Ijumaa, 24 Rajab 1446 | 2025/01/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  27 Dhu al-Hijjah 1441 Na: 1441 / 89
M.  Jumatatu, 17 Agosti 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Wako Wapi Wajukuu wa Muhammad bin Qasim, Wahamasishe Jeshi Kutokana na Vilio vya Naseema Bano na Dada Zake wa Kiislamu Wanaonyanyaswa katika Kashmir Iliyo Kaliwa?!

Huku akiangazia ubakaji wa halaiki uliofanywa na jeshi la India mnamo 1991 katika vijiji viwili vya Kashmir Iliyo Kaliwa, Waziri wa Shirikisho anayehusika na Haki za Kibinadamu Dkt. Shireen Mazari mnamo 15 Agosti 2020 alitangaza, "Ni kwa nini Afisi ya Kigeni haikuyakabili mashirika mengine ya kimataifa na mashirika ya haki za wanawake yanayopigania haki za wanawake ili kufichua unyama huu?" Huku akifichua nyufa ndani ya serikali juu ya kupuuzwa kikamilifu kwa Kashmir Iliyo Kaliwa, ambapo imechochoa hasira kubwa kwa Waislamu wa Pakistan, Waziri huyo wa Shirikisho anayehusika na Haki za Kibinadamu ni lazima atangaze kufeli kikamilifu kwa wizara yake mwenyewe kuleta mabadiliko yoyote madhubuti kwa wanawake wa Kashmir Iliyo Kaliwa. 

Hakika, serikali ya Bajwa-Imran imefeli hata kulinda haki za hata mwanamke mmoja kutoka Kashmir Iliyo Kaliwa, kupitia mkakati wa makosa wa kulisihi sanamu la jiwe la Umoja wa Mataifa. Ni mwezi mzima sasa tangu ombi la dhamana la mwanamke wa Kashmir mwenye umri wa miaka 57, Naseema Bano, kukataliwa na mahakama moja ya eneo la Kashmir Iliyo Kaliwa na India mnamo 14 Julai 2020. Alikamatwa na jeshi la India na polisi katika operesheni ya pamoja iliyofanywa wiki ya mwisho ya Juni. Nyumba yake ilivamiwa, binti yake kupigwa na vyombo vyake vya thamani kuporwa na majeshi ya Dola ya Kibaniani. Alikamatwa chini ya sheria maarufu ya UAPA kwa mashtaka ya kutoa msaada wa vifaa na makao kwa wapiganaji wa Kashmir, ambao wanachukuliwa kama "magaidi" na Dola hiyo ya Kibaniani. Familia ya Naseema imehusika katika mapambano ya ukombozi wa Kashmir tangu 1990. Wengi wa jamaa za Naseema ima wako gerezani au wameuwawa mashahidi, akiwemo kijana wake mdogo ambaye aliuwawa shahidi na jeshi la India mnamo 2018, huku kijana wake mkubwa akiwa gerezani. Afya yake inazidi kuzorota kwa hali mbaya za gereza, huku akiwa tayari anaugua shinikizo la damu na kisukari.

Kesi ya Naseem Bano iko mbali na kesi ya mama mmoja Muislamu wa Kashmir aliyetendewa unyama kama huo, Tangu uzingiraji wa Modi wa Kashmir Iliyo Kaliwa uanze mnamo 5 Agosti 2019. Ikiwa kweli watawala wa Pakistan wanawachukulia wapiganaji wa Kashmir kama wanaopigana kwa haki kwa ajili ya ukombozi, basi ni nini kina wazuia kutuma majeshi yetu yaliyo tayari kuwasaidia, badala ya kulisihi sanamu la jiwe? Ni kipi kinachowazuia wao, wakati ambapo watoto wetu wazuri ndani ya majeshi wanahisi uchungu wa dada zetu wanaonyanyaswa na wana zaidi ya uwezo wa kuikomboa Kashmir? 

Rahisi, watawala hawa ni watumwa wa mabwana wa kikoloni wanaosisitiza mazoezi ya Pakistan ya kujizuia mbele ya ukuaji wa unyanyasaji wa Dola ya Kibaniani.

Ni chini ya kutawala kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kumefichua kwamba majeshi huhamasishwa na vilio vya wanawake. Kwa vilio vya mwanamke mmoja Muislamu, aliye nyanyaswa na dhalimu Raja Dahir mjini Sindh, jeshi la Muhammad Qasim lilihamasishwa, na kumaliza utawala huo wa Raja Dahir. Ni jukumu letu kuwasihi baba zetu, kaka na watoto wetu ndani ya jeshi, walio wakali juu ya heshima ya mwanamke wa Kiislamu, kutoa nusra kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah wa Njia ya Utume, ili waweze kumaliza uvamizi wa unyanyasaji pasi na kuchelewa zaidi.

Mwenyezi Mungu (swt) asema,

 (وَمَا لَكُمْ لاَ تُقَاتِلُونَ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱلْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ ٱلرِّجَالِ وَٱلنِّسَآءِ وَٱلْوِلْدَانِ ٱلَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَآ أَخْرِجْنَا مِنْ هَـٰذِهِ ٱلْقَرْيَةِ ٱلظَّالِمِ أَهْلُهَا)

“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu.” [Surah An-Nisa'a 4:75].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu