Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  6 Rabi' II 1444 Na: 1444/03
M.  Jumatatu, 31 Oktoba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Enyi Watu wa Kinana: Uvumilivu wenu ni Udhalilifu na Kimya chenu ni Uhalifu Yapi Yatokea baada ya Mawimbi Mtawalia ya Ueleshaji?!
(Imetafsiriwa)

Mnamo Alhamisi asubuhi, Oktoba 27, 2022, Benki Kuu ya Misri ilipandisha viwango vya riba kwa pointi 200, wakati wa mkutano wa kipekee, hivyo kiwango cha maregesho ya amana na mikopo ya usiku mmoja kikawa asilimia 13.25 na asilimia 14.25, mtawalia, na taarifa ya Benki Kuu. Taarifa hiyo ilijumuisha aya muhimu ambapo ilisema: "Hatua za mageuzi zimechukuliwa ili kuhakikisha utulivu wa uchumi mkuu na kufikia ukuaji endelevu na shirikishi, na ili kufikia hili kiwango cha ubadilishanaji kitaakisi thamani ya Pauni ya Misri dhidi ya sarafu zingine za kigeni, kupitia usambazaji na mahitaji, ndani ya kiwango nyumbufu cha ubadilishanaji wa fedha.” Mara tu uamuzi huo ulipotolewa, pauni ilianza kushuka dhidi ya dolari kwa kasi, kwani bei ya dolari kwenye benki ilizidi pauni 22, baada ya kuwa thabiti kwa muda kwa pauni 19.65, na dolari inaendelea kuongezeka kila wakati. (Sky News Arabia, 10/27/22)

Afisa mkuu wa timu ya majadiliano ya IMF na Misri kuhusu mikopo mipya alitoa taarifa siku hiyo hiyo akielezea kukaribisha kwa timu hiyo kwa hatua za hivi majuzi zilizochukuliwa na mamlaka na utekelezaji wa mfumo nyumbufu wa kudumu wa viwango vya ubadilishanaji wa fedha. Hatua ya Benki Kuu ya Misri kwa mfumo nyumbufu wa viwango vya ubadilishaji fedha ni hatua muhimu na ya kukaribisha katika kutatua kukosekana kwa mizani ya nje ya usawa, kuimarisha ushindani wa Misri na kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni. Ahadi ya unyumbufu wa kudumu kwa kiwango cha ubadilishanaji katika mustakabali itakuwa sera ya msingi ya kujenga upya na kulinda unyumbufu wa muda mrefu wa nje wa Misri. (Jarida la HAPI, 10/27/22)

Utawala huu umefikia, katika nguvu na udhalimu wake, yale ambayo watangulizi wake hawakuyafikia, kana kwamba inaikimbiza Misri kwenye shimo. Mikopo hii iliyofuatana juu ya yale yaliyomo ndani yake katika riba na dhambi kubwa inayomkasirisha Mwenyezi Mungu Mtukufu, Magharibi haitoi kwa watawala wa nchi yetu bila ya masharti, bali inafungamanishwa na maamuzi ya kisiasa yanayoruhusu udhibiti wa utajiri wetu wa mali ghafi, mafuta  ... nk. Inafungua soko kubwa la bidhaa zake, na kuhalisia ni mikopo ya lazima ambayo Magharibi inawajibisha vibaraka wake kuomba na kutekeleza mapendekezo yanayoambatana nayo, maamuzi na sera za maafa na hatimaye kujisalimisha kwa nchi za Magharibi na makampuni yake kupora utajiri wa Misri. Mikopo hii ilikuwa na ingali ni chombo cha kikoloni mikononi Magharibi ambayo kwayo inaeneza ushawishi wake kwa nchi ambazo utajiri wake unapaswa kuporwa. Mikopo hiyo ni hatari sana kwa uhuru wa nchi na uamuzi wake wa kisiasa, na utawala na wanasiasa wake wanalijua hili na wanafahamu vyema hatari yake, lakini wanajua kwamba maamuzi ya mabwana zao ni faradhi kutekelezwa, hata kama ni juu ya maiti za watu wa Kinana. Juu ya hili, mikopo hii haiwapatii watu wa Misri chochote kutoka kwayo, haichangii maendeleo yao, na haiwapi chochote cha maisha ya staha ambayo serikali inazungumzia. Badala yake, wanaathiriwa tu na mizigo na wajibu unaoandamana nayo na sera mbaya zinazokula akiba zao na kuharibu juhudi zao.

Ueleshaji huu sio wa kwanza na hautakuwa wa mwisho, na ni uamuzi uliotangazwa katika utekelezaji wa sera za IMF zinazoruhusu makampuni ya nchi wahisani kupora zaidi utajiri wa nchi na ufujaji wa mali na akiba za wananchi wa Misri kwa utaratibu. Pengine ni sehemu ya mchakato wa kudhibiti ambao haujaisha, kwa watu wa Misri ambao wangali ni waasi na wangali wana matumaini ya wokovu kutoka kwa junta ovu na mfumo wake mbovu wa kibepari, na miito ya mapinduzi yaliyotangazwa ni mashahidi bora zaidi.

Hakika Misri, pamoja na mali, rasilimali, na neema zake, na nguvu zake kubwa za kibinadamu, haihitaji kabisa mikopo hii na sera na maamuzi yanayoambatana nayo. Misri ina rasilimali zinazotosheleza na kuitajirisha, na hata za kulisha dunia nzima kama ilivyo fanya huko nyuma. Inachohitaji Misri kihakika ni kutabikishwa kwa mfumo wa Uislamu (Khilafah), ili kuthibitisha uwezo wake kwa mtazamo wake sahihi wa fedha, utajiri na mali, wenye kuweka msingi wa dhahabu na fedha kama mbadala wa karatasi zote ambazo hazina thamani, hivyo sarafu ya dola ina thamani yenyewe ya kindani, hakuna mikopo ya riba, hakuna mfumko wa bei, na hakuna kuelea wakati huo, na mali imegawanywa kwa kigawanyo cha Mwenyezi (miliki ya umma, miliki ya mtu binafsi na miliki ya dola). Na inaonesha kuwa mali iliyozikwa, ikiwemo mafuta na vitu vyake, vyote ni mali ya umma ambayo dola hairuhusiwi kuitoa kupitia kuiuza, kuikodisha, zawadi, kutoa makubaliano ya uchunguzi na kadhalika. Badala yake, dola lazima isimamie uchimbaji wake yenyewe au kwa kuajiri mtu kufanya kazi hii kwa niaba yake. Na hivyo kuziba njia kwa makampuni ya Magharibi yanayopora utajiri huo, na dola hairuhusiwi kuuza mali hii kwa raia kama ilivyo ndani ya mali ya umma inayomilikiwa nao, bali ni lazima ifanye kazi ya kugawanya mali hii au mapato yake kati ya raia kwa usawa, bila kujali dini, rangi, jinsia au dhehebu.

Huu ndio uhalisia wa mali ambayo Magharibi inazipora kwa mikopo na makampuni yake, na serikali hii inapuuza kwa makusudi, huku ikiwalinda na kuwawezesha wezi wa mali na kunyamazisha midomo yote inayoihitaji.

Enyi Watiifu katika Jeshi la Kinana: Lau utawala huu usingesalimika kutoka upande wenu na ukakudhamini kimya chenu, haungesubutu kufanya vitendo kama hivyo, wala kudharau Misri na watu wake, wala usingepuuza haki na mali yake, na kwamba kwa kunyamaza kwenu mnawaangusha watu wa Misri mahali ambapo ni lazima muwasaidie, basi jiandaeni kuulizwa maswali na Mwenyezi Mungu Mtukufu mbele ya Mtume wake (saw), au kuweni upande wa Umma na muunusuru na muinusuru Dini yenu kwa kukata kamba za utawala huu na utiifu wake kutoka shingoni mwenu, na mshirikiane nao kusimamisha dola inayokata mikono ya Magharibi inayoichezea nchi hii, na kufunga milango ya mikopo na janga inayolileta, na kuiregesha Misri kama ngao kwa Ummah kama ilivyokuwa.

Enyi Watu wa Kinana: Hakuna wokovu kwenu ila kwa maregeo ya kweli kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutekeleza dini yake na sheria yake. Hakuna wokovu kwenu ila kwa njia ya mapinduzi ya kweli ambayo yanabeba mradi wa Uislamu unaokudhihirisheni, kufikia uadilifu na kheri ndani yenu, na kuhifadhi mali yenu.

Hakuna mbadala mbele yenu ila Khilafah kwa njia ya Utume itakayoweka ndani yenu uadilifu na usawa munaoutaka na itakayokuhuisheni na kuhuisha Kinanah yenu na kuiregesha kama ilivyokuwa ikiilisha dunia. Mradi huu umebebwa na Hizb ut-Tahrir pekee, basi kuweni na msaada na nusra, na mubebe pamoja nao mradi huu mtukufu, kwani ndani yake mna kheri yenu na utukufu wenu, na ndani yake mna wokovu wenu na wokovu wa Misri yenu na Ummah wenu, na mtayakumbuka tunayowaambieni, na sisi tunamkabidhi Mwenyezi Mungu mambo yetu.

[وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَى آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِمْ بَرَكَاتٍ مِنَ السَّمَاءِ وَالأَرْضِ]

“Na lau kuwa watu wa miji wangeli amini na wakamchamngu, kwa yakini tungeli wafungulia baraka kutoka mbinguni na katika ardhi. Lakini walikanusha basi tukawapatiliza kwa sababu ya yale waliyo kuwa wakiyachuma.” [Al-A’raf: 96]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu