Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  14 Shawwal 1444 Na: 1444/16
M.  Alhamisi, 04 Mei 2023

 Maoni kwa Vyombo vya Habari

Utiifu kati ya Uislamu na Ubepari
(Imetafsiriwa)

Aliyekuwa Mufti Mkuu wa Misri, Mkuu wa Kamati ya Masuala ya Kidini na Kamati ya Awqaf (Wakfu) Bungeni, Ali Gomaa alisema kuwa fahamu ya uraia katika zama za kisasa ni mkataba wa kijamii kati ya mtu binafsi na dola na fahamu hiyo ndiyo iliegemezwa fahamu ya Utaifa juu yake, ambayo inahusisha haki na wajibu wa mtu binafsi katika jamii. Wakati wa ushiriki wake, mnamo Jumatano jioni, katika kongamano lililoandaliwa na Kitivo cha Sheria katika Chuo Kikuu cha Alexandria chini ya kichwa "Uraia kati ya Ukristo na Uislamu", Gomaa aliongeza utambuzi wa fahamu hii katika historia ya Kiislamu ulikuja kupitia mifano kadhaa katika zama za ujumbe wa Muhammad na Khulafa'a ar-Rashidin, kwa njia ya taswira kadhaa katika jumii za Makka, Madina na Abyssinia. Alifafanua kuwa dola katika Uislamu ni dola ya kiraia na inatofautiana na dola za kidini na za kisekula, ambayo msingi wake ni mgawanyo wa madaraka ya bunge, mahakama na baraza la mawaziri, lakini maadamu sheria iko ndani ya mfumo wa Shariah ya Kiislamu, hii ina maana kwamba uraia ndiyo njia salama zaidi ya kuishi pamoja katika zama za sasa. (Al-Masry Al-Youm, 3/5/2023).

Uraia unamaanisha kwamba mtu binafsi ambaye anafurahia uanachama katika nchi anastahili fadhila ambazo uanachama unajumuisha. Na kwa maana yake ya kisiasa, uraia unamaanisha haki zilizohakikishwa na dola kwa wale wanaoshikilia utaifa wake, na wajibu uliowekwa juu yake; au unaweza kumaanisha ushiriki wa mtu binafsi katika mambo ya nchi yake, na hisia yake ya kuwa mmiliki. (Wikipedia) Uraia ni sawa na utaifa ulioasisiwa na serikali katika mfumo wa kibepari, kulingana na wao dola ndiyo inayotoa utaifa, na ndiyo inayoubatilisha.

Katika Uislamu, inalingana na at-Tabi’iah (raia wa Kiislamu), ingawa kuna mfanano kati ya at-Tabi’iah na utaifa, tofauti kati yao ni kubwa. At-Tabi’iah ni hukmu ya kisheria ambayo mtawala na mtawaliwa wako chini yake, na dola inaendelea katika hukmu zake kwa mujibu wa hukmu za Shariah. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَالَّذِينَ آمَنُواْ وَلَمْ يُهَاجِرُواْ مَا لَكُم مِّن وَلاَيَتِهِم مِّن شَيْءٍ حَتَّى يُهَاجِرُواْ]

“Na wale walio amini lakini hawakuhama, nyinyi hamna waajibu wa ulinzi kwao hata kidogo mpaka wahame.”[Al-Anfal: 72]. Kwa hiyo maana ya Ayah ni kwamba ikiwa wamehama, basi wewe umekuwa mlinzi juu yao, yaani wanabeba uraia wa dola ya Kiislamu, na dola ya Khilafah haina haki ya kumnyang'anya raia wake uraia.

Neno 'at-Tabi'iah' linamaanisha kuwepo kwa chombo cha utendaji kwa ajili ya mkusanyiko wa viwango, fahamu na ukinaifu, na kuwepo kwa watu wanaoshirikiana katika fahamu sawa na kuongozwa na hisia sawa, chombo hiki cha utendaji kinatekeleza mfumo mmoja kwa watu hawa. Itakuwa ni mfumo mmoja, fahamu moja, na hisia moja yenye chanzo kimoja, ambayo yote yanatoka kwenye Al-Aqidah (itikadi) ya jamii hii, Aqidah ya Kiislamu.

Uhusiano wa kila mmoja wa watu katika jamii hii na chombo hiki cha utendaji ni uhusiano wa Tabi’iah. Unajumuisha utiifu kutoka kwa watu, na kutoka kwa Dola, (Serikali) umoja wa mtazamo juu ya watu wake katika utawala, idara, mahakama, kusimamia mambo, na kadhalika. At-Tabi’iah ni utawala wa Kiislamu ambao kila Khalifa na watu wake hutekeleza wajibu wao wa kuwakurubisha kwa Mwenyezi Mungu (swt) katika kutafuta ujira na thawabu (malipo).

Hizb ut Tahrir imetayarisha rasimu ya katiba inayojumuisha ibara zinazoelezea At-Tabi’iah (uraia), ni nani anayeushikilia, na vifungu vyake ni vipi:

Ibara ya 5: Raia wote wa Dola ya Kiislamu wanafurahia haki na wajibu wa Shari’ah.

Ibara ya 6: Dola imeharamishwa kubagua hata kidogo watu binafsi katika masuala ya utawala, mahakama na usimamizi wa mambo au mfano wake. Badala yake, kila mtu anapaswa kutendewa kwa usawa bila kujali kabila, Dini, rangi au kitu chengine chochote.

Hili halifanyiki wala halifanywa isipokuwa katika Dola ambayo Hizb ut-Tahrir inaifanyia kazi usiku na mchana ikiwatafuta Maanswari (wenye kunusuru) kama Answari wa zamani ili kutoa bay’ah kwa Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw) na nusra kwa Dini yake.

Enyi Waadilifu katika Jeshi la Kinana: Kamba za watawala zinazozunguka shingo zenu ni dhaifu kuliko uzi wa buibui, basi zikateni, hakuna kinachotegemewa zaidi ya kamba ya Mwenyezi Mungu yenye nguvu, ziunganisheni kamba zenu kwa wafanyikazi wenye ikhlasi kuutabikisha Uislamu katika kumnusuru Mwenyezi Mungu (swt), Mtume wake (saw) na Dini yake ili wasimamishe dola yake ambayo ndani yake mna wokovu wenu na wokovu wa Ummah wenu, Mwenyezi Mungu akupeni ushindi na msimamishe Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, inayotabikisha Uislamu kwa uadilifu wake ili watu wazione sheria zake kuwa ni uhalisia wa kivitendo unaofumbatwa ili waingie katika Dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi, hakika utukufu na furaha itakuwa ni yenu endapo mtafanya hivyo, Mwenyezi Mungu akujaalieni muwe miongoni mwa watu wake na wasaidizi wake, Allahuma Amin.

[وَالَّذِينَ آمَنُواْ وَهَاجَرُواْ وَجَاهَدُواْ فِي سَبِيلِ اللهِ وَالَّذِينَ آوَواْ وَّنَصَرُواْ أُولَـئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقّاً لَّهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ]

“Na walio amini wakahama na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na walio toa mahala pa kukaa na wakanusuru, hao ndio Waumini wa kweli. Watapata msamaha wa Mwenyezi Mungu na kuruzukiwa kwema.” [Al-Anfal: 74]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu