Ijumaa, 24 Rajab 1446 | 2025/01/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  4 Dhu al-Qi'dah 1444 Na: 1444/17
M.  Jumatano, 24 Mei 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Jeshi la Al-Kinana ni Ngao ya Uislamu na Msaidizi wa Ummah Hivyo ndivyo lilivyokuwa na hivyo ni lazima Lirudi Kuwa
(Imetafsiriwa)

Hayat Washington ilisema kwenye tovuti yake, Jumatatu, 22/5/2023, kwamba vyombo vya habari vya Nigeria viliripoti kwamba Shirika la Miradi ya Huduma ya Kitaifa ya Wizara ya Ulinzi ya Misri inakusudia kuwekeza katika sekta ya kilimo katika jimbo la Ogun (magharibi). Kulingana na tovuti ya Remo TV, gavana mtendaji wa jimbo hilo, Dabo Abiodun, alipokea idadi ya maafisa wa Shirika la Miradi ya Huduma ya Kitaifa ya Misri, na kufanya mkutano nao katika mji wa Abeokuta, mji mkuu wa jimbo hilo. Gavana huyo alitangaza katika chapisho kwenye akaunti yake ya Twitter kwamba maafisa wa Utumishi wa Umma wa Kitaifa wa Misri wameelezea nia yao ya kuwekeza katika sekta ya kilimo katika jimbo hilo. Kwa mujibu wa tovuti hiyo, mkuu wa ujumbe wa Misri, Meja Jenerali Walid Morsi, alisema kuwa kifaa hicho kitalenga kukuza mazao (yenye faida) ya chakula na biashara ambayo yatasafirishwa kwenda nchi yao na sehemu zengine za ulimwengu.

Mbali na uwezekano wa uwekezaji huu na kwa nini haujaanzishwa nchini Misri, hata kama yanaonekana kuwa maswali ya kimantiki, utafiti wa kweli ambao lazima tuangalie katika habari hii ni dori ya majeshi na kazi yao halisi, na ni yapi madhumuni ya yale ambayo utawala hutoa kwa jeshi katika suala la faida ambazo mabepari wenyewe wamepunguza na kusukuma Mfuko wa Fedha wa Kimataifa kuingilia kati ili kulazimisha. Kuliondoa jeshi katika uchumi, jambo ambalo haujafanya hadi sasa na pengine hautafanya katika muda mfupi ujao kutokana na uzito wa jambo hilo na kupoteza uaminifu wa makamanda wa jeshi wanaomuunga mkono Sisi katika kutawala Misri.

Madhumuni ya utawala wa kutoa marupurupu haya kwa makamanda wa jeshi ni kuhakikisha uaminifu wao na kujipanga nyuma yake mbele ya harakati zozote zinazowezekana za watu wa Misri kutokana na sera mbaya zinazowahusu na maamuzi yake inayowatekelezea au kuwalazimisha kufanya, kama vile kuhamishwa kwa baadhi ya Wamisri kutoka kwa nyumba zao, kama inavyotokea huko Sinai au kuwalazimisha kuziuza na kuzitelekeza, kama ilivyotokea katika Pembetatu ya Maspero na inavyotokea huko Al-Warraq na kwengine, na kama itakavyotokea katika eneo lolote ambalo serikali itaona linafaa kwa uwekezaji. Sera hizi pamoja na utekelezaji wa ubepari ambao hautoi tena na wala hauna suluhu kwa matatizo ya watu, umeifanya migogoro hiyo kuwa mibaya zaidi, hadi ukusanyaji wa watu wa riziki zao za kila siku tu unachukuliwa kuwa ni wa kishujaa siku hizi, na kwa muendelezo wa sera ambazo matokeo yake yanajulikana kabla ya utekelezaji wake, na hatujui jinsi watu wanavyobeba matokeo yake, jambo hilo linaonya juu ya mlipuko. Jibu la dhahiri ambalo linacheleweshwa tu na watu kutoona njia badali ya kweli ya mfumo huu, ambayo ina uwezo wa kutatua shida zao.

Hivyo basi, tunaweza kusema kwamba marupurupu haya ni rushwa katika hali halisi, ambayo utawala huo unapofusha macho na nyoyo za viongozi wa jeshi na wale walio nyuma yao kutokana na dori yao halisi ya kuwalinda watu dhidi ya uvamizi wake, na kufanya kazi ili kufikia matarajio yao ya kweli ya maisha yenye staha ambayo hayawezi kupatikana chini ya urasilimali na ala zake za watawala vibaraka na hayawezi kupatikana isipokuwa kwa mfumo badali wa aina ile ile ya Aqidah (itikadi) ya watu na wenye masuluhisho ya kweli ya matatizo yao, ambayo yanapatikana tu ndani ya Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Dori halisi ya majeshi sio kuingia katika uchumi, viwanda, au kilimo, na dori yao ni kulinda mipaka, kuhifadhi dola, kulinda Aqidah yake, na kubeba Uislamu kwa ulimwengu kupitia da’wah na jihad, na kwa hivyo, jeshi la Misri halichezi dori lake, kinyume na ukweli kwamba marupurupu lililopewa kwa ukweli lazima yapewe watu wote, kwa hivyo hakuna kodi au ushuru wa forodha na ardhi inatolewa kwa watu na kumilikiwa nao kupitia kuilima ardhi, na dola haikusanyi thamani kutoka kwao, kwani hivi ndivyo Sharia ilivyoweka juu ya dola ya Kiislamu.

Enyi Wanyoofu katika Jeshi la Kinana: Kile ambacho utawala unakupeni hakitakutajirisheni na wala hakitakunufaisheni, bali kitakupelekeni kwenye maangamizo na kitakufanyeni washirika katika uhalifu wake mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi msikikubali na neno la msingi, na kwa jina la Mwenyezi Mungu, mna haki ambazo utawala unakunyang'anyeni kubwa zaidi ya kile unachokupeni. Ni vyema, mtafute kheri kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa ushindi kwa ajili ya dini yake inayong'oa mfumo huu wa utumwa kutoka shingoni mwenu na kuuweka utawala katika mikono ya wenye ikhlasi wanaofanya kazi ya kuutabikisha Uislamu na kusimamisha Khilafah Rashida ya pili. Mwenyezi Mungu ajaalie ufunguzi mikononi mwenu, ili mpate ushindi mkubwa duniani na Akhera.

[وَالَّذِينَ آمَنُواْ وَهَاجَرُواْ وَجَاهَدُواْ فِي سَبِيلِ اللهِ وَالَّذِينَ آوَواْ وَّنَصَرُواْ أُولَئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقّاً لَّهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ]

“Na walio amini wakahama na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na walio toa mahala pa kukaa na wakanusuru, hao ndio Waumini wa kweli. Watapata msamaha wa Mwenyezi Mungu na kuruzukiwa kwema.” [Al-Anfal:74]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu