Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  2 Jumada I 1446 Na: 1446/11
M.  Jumatatu, 04 Novemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Enyi Wanajeshi wa Misri (Kinana): Ni lini Mtaifuta Aibu ya Utawala wa Kihaini na Kuosha Mikono Yenu kutokana Nao?
(Imetafsiriwa)

Siku chache zilizopita, utawala wa Misri ulikanusha kupokea meli ya mizigo katika bandari ya Alexandria ikiwa imesheheni shehena za silaha na vilipuzi kwa ajili ya umbile la Kiyahudi, licha ya kuwepo ushahidi mkubwa kwamba serikali ya Misri iliipokea, kuwezesha kuwasili kwake, na kutoa msaada unaohitajika na mahitaji mpaka shehena yake ifikie umbile hilo nyakuzi ili kukamilisha mwendo wake wa kuua watu wetu katika Ardhi Iliyobarikiwa. Jambo hilo halikuishia hapo, na mabishano hayo hayakwisha hadi watu walipoona manuari ya umbile nyakuzi ikipitia kwenye Mkondo wa Suez, ikiwa imebeba bendera ya Misri ubavuni mwa bendera yake. Waliiona na kuiangalia kwa macho yaliyojaa hasira kwa serikali inayowazingira watu wetu mjini Gaza, inayomuunga mkono muuaji wao, na hata kushiriki katika kuwaua.

Katika kisingizio kibaya zaidi kuliko dhambi lenyewe, vinywa vya serikali vilijitokeza kuhalalisha kupita huku kwa kudai kwamba Mkondo wa Suez ni njia ya maji ya kimataifa chini ya makubaliano ya kimataifa ambayo Misri haiwezi kuzuia meli yoyote kuvuka, hata ikiwa ni ya nchi yenye uadui, hata ikiwa ni manuari inayonyanyua bendera yake ubavuni mwa bendera ya Misri wakati wa kupita huko, kana kwamba utawala huo unawakejeli watu na kuwaudhi kwa vitendo vyake na kuwachokoza kwa tabia yake kana kwamba inawazoma!

Makubaliano ya kimataifa yanazifunga tu dola vibaraka zilizo chini ya ufuasi, na hayazifungi dola imara zenye kumiliki ubwana, hasa ikiwa yanagongana na maslahi yao. Ndio maana tunauona utawala wa Misri ukihalalisha unyenyekevu na utiifu wake kwa makubaliano ya kimataifa, na iwapo mikataba hii inagongana na maslahi ya Marekani, tutaikuta inanguruma na kudai ushujaa na kuitisha ushujaa ambao haina.

Msimamo wa serikali si wa ajabu au wa kushangaza; msimamo wake unajulikana, kama ambavyo daima imekuwa mlinzi mwaminifu wa umbile la Kiyahudi lililonyakua Ardhi Iliyobarikiwa, na hili liliimarishwa na mkataba wa uhaini na uliotangazwa wa uhalalishaji mahusiano uitwao Camp David.

Kinachoshangaza kweli ni msimamo wa wale wanaokaa kimya kuhusu udhalilishaji wa utawala huu na uhaini wake wa wazi ambao vyombo vya habari haviwezi tena kuficha, bali uhalalishaji wao umekuwa mbaya zaidi kuliko uhalifu wenyewe.

Wajibu wa Misri na jeshi lake ni kukataa makubaliano yote ya kihaini, kuanzia na makubaliano ya usafiri kupitia mkondo huo, kupitisha Makubaliano ya Camp David na kumalizia na makubaliano ya biashara na kiuchumi yaliyofuata, na kutangaza vita kamili dhidi ya umbile nyakuzi hadi ukombozi wa Palestina yote. Tunajua kwa yakini kuwa hivi ndivyo kila askari wa jeshi la Misri (Kinana) anatamani, na hakuna kinachomzuia kufanya hivyo au kusimama baina yake na kulifanikisha hili isipokuwa utawala wa unyenyekevu unaolidhibiti jeshi na kulifanya kuwa mtumishi wa umbile hilo nyakuzi.

Enyi Wanajeshi wa Misri (Kinana): Mulikuwa na mungali ni ngao kwa Ummah na silaha mkononi mwake, basi regesheni uhuru wenu, unganeni na Ummah wenu, kateni kamba za watawala wanaokuzungukeni, na uachaneni na fadhila, vyeo, ​​na mishahara yao. Wekeni mikono yenu katika mikono ya wale watakuongozeni kwenye Pepo ambayo upana wake ni kama mbingu na ardhi, na mubebe pamoja nao hamu ya Ummah wenu na murudishe nao mamlaka yake chini ya kivuli cha Khilafah Rashida kwa juu ya njia ya Utume, ambayo itaitakasa Ardhi Iliyobarikiwa kutokana na Mayahudi kupitia nyinyi, basi njooni kwenye silaha na mafanikio.

[وَاتَّقُواْ فِتْنَةً لاَّ تُصِيبَنَّ الَّذِينَ ظَلَمُواْ مِنكُمْ خَاصَّةً وَاعْلَمُواْ أَنَّ اللهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ]

“Na jikingeni na Fitna ambayo haitowasibu walio dhulumu peke yao kati yenu. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.” [Al-Anfal:25]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 
http://hizb.net/
E-Mail:  info@hizb.net

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu