya makaa ya vijana wake, ambao mgongo wao uliwakishwa kwa kuambukizi ya dhulma na ukandamizaji wa serikali. Je, harakati hii itafanikiwa vipi na lini? Na je ni kipi hasa chenye ikomboa Misri? Na harakati yoyote inahitaji nini ili kufanikiwa?

Kwanza: Ni lazima tuelewe kwamba tatizo letu haliko kwenye utawala wa al-Sisi binafsi, licha ya kila kitu ndani yake, na wala hatutilii maanani yeye kuwa mwanajeshi na sio raia. Tatizo ni mfumo ambao al-Sisi anatawala na ambao kwao Abdel Nasser alitawala kabla yake, kisha Sadat na Mubarak, hadi Morsi. Kufeli kulifuatiwa na kufeli na migogoro, ambayo baadhi yake huburuza mengine, kwa hivyo suluhu yoyote inayojumuisha kuupa uhai utawala wenyewe na badala yake kubadilisha tu rais kama ilivyotokea huko nyuma ni kuyatibua mapinduzi na kupora matakwa ya vuguvugu hilo na kuregea tena mwanzo kabisa, kama ilivyotokea katika harakati za Januari 2011, ndiyo maana mfumo mzima lazima ung'olewe. Pamoja na zana na nembo zake zote.

Pili: Mwenye kuunga mkono utawala huu na tawala zote za vibaraka zinazotawala nchi yetu ni mkoloni kafiri Magharibi, ili wasiache utumwa wa utiifu na utegemezi na ili uporaji wake wa mali yake na ufukarishaji wa watu wake usikome. Ndio maana utiishaji wa Magharibi katika sura na aina zake zote na kila kinachopelekea hilo kifurushwe na kila anayeiwakilisha miongoni mwetu afukuzwe.

Tatu: Mapinduzi au vuguvugu lolote lisilobeba mradi mbadala wa ubepari wa kidemokrasia unaotawala nchi yetu na yasiyo ongozwa na wanaume wanaofahamu mradi mbadala na jinsi ya kuuleta madarakani na kuutekeleza kivitendo, ni harakati ambayo bila shaka itafeli tangu kuanzishwa kwake, na maadui zake watavuna matunda yake. Tumejaribu na kuona jinsi utawala wa vibaraka wa Marekani umerudi kwa ukali na uovu zaidi, hata baadhi ya watu wa kawaida wamelalamika juu ya enzi za Mubarak mhalifu!

Njia pekee ya mapinduzi yoyote kufanikiwa katika nchi za Kiislamu ni kwa kubeba mradi wa Ummah, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, na kuungwa mkono kwake na watu wenye nguvu na ulinzi, watiifu miongoni mwa watoto wa Ummah huu walio ndani ya majeshi. Kitu chochote chengine kando na hili, itakuwa ni kuzunguka katika mduara mbaya, na kuutolea utegemezi wa nchi kwa mkoloni Magharibi na kuendelea kuishi chini ya utiifu wake. Mradi huu ni ule ambao Hizb ut Tahrir inaubeba na kuwalingania watu wa Ummah kuubeba na kuukumbatia na kuutafutia nusra kutoka kwa wenye ikhlasi katika majeshi ili kuutekeleza kikamilifu kivitendo, kwa mapana na marefu, na wazo lake limekuwa ni rai jumla katika Ummah unaoipenda Dini yake na kutamani kuishi chini ya kivuli chake.

Enyi Wenye Ikhlasi katika Jeshi la Al-Kinana: Mnawajibika mbele ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa jinai zote za utawala huu. Ulikuwa jeuri dhidi ya Mwenyezi Mungu, Dini yake na waja wake pindi ulipokuwa salama kutoka upande wenu, kupitia mishahara, ruzuku, na marupurupu ambayo yanapofusha kwayo macho yenu, ambayo kwa hakika ni rushwa, ili ukutumieni kuwashambulia watu wenu na kuwezesha nchi za Magharibi kupatiliza fursa ya utajiri wao. Na mumeona jinsi wanavyoteseka watu wenu nchini Misri, na dhiki walizo nazo, basi kuweni njia ya wokovu wao na muwasaidie na muinusuru Dini yenu na kuweni upande wa Ummah wenu. Hizb ut Tahrir inauweka mradi huu mikononi mwenu huku mukiwa kwenye kizingiti cha wimbi jipya la mapinduzi, ili iwe ni njia mbadala inayofanikisha matarajio ya watu na kushughulikia matatizo yao yote kwa ufumbuzi wa kweli, sio udanganyifu na mangati mithili ya kile ubepari unachokuuzieni. Kwa hiyo, ubebeni, unusuruni kwa sababu ninyi ni watu wake na mna haki zaidi ya kuubeba. Wacheni uwe ndio hitaji lenu ambalo hamukengeuki nalo. Kwa hili mutapata radhi za Mola wenu, na ndani yake kuna wokovu wa Misri na Ummah kutoka katika makucha ya Magharibi, zana zake na mfumo wake uliooza. Basi acheni liwe ndio lengo lenu, huenda Mwenyezi Mungu (swt) akatimiza ahadi yake kupitia nyinyi, ili Khilafah Rashida ya pili isimamishwe kwa mikono yenu, hivyo mupate ushindi mkubwa.

[وَالَّذِينَ آمَنُواْ وَهَاجَرُواْ وَجَاهَدُواْ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَالَّذِينَ آوَواْ وَّنَصَرُواْ أُولَـئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقًّا لَّهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ]

“Na walio amini wakahama na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na walio toa mahala pa kukaa na wakanusuru, hao ndio Waumini wa kweli. Watapata msamaha wa Mwenyezi Mungu na kuruzukiwa kwema.” [Al-Anfal: 74]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu