Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  29 Muharram 1445 Na: 1445/02
M.  Jumatano, 16 Agosti 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Serikali ya Misri Haitabanni Uislamu na Haihifadhi Hudud zake, na vile vile Al-Azhar
(Imetafsiriwa)

Nchini Misri, matukio ya kuwalazimisha wale wanaosilimu kutoka imani ya Kikubti kuukana Uislamu yanatokea mara kwa mara, mara nyingi hufanywa na kanisa na vyombo vya usalama, kwa ukimya kamili au wa karibu kamili kutoka kwa Mashiakhet Al Azhar (uongozi wa Al Azhar). Tukio la Maryam Sameer Fayez, Wafaa Qostantin, Camellia Shehata, na wengine kulazimishwa kuritadi ni mfano tu wa mwelekeo huu uliotabanniwa na kanisa na vyombo vya usalama vya serikali. Serikali hii haipingi kuritadi kwa Waislamu na haisiti kuwalinda wale wanaotangaza kutokuamini kwao Mungu au kuikashifu Quran, Sunnah na wapokezi wa Hadith. Bali, inawapa nafasi za kuukashifu Uislamu na kujaribu kuzua shaka miongoni mwa watu. Hili linadhihirika katika kesi za Islam Al-Behery, Ibrahim Issa, na wengineo. Hivyo basi, sisi katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Misri tunasisitiza yafuatayo:

1- Jukumu la kulinda dini ni jukumu la dola, na ni moja ya malengo makubwa ya Shari’ah tukufu (sheria ya Kiislamu). Inachukua nafasi ya kwanza kuliko ulinzi wa uhai, mali, na heshima.

2- Serikali ya Misri yenyewe inajulikana kwa kuupinga Uislamu na Waislamu, kwa hivyo haimkiniki hata kidogo kutetea matukufu ya Uislamu. Shirika la Kimataifa la Kumnusuru Mtume wa Uislamu lilivituhumu vyombo vya usalama kwa kumkabidhi dada Mariam kwa kanisa hilo. Shirika hilo lilisema, "Baada ya Mariam Sameer Fayez kutangaza kusilimu huko Al-Azhar na kutangaza kusilimu kwake kwenye vyombo vya habari, usalama wa Misri ulimkabidhi kwa kanisa, na kusababisha Waislamu kushangazwa na tukio la uchochezi na dhulma ambapo Mwanasheria Naguib Gabriel anatokea kanisani pamoja na dada yetu Mariam, na kutangaza kurudi kwake katika kulikumbatia kanisa - kwa nguvu na kwa lazima."

3- Ripoti za Kimagharibi zimethibitisha kuwa Uislamu ndio dini inayokuwa kwa kasi zaidi duniani. Ni wazi kwa mtu yeyote mwenye akili timamu kwamba sababu ya haya ni mwongozo wao kwa usahihi wa Uislamu kwani unakinaisha akili, kuafikiana na maumbile ya mwanadamu, na kuleta utulivu moyoni. Kwa hiyo, kile ambacho kanisa linafanya ni upotoshaji dhidi ya mwelekeo huu. Majaribio ya kuwashurutisha Waislamu kuritadi yalikuwa na lengo la kuimarisha juhudi hizi kupitia ushirikiano wa tawala za vibaraka watiifu kwa vita vya msalaba vya Magharibi. Sababu hasa iliyo nyums ya kuimarishwa kwa washirikina wa Kikristo dhidi ya Dini ya Tawhid (dini inayompwekesha Mungu) ni serikali yenyewe.

4- Tuna uhakika kwamba wanadamu kwa ujumla wake wanauhitaji sana Uislamu mtukufu, na hitaji hili si la kiroho pekee, linalojaza pengo la kiroho lililopo miongoni mwa Wakristo na wengineo. Ni hitaji pia la mfumo mpana wa maisha unaosimamia mambo yao kulingana na yale aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu, kuwakomboa kutoka katika dhulma na ulafi wa ubepari ambao umeifanya dunia kuwa pori, ambapo wenye nguvu huwala wanyonge. Kwa sababu hiyo, licha ya wingi wa mali, watu wengi duniani wamefukarika.

5- Kinachowazuia wasiokuwa Waislamu kote duniani, wakiwemo Wakristo wa Kanaan, wasiingie katika Uislamu ni kutotabikishwa kwake ndani ya Dola yake. Kwa hiyo, kukaribia kusimamishwa kwa Khilafah, Bi idhni Allah, kupitia utabikishaji wake wa Uislamu ndani ya nchi na uenezaji wake kwa watu walio nje ya nchi, kutawaongoza watu kusilimu kwa mawimbi. Hivyo, kuwanusuru watu binafsi kama Dada Maryam na wengine waliolazimishwa kuritadi kunahitaji kuondolewa kwa serikali ya kisekula inayotawala na kusimamishwa kwa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume badala yake. Hili ndilo tunalowalingania watu wa Kinana, hasa wale wenye ikhlasi ndani ya majeshi yake wajitahidi kwalo.

[إِذَا جَاءَ نَصْرُ اللهِ وَالْفَتْحُ * وَرَأَيْتَ النَّاسَ يَدْخُلُونَ فِي دِينِ اللهِ أَفْوَاجاً * فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَاسْتَغْفِرْهُ إِنَّهُ كَانَ تَوَّاباً]

“Itakapo kuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ushindi, (1) Na ukaona watu wanaingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi, (2) Zitakase sifa za Mola wako Mlezi, na umwombe msamaha; hakika Yeye ndiye anaye pokea toba. (3)” [An-Nasr 1-3]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu