Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  27 Muharram 1445 Na: 1445/01
M.  Jumatatu, 14 Agosti 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Uchaguzi Sio Suluhisho na Hautaleta Jambo Lolote Jipya, Hata kama Watu Wanaotekeleza Utawala Watabadilika na Wanajeshi Kuondolewa kwenye Orodha
(Imetafsiriwa)

Siku hizi, sauti zinamtaka Sisi ang’atuke na aondoke kwa salama kutoka kwa mandhari. Wakosoaji wa sera na maamuzi yake wameibuka kutoka kwa wale waliolelewa katika kukumbatia serikali hiyo na walikuwa miongoni mwa nguzo zake enzi ya Mubarak.

Katika mahojiano na The Independent, Hossam Badrawi alitaka taasisi ya jeshi iachilie kutokana na uwekezaji na ushindani, na kwa hiyo "kubaki mlinzi wa serikali na Katiba" na kudai uhamishaji wa madaraka, huku mbunge wa zamani Ahmed Tantawi akitangaza nia yake ya kugombea urais wa dola hii. Hii ilitanguliwa na ukosoaji kutoka kwa wapinzani nje ya nchi na wataalamu wa vyombo vya habari, pamoja na wale walio nyumbani, kama vile Imad Adeeb katika makala yake, "Udanganyifu kwamba" hali iko chini ya udhibiti"!" ya 28 Februari iliyopita. Sauti hizi kubwa hazingeonekana na kutangaza ukosoaji wao, wala wasingesubutu kupinga serikali na sera zake kutoka ndani ya nchi, wala kugombea urais, kama isingekuwa kwa idhini kutoka kwa serikali yenyewe na kama ingekuwa haijaridhika na hayo kwa sababu yanatumikia maslahi yake.

Kile tunapaswa kuamua tangu mwanzo ni kwamba mfumo sio mtu binafsi na hauwakilishwi na rais, serikali, au ala zozote za kutekeleza mfumo ambao kuwabadilisha, hakubadilishi mfumo na sera zake hazibadiliki. Badala yake, mfumo ni itikadi ambayo juu ya msingi wake dola imeasisiwa na kuamua muundo na mipaka yake, na ambao katiba, sera, sheria, na vifungu vyote vinavyotekelezwa katika serikali vinaibuka. Mubarak, Morsi, Sisi, au wengine huzitekeleza maadamu msingi unabaki ule ule na haujabadilika.

Utawala ambao umetawala Misri kwa miongo kadhaa, na ambao umesababishia watu mateso ni mfumo wa kisekula wa kidemokrasia, ambao watu waliasi ili kuubadilisha. Laiti isingekuwa Magharibi na vibaraka wake kugeuka na kuwadanganya kwa kubadilisha raisi wa serikali na kuibakisha serikali kama ilivyo, na hata kuizalisha upya kwa njia mbaya zaidi, ambayo ndio sababu watu wanateseka kutokana nayo, kwa zaidi ya muongo mmoja, wakati ambao wameonja janga la umaskini, bei za juu, uporaji, ukandamizaji, na udhalilishaji, pamoja na migogoro mibaya ya kiuchumi, ambayo inadhihirisha mapinduzi ya halisi ambayo jeshi wala polisi hawataweza kuyakabili. Pengine mabwana waliuona muhanga wa Sisi ili serikali iweze kusimama kwa kipindi chengine, hadi watakapopanga upya nyaraka na kuwadanganya watu wa Misri kwa mara nyengine tena.

Enyi watu wa Misri, Kinana: Hamuhitaji uchaguzi ambao hubadilisha tu raisi wa serikali na kuibakisha serikali fisadi kama ilivyo, wala hamuitaji demokrasia inayoshindwa ambayo kwayo inatawaliwa. Badala yake, munahitaji utambuzi wa kweli wa hukmu za Uislamu na kwamba ndio pekee ambao unaoboresha hali yenu na unaokutoeni kutokana na kile mulichoko ndani yake. Kwa hivyo, kuweni pamoja na ndugu zenu, Mashababu wa Hizb ut Tahrir na muwahimize watoto wenu wanyoofu ndani ya majeshi kuwanusuru, ili kusimamisha Khilafah Rashida kwa Njia ya Ume, kwani ndiyo izza ya ulimwengu huu na Akhera.

Enyi Wenye Ikhlasi katika Jeshi la Kinana: Wakati Ibn Taymiyyah, Mwenyezi Mungu amrehemu, alipofungwa gerezani huko Damascus, mtekelezaji adhabu akamwendea na kumwambia: "Nisamehe, Sheikh wetu, kwa kuwa nimeamrishwa." Ibn Taymiyyah akamwambia: "Naapa kwa Mwenyezi Mungu, lau kama isingekuwa kwa sababu ya wewe, wasingekuwa madhalimu." Na tunasema, twaapa kwa Mwenyezi Mungu, lau isingekuwa kwa sababu yenu, serikali isingekuwa dhalimu kwa watu wenu nchini Misri, wala isingewakandamiza, wala isingeweza kuwafanya watumwa kama inavyofanya sasa. Twaap kwa Mwenyezi Mungu, nyinyi ndio mtawajibika Siku ya Uwasilishwaji, siku mtakapoitwa.

[وَقِفُوهُمْ إِنَّهُمْ مَسْئُولُونَ] “Na wasimamisheni. Hakika hao watasailiwa.” [As-Saffat 37:24], kwa hivyo tayarisheni jibu lenu. Naapa kwa Mwenyezi Mungu, munakabiliwa na machaguo mawili; Kubaki munahema nyuma ya ulimwengu na starehe zake za kupita, kisha mutakutana na Mwenyezi Mungu hali mumeufelisha Ummah wenu, kwa hivyo aibu na majuto yaliyoje siku hiyo! Au muwe ubavuni mwa Ummah wenu na Dini yenu, na kuipa Nusrah (msaada) Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa Njia ya Utume.

[وَالَّذِينَ آمَنُواْ وَهَاجَرُواْ وَجَاهَدُواْ فِي سَبِيلِ اللهِ وَالَّذِينَ آوَواْ وَّنَصَرُواْ أُولَئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقّاً لَّهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ]

“Na walio amini wakahama na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na walio toa mahala pa kukaa na wakanusuru, hao ndio Waumini wa kweli. Watapata msamaha wa Mwenyezi Mungu na kuruzukiwa kwema.” [Al-Anfal 8:74]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu