Jumatatu, 25 Jumada al-thani 1447 | 2025/12/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi: Dkt. Muhammad Al-Umda Hammad

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, kwa nyoyo zilizoridhika na amri ya Mwenyezi Mungu, macho yanayobubujika machozi, na huzuni kubwa, inaomboleza mmoja wa mashababu wake aliyebeba ulinganizi wa kuregesha maisha kamili ya Kiislamu; kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, Mwenyezi Mungu amsamehe: Dkt. Muhammad Al-Umda Hammad

Soma zaidi...

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Wamzuru Katibu Mkuu wa Chama cha Wanasheria katika Jimbo la Al-Jazirah

Mnamo Jumanne, 2 Disemba 2025, ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, ukiongozwa na Mhandisi Mahdi Muhajir, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, na akifuatana na Ustadh Omar Ibrahim, pia mwanachama wa Hizb ut Tahrir, na Mhandisi Walid Kamil, walimtembelea Ustadh Imad Ismail Muhammad Ahmad, Katibu Mkuu wa Chama cha Wanasheria katika Jimbo la Al-Jazirah, afisini kwake Wad Madani.

Soma zaidi...

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Wakutana na Mkuu wa Chama cha Wanasheria katika Jimbo la Bahari Nyekundu

Mnamo Jumatatu, 1 Disemba 2025, ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, ukiongozwa na Ustadh Nasser Ridha, Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan, akifuatana na Ustadh Abdullah Ismail, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan, walimtembelea Dkt. Imad al-Din Muhammad Hamdallah, mkuu wa Chama cha Wanasheria katika Jimbo la Bahari Nyekundu, afisini kwake Port Sudan.

Soma zaidi...

Sera ya Elimu Baina ya Kufeli kwa Dola ya Kisasa na Ruwaza ya Khilafah Rashida

Sera ya elimu nchini Tunisia, kama moja ya nguzo za dola ya kisasa, imefeli, na mageuzi yanayorudiwa rudiwa hayajafanikiwa. Watoto wetu wamekuwa chini kabisa katika orodha ya kimataifa, na shule na vyuo vikuu vyetu viko nje ya uainishwaji, huku makumi ya maelfu ya wanafunzi wakiacha shule kila mwaka na kutupwa mitaani, ili kumezwa na ukosefu wa ajira, dawa za kulevya, mashua za vifo, na vikundi vya uhalifu, hadi kila mtu atakaposhuhudia ufisadi wa mtaala wa elimu na kufeli kwa matokeo yake, bila kusahau kutengwa kwa walimu na kuwaacha chini kabisa katika ngazi ya mshahara.

Soma zaidi...

Trump, Kupitia Azimio la Umoja wa Mataifa na kwa Msaada wa Watawala Waislamu, Anajiandaa Kuiweka Gaza na Eneo la Ash-Sham Chini ya Udhibiti wa Moja kwa Moja wa Kikoloni

Wakati wowote Amerika inaposhindwa kufanya jambo peke yake, hutumia mwavuli dhalimu wa Umoja wa Mataifa. Azimio la kishetani nambari 2803, lililoundwa kukandamiza upinzani wa Palestina, ni hila ya hivi karibuni ya Farauni wa leo, Trump. Kulingana na azimio hili ovu lililopitishwa tarehe 17 Novemba, ambalo serikali ya Pakistan ililipigia kura kwa aibu chini ya amri ya Trump, utawala wa Gaza utawekwa chini ya “Bodi ya Amani (BoP),” inayoongozwa binafsi na Farauni Trump. Azimio hilo hilo lililopitishwa tarehe 17 Novemba linatoa mamlaka kwa “Kikosi cha Kimataifa cha Utulivu,” kinachojumuisha wanajeshi kutoka nchi za Kiislamu, kulinda umbile la Kiyahudi na kupokonya silaha upinzani wa Palestina. Kivitendo, hili litakigeuza kuwa “Kikosi cha Ulinzi cha Israel” kinachofanya kazi chini ya amri ya Trump. “Bodi hii ya Amani (BoP)” na muundo wake wa usalama unaoambatana nayo itasimamia Gaza hadi tarehe 31 Disemba 2027, pamoja na uwezekano wa kuongezwa muda.

Soma zaidi...

Pakistan, Nchi Safi, Haiwakaribishi Wala Haiwasalimu Vizazi vya Khiyana vya Wasaliti

Baada ya kimya cha wafu makaburini cha serikali za vibaraka zinazobebesha mzigo ardhi za Waislamu, kuhusu mauaji ya Kiyahudi mjini Gaza kwa zaidi ya miaka miwili, vibaraka wa Amerika na Uingereza, washirika wa Mayahudi, walianza kuchukua hatua na kuwa wachangamfu katika kutekeleza mpango wa Trump wa kufilisi kile kilichobaki cha upinzani huko Palestina, kukandamiza na kuua watu mjini Gaza, na kubomoa kile ambacho Mayahudi hawakubomoa cha mawe. “Jenerali anayependwa zaidi wa Trump” Asim Munir alitembelea Jordan mnamo 26 Oktoba, na kwa badali yake, mnamo 16 Novemba 2025, Mfalme Abdullah II bin Al-Hussein, Mfalme wa Ufalme wa Hashimiya wa Jordan na Kamanda Mkuu wa Vikosi vya Wanajeshi wa Jordan, alitembelea Pakistan, akifuatana na binti yake Salma binti Abdullah II bin Al-Hussein, na ujumbe wa maafisa wa kiraia na kijeshi wa Jordan.

Soma zaidi...

Vikosi vya Pakistan Lazima Vitumwe Kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, Sio Kutimiza Ndoto za Adui wa Mwenyezi Mungu (swt), Trump, na Mayahudi!

Kutumwa kwa vikosi vya jeshi la Pakistani Gaza kuwanusuru watu wake na kupigana na Mayahudi ambao wameendelea na operesheni ya mauaji ya halaiki huko, tangu tarehe 7 Oktoba 2023 hakukujadiliwa kamwe, kwa kisingizio kwamba Gaza iko mbali, na kwamba wajibu wa Sharia wa kuinusuru unawaangukia wale walio karibu zaidi. Lakini mara tu bwana wa serikali ya Pakistan na adui wa Mwenyezi Mungu (swt), Trump, alipoamuru serikali hii kutuma vikosi ili kufikia ndoto zake mjini Gaza, ghafla Pakistan ikawa nchi jirani na Gaza, na vikosi vya jeshi la Pakistan vimewekwa tayari kufanya operesheni za kijeshi nje ya mipaka ya kitaifa ya Pakistan. Hivyo uongo wa serikali hii ulifichuliwa kuhusu kutoweza kwake kutuma vikosi vya jeshi kuwanusuru watu wetu mjini Gaza.

Soma zaidi...

Mahouthi Wawakamata Mashababu wa Hizb ut Tahrir kwa Kufichua Mkataba wa Trump!

Mnamo Ijumaa, 21/11/2025, kundi la Mahouthi katika Jimbo la Ibb liliwakamata wanachama wawili wa Hizb ut Tahrir, ndugu: Osama Muhammad Mas’ad Al-Wurafi (umri wa miaka 19) na Ibrahim Muhammad Mas’ad Al-Wurafi (umri wa miaka 15) kufuatia usambazaji wao wa toleo lililotolewa na Hizb ut Tahrir lenye kichwa: “Trump Anawaongoza Wafuasi Wake miongoni mwa Watawala katika Ardhi za Waislamu Kwenye Mkataba wa Fedheha na Aibu, Wakiinamisha Vichwa Vyao Nyuma Yake kwa Kuiweka Gaza Hashem chini ya Usimamizi na Ukoloni!” Toleo hili lilisambazwa nchini Yemen na nchi nyingi za Waislamu.

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu