Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  20 Rabi' II 1446 Na: 1446/10
M.  Jumatano, 23 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kuikomboa Palestina na Kuwanusuru Watu Wake Ni Jukumu la Lazima kwa Jeshi la Kinanah – Misri
(Imetafsiriwa)

Kufuatia vitendo vya kihalifu vya Mayahudi na uvamizi wao dhidi ya watu wetu katika Ardhi Iliyobarikiwa, pamoja na juhudi zao za kuudhoofisha Ummah na kuzima ari ya upinzani kwa kuua viongozi na wapiganaji wenye ushawishi, kuwakandamiza watoto wasio na hatia, wanawake, wazee, hata wagonjwa na waliojeruhiwa, tunathibitisha kwamba ukweli kuhusu Ummah huu uko wazi. Unaweza kuwa mgonjwa, lakini haufi; haukukusudiwa kuangamia. Badala yake, uko karibu na ushindi utakaorudisha heshima na hadhi yake chini ya Uislamu na dola yake. Wakati huo, Mayahudi hawatapata mbingu ya kuwa chini yake wala ardhi ya kuwategemeza, wala Magharibi ya kuwalinda, kwani hapo Magharibi itawatelekeza na kujiweka mbali na jinai ambazo imezishajiisha na kuziidhinisha kwa muda mrefu.

Tunaukumbusha Ummah kwamba kadhia ya Palestina ndio shina lake na linapaswa kubaki katikati ya mazingatio yake. Wajibu wa halali kuhusu matendo ya umbile la Kiyahudi haupaswi kufungika kwa kulaani au kupinga pekee; badala yake, inatoa wito wa hatua za dhati na za kivitendo ili kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa.

Dori ya Misri, pamoja na uwezo wake wa kijeshi na kimkakati, isiishie kwenye upatanishi kati ya watu wa Palestina na Mayahudi. Badala yake, dori lake ni kuliondoa kabisa ubile hilo la kutisha, kuitakasa Ardhi Iliyobarikiwa na uchafu wao milele.

Enyi Askari wa Kinanah: Nyinyi ni kizazi cha Salah al-Din, ambaye aliikomboa Al-Quds kutoka kwa Wapiganaji Msalaba, na warithi wa Sultan Qutuz na Sultan Baybars, na majeshi yao ambayo yaliwasitisha Mongoli kusonga mbele, na kuwazuia kwa kuwashinda. Mumekuwa ngao kwa Ummah huu na chanzo cha msaada. Timizeni wajibu wenu na mushike aliyokuamrisheni Mwenyezi Mungu. Muna uwezo wa kweli wa kuikomboa Palestina na kusaidia watu wake kwa muda wa masaa machache. Jiondoleeni watawala wa madhara ambao wanakuzuieni kutekeleza wajibu na heshima hii adhimu mpaka muwe na wema unaostahiki tu wale wanaoisimamisha Raya (bendera) ya Mtume (saw) kwa uaminifu, wanaoulinda Ummah, na wanaolinda maeneo yake matukufu bila ya kulegeza kamba haki zake.

Wakataeni watawala hawa na mikataba yao yote batili. Ipeni nusrah (uungaji mkono) Hizb ut Tahrir kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, kwani itakutakeni muikomboe Palestina na kuyatakasa matukufu yake. Tunamuomba Mwenyezi Mungu akujaalieni kuwa askari wake, Jeshi la Kinanah.

[وَمَا لَكُمْ لاَ تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاء وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَـذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيّاً وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيراً]

“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako” [Surat An-Nisa:75]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 
http://hizb.net/
E-Mail:  info@hizb.net

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu