Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  28 Safar 1446 Na: 1446/08
M.  Jumatatu, 02 Septemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Je, Barabara ya kuelekea Quds inapitia Mogadishu?!
(Imetafsiriwa)

Mnamo siku ya Jumamosi, Waziri Mkuu wa Misri Dkt. Mostafa Madbouly alithibitisha uungaji mkono usioyumba wa Misri kwa taifa ndugu la Somalia na kujitolea kwake katika kuimarisha umoja wa nchi hiyo. Alibainisha kuwa “kipindi kijacho kina ahadi kubwa kwa watu wa Somalia.” Madbouly alisema, “Kufikia umoja wa Somalia na kuunga mkono ndugu zetu wa Somalia katika awamu hii ni mojawapo ya vipaumbele vya juu vya dola ya Misri,” akiongeza kuwa dhamira hii inaonekana kupitia “ziara rasmi za ngazi ya juu kati ya pande zote mbili katika kipindi cha nyuma.” Waziri Mkuu alisisitiza kujitolea kwa Misri kutoa “msaada unaohitajika kwa ndugu Somalia katika nyanja zote.” (Sky News, 1/9/2024).

Kauli hizi na misimamo thabiti inatukumbusha Iran na chama chake nchini Syria walipoipa kisogo Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, na kuwaruhusu Mayahudi kueneza ufisadi huku wakifanya mauaji dhidi ya watu wa Syria waliokuwa wanamuasi dhalimu Bashar, kibaraka wa Marekani. Walinyanyua kauli mbiu, “Njia ya kuelekea al-Quds inapitia Aleppo, Qalamoun, na miji mingine ya Syria!” Halikadhalika utawala wa Misri umejitia uziwi kwa jinai za Mayahudi katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina na kutuma askari wake nchini Somalia. Je, sasa itanyanyua kauli mbiu, “Njia ya kuelekea al-Quds na Gaza inapitia Mogadishu?” Je, utawala wa Misri una uwezo wa kutuma watu na silaha Mogadishu lakini hauna uwezo wa kuwapeleka Gaza? Au ni usaliti tu, ulaji njama, uadui dhidi ya Uislamu na Waislamu, na utiifu kwa ukafiri na makafiri, wanaoongozi miongoni mwao wakiwa ni Mayahudi?

Chini ya kichwa cha habari “Silaha za Misri nchini Somalia: Je, Makabiliano na Ethiopia yanakaribia?” BBC iliripoti mnamo tarehe 30/8/2024: “Saa chache baada ya ndege mbili za kijeshi za Misri zilizojaa silaha na vifaa vya kijeshi kutua Somalia, taarifa ya Ethiopia yenye maneno makali ilitolewa, ikishutumu jirani yake Mogadishu kwa kuharibu eneo hilo. Taarifa ya Ethiopia haikutaja moja kwa moja jina la Misri, lakini ilisema kwamba ‘nguvu zinazojaribu kuchochea taharuki kwa malengo ya muda mfupi lazima ziwe na matokeo mabaya,’ ikiashiria uwezekano wa kuongezeka kwa taharuki katika Pembe ya Afrika Wataalamu kutoka Misri na Ethiopia waliozungumza na BBC walikubali kwamba ‘hakuna makabiliano ya moja kwa moja yatatokea kati ya Cairo na Addis Ababa,’ ingawa mtaalamu wa programu za Afrika katika Chatham House jijini London alionya kwamba ‘mgogoro huo unaweza kuongezeka na kusababisha matukio zaidi yasiyotarajiwa.’”

Ethiopia pia ilitangaza kuwa Musa Bihi Abdi, Rais wa Somaliland, alipokea hati za utambulisho za Teshome Shunde Hameto, balozi mpya aliyeteuliwa wa Ethiopia katika eneo hilo, katika hatua inayoongeza taharuki kati ya nchi hizo tatu: Misri, Somalia na Ethiopia.

Uhalisia wa mgogoro katika Pembe ya Afrika ni kwamba unawakilisha mzozo wa madaraka kati ya Marekani, ambayo inashikilia mamlaka, na Uingereza, ambayo inajaribu, kupitia wateja wake nchini Imarati, kupata nafasi au kupambana na uwepo wa Marekani huko. Mtazamo wao umekuwa katika eneo la Somaliland, ambalo lilitangaza uhuru. Ushiriki wa Misri nchini Somalia, utoaji wake wa silaha na msaada wa kijeshi, na uimarishaji wa uhusiano wa kibiashara, kiuchumi na uwekezaji haulengi kukabiliana na Ethiopia au kutatua mzozo wa maji unaohusiana na Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance (GERD). Utawala wa Misri uliachana na suala la maji uliporuhusu kujengwa kwa bwawa hilo, ambalo lingeweza kusababisha maafa kwa Misri na Sudan, huku Ethiopia ikipata hasara kidogo.

Ili kuliona jambo hilo kwa uwazi zaidi, tunahitaji kuregea nyuma kidogo: Mkataba wa pande tatu ulitiwa saini miaka michache iliyopita kati ya Ethiopia, DP World (zamani Dubai Ports International), na Mamlaka ya Bandari ya Somaliland mnamo Machi 1, 2018, kuipatia DP World. asilimia 51 ya hisa katika Bandari ya Berbera, huku Ethiopia ikipata 19%, na 30% iliyobaki chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Bandari ya Somaliland. Makubaliano mapya kati ya Imarati, Somaliland, na Ethiopia yanaeleza kuwa DP World itakuwa na jukumu la kusimamia na kuendeleza bandari ya Berbera, licha ya pingamizi na ukosoaji wa Wasomali, Waarabu, na kimataifa kuhusu makubaliano haya mapya ya Addis Ababa. Mwanzoni mwa mwaka huu, Addis Ababa ilitangaza kusainiwa kwa mkataba wa makubaliano na eneo lisilotambulika la Somaliland kukodisha kilomita 20 pambizoni mwa bandari ya Berbera kwenye Ghuba ya Aden, na kuipa njia ya Bahari Nyekundu kwa miaka 50 kwa madhumuni ya kibahari na kibiashara, kwa kubadilishana na kutambua Somaliland kama nchi huru. (Dhat Masr, 28/1/2024)

Rais wa zamani wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo aliishutumu Imarati kwa kudharau ubwana wa kitaifa wa nchi yake kutokana na hatua yake ya kuanzisha kambi za kijeshi katika maeneo yenye uhuru nusu kama Somaliland na Puntland bila kushauriana na serikali ya shirikisho, pamoja na kuunga mkono tawala za kikanda zinazotafuta uhuru. Mizozo hiyo iliongezeka baada ya bunge la Somalia kupitisha sheria mwezi Machi 2018 inayotaka kusitishwa kwa shughuli zote za kiuchumi na kijeshi za UAE nchini humo. Mnamo Aprili mwaka huo huo, mzozo uliongezeka wakati mamlaka za Somalia ziliponyakua vilivyokuwa ndani ya ndege ya Imirati iliyokuwa imebeba takriban dolari milioni 10 pesa taslimu, ikidai kuwa ilikusudiwa kuvuruga shughuli katika Somaliland na Puntland. (Raseef22, 20/12/2023)

Harakati za Imarati katika eneo hilo ni kwa niaba ya Uingereza na zinalenga kupanua ushawishi wake, ambao bila shaka utakabiliwa na wateja wa Marekani nchini Somalia, Ethiopia, Misri na kwengine. Hili linaufanya mzozo kati ya Marekani na Uingereza juu ya ardhi zetu na rasilimali zake, huku damu ya Ummah ikiwa ndio mafuta yanayotolewa kafara kwa manufaa ya dola za Magharibi. Uwepo wa Ethiopia nchini Somaliland na kuingia kwa Misri katika hali ya mizozo iliyopo kunalenga kuisukuma Uingereza na vibaraka wake nje ya mlingano au kuwalazimisha kufanya kazi ndani ya muundo wa mipango ya siku za usoni ya Marekani kwa eneo hilo. Hii ina maana ama kuondoka kwa Uingereza kutoka kwenye kinyang'anyiro au kupunguzwa kwake hadi kushindania tu utawala na Marekani, kuilazimisha kukubali dori iliyoainishwa na Marekani kwa ajili yake na vibaraka wake. Uhalisia wa kusikitisha ni kwamba Bahari Nyekundu na pwani ya Somalia zimekuwa uwanja wa dola za Magharibi kugombea udhibiti, huku zikizungukwa na nchi za Kiislamu ambazo tawala zake, kwa bahati mbaya, zinatii amri za nchi za kikafiri za Magharibi na kupigana chini ya bendera yake.

Utawala wa Misri kwa haraka ulikimbilia Somalia kusini, kuashiria vitisho na maonyo kuelekea Ethiopia, licha ya kila mtu kujua kwamba hautafanya lolote na hautasubutu kurusha risasi hata moja kwa Ethiopia au bwawa lake. Uwepo wake huko ni kwa matakwa ya Marekani na kutumikia maslahi yake, kama inavyofanya huko Gaza, kuizingira, kushiriki katika kuua watu wake, na kusimama kama kizuizi kati ya jeshi la Misri na wajibu wake wa kuikomboa Palestina na kunusuru watu wake. Haya, ni huku wakiwa ndani ya umbali wa pua na mdomo, damu yao ikimwagwa huku wakiililia Misri na jeshi lake mchana na usiku bila msaada au nusra yoyote!

Umoja wa ardhi za Somalia na nyinginezo kwa hakika ni baraka, lakini umoja huo hautakuja kwa mapenzi ya Marekani, wala kwa kufanya uratibu nayo, wala chini ya mamlaka ya vibaraka wake. Umoja wa kweli unaweza kupatikana tu chini ya Uislamu na dola yake. Kinachohitajika zaidi kwa Misri na jeshi lake ni kuwanusuru watu wanaodhulumiwa na kuikomboa Palestina kutokana na umbile nyakuzi linalokalia kimabavu ardhi ya Kiislamu, ambalo lazima lipingwe na kung'olewa bila kuchelewa.

Enyi Wenye ikhlasi katika Jeshi la Kinanah: Miradi na maneno matupu ya utawala yanakula juhudi zenu katika yale ambayo hayatawanufaisha nyinyi duniani, wala kuwaokoa Akhera. Badala yake, inakuzuieni na wajibu wa ukombozi wa Ardhi Iliyobarikiwa na nusrah ya watu wake, ambayo kwayo mtaulizwa mbele ya Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama. Kwa hivyo, tayarisheni jibu lenu kwa Mwenyezi Mungu, au uondoeni utawala huu, jitakaseni na uchafu wake na khiyana yake, na itangazeni dola inayotabikisha Uislamu miongoni mwenu na kuubeba ulimwenguni kama ujumbe wa uongofu na nuru. Hii ni dola inayokusukumeni kuelekea kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu katika dunia hii na Akhera, kuyakusanya majeshi yenu ili kuzikomboa ardhi zote za Kiislamu, si Palestina pekee, na kuwanusuru wanaodhulumiwa ndani yake. Dola ya Kiislamu inayomridhisha Mwenyezi Mungu, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal:24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 
http://hizb.net/
E-Mail:  info@hizb.net

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu