Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  1 Muharram 1442 Na: 1442 / 01
M.  Alhamisi, 20 Agosti 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Katika Kuikumbuka Hijra ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) Yenye Kunukia na Kuzaliwa kwa Dola ya al-Madina al-Munawwara

Kila mwaka katika siku hii, Tarehe Moja Muharram al-Haraam, Waislamu hukumbuka kumbukumbu inayonukia kutoka katika historia ya hadhara yao tukufu; kumbukumbu ya kuzaliwa Ummah bora ulioletwa kwa watu, kupitia kusimamishwa Dola ya Haki duniani, Dola ya Mtume Muhammad (saw), Dola ya al-Madinah al-Munawwarah. Ni ndani ya dola hii tukufu ambapo Mtume wa Rehma (saw) alitabikisha Ujumbe (Risaalah) ambao Mwenyezi Mungu (swt) alimtumiliza kwao. Hivyo, yeye (saw) aliwatoa watu kutoka katika kiza cha upotovu hadi katika nuru ya Uislamu. Hakika, Waislamu wana haki ya kukumbuka siku hii, kwa kutafakari maana za Hijra ya Mtume inayonukia, ambapo tutaja baadhi yake, kama ifuatavyo: 

Kwanza: mwenye kutafakari juu ya tukio hili la Hijra, kwa fikra angavu, fungamano la Hijra na lile lililoitangulia linakuwa wazi. Hakika, Hijra lilitanguliwa na Bay'ah ya Pili ya Aqabah, ambapo Watu wenye kumiliki Nguvu na Ulinzi wa Al-Aws na Khazraj walitoa ahadi ya utiifu (Bay'ah) kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), ya kumpa Nusra (Usaidizi wa Kinguvu) ili kusimamisha Dola ya kwanza ya Uislamu. Hakika, kwa anaye tafakari kwa makini Sera ya Mtume atagundua jambo hili. Hivyo basi, natuzingatieni maneno ya al-Abbas bin Ubaadah al-Answari, akihakikisha Ahadi ya Utiifu shingoni mwa Maanswari (Wenye kunusuru), "Enyi watu wa Khazraj! Je, mnatambua kile mnachojifunga kwacho katika kutoa ahadi ya usaidizi wenu kwa mtu huyu? Inamaanisha kupigana na kila mtu, mwekundu na mweusi. Ikiwa mnadhani kuwa mtakapopoteza mali yenu na watukufu wenu kuuwawa, mtaachana naye, basi fanyeni hivyo sasa, kwani naapa kwa Mwenyezi Mungu (swt) mtakapo fanya hivyo itawaletea fedheha hapa duniani na kesho Akhera. Lakini, ikiwa mnadhani kuwa mtakuwa wakweli kwa ahadi yenu, hata kama mtapoteza mali zenu na watukufu wenu kuuwawa, basi mchukueni, kwani naapa kwa Mwenyezi Mungu (swt) hilo litawanufaisheni hapa duniani na kesho Akhera." Maanswari wakajibu, "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), nyosha mkono wako ili tukupe bay'ah." Hivyo Mtume (saw) akanyosha mkono wake na wakampa bay'ah. Hijra ilitokea baada ya Maanswari kuingia katika Uislamu, kama itikadi na mfumo kamili wa maisha, na sio tu kama ibada za kibinafsi na tabia njema (akhlaq). Lau kama Uislamu ungekuwa ni ibada za kibinafsi na tabia njema pekee, Maqurayshi kamwe hawangeupinga, na kuwatesa Waislamu kwa ajili ya Dini yao. Lau kama Uislamu ungekuwa ni ibada za kibinafsi na tabia njema pekee, Makruseda wa Kimagharibi hawangeanzisha vita vya Kimsalaba ili kuumaliza Uislamu na Waislamu, katika zama zote hadi leo, ambapo kampeni za kimsalaba zinauhujumu Uislamu halisi, Uislamu wa Kisiasa, Uislamu unaosimamia siasa na utawala kama mfumo kamili wa maisha. 

Pili: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alifahamu kazi yake, aliyotumwa kuja kuifanikisha, hivyo punde tu tukio la Hijra lilipomalizika, punde tu Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alipotia mguu wake katika ardhi ya al-Madina, yeye (saw)  aliweka sheria za dola mpya kwa mujibu wa Wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) ulivyo hitaji kutoka kwake. Hivyo, yeye (saw) alijenga Msikiti kuwa ndio makao makuu ya dola na yeye (saw) aliandika Saheefa ambayo ilikuwa ndio katiba ya dola hiyo, iliyofafanua haki na majukumu na kudhibiti mahusiano. Yeye (saw) alianza kutekeleza hukmu za Shariah ili kudhibiti kivitendo mahusiano na kutekeleza adhabu za Kisheria juu ya wale waliokiuka hukmu za Kiislamu. Al-Madina ilikuwa ni dola iliyo ongozwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), aliyekuwa ndiye kiongozi wa dola kwa maana yake halisi. Hivyo, pindi Wahyi ulipomshukia (saw), aliufikisha kwa wadhifa wake kama Mtume, huku yeye (saw) akitekeleza kivitendo kwa wadhifa wake kama kiongozi wa dola. Hivyo, hukmu za Jihad, njia ya kivitendo ya Kisheria ya ubebaji Uislamu kwa watu, zilipitishwa. Hivyo, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alifunga bendera za vita na kutuma vikosi katika safari za kivita, akidhihirisha kwa kila mtu ujio wa umbile jipya la kisiasa mjini al-Madina, akionyesha nguvu na kutangaza waziwazi ufahari wa dola hii. Hatua zote hizi ambazo yeye (saw) alizichukua, zinaashiria kuwa Dini Tukufu ya Uislamu ambayo Mtume (saw) aliileta, imekuja kuwatawala watu kwa Uislamu na sio tu kuwalingania katika Uislamu. Hivyo basi, Waislamu ni lazima pia washerehekee kuingia kwa watu katika Uislamu makundi kwa makundi, ndani ya kivuli cha utawala wa Uislamu.     

Tatu: Ni juu ya Waislamu wa leo kuiregesha Hijra katika maana yake halisi. Hivyo Waislamu nawabebe Da'wah ya Uislamu pamoja na Hizb ut Tahrir, waukukute ulimwengu kutoka mabegani mwao, hadi Waislamu wairudishe Hijra katika mahali na lengo lake linalostahiki. Ni juu yao kuifanya kadhia ya kuhukumu kwa Uislamu kadhia yao nyeti. Hakika, ni juu yao kuufanya usimamishaji wa Khilafah ya Pili kwa Njia ya Utume hamu yao kubwa, kiasi ya kuwa Radhi za Mwenyezi Mungu (swt) ndio lengo kuu la malengo yao yote. Ni kwa kupitia hili, na hili pekee, ndipo maana na lengo la Hijra yatapatikana katika nafsi za Waislamu. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

 [إِنَّا لَنَنصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ]

“Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watapo simama Mashahidi.” [Surah al-Ghaafir 40:51]. Ama kwenu nyinyi, Enyi Watu wa Nguvu na Uwezo! Nyinyi ndio Maanswari (Wenye kunusuru) wa Mwenyezi Mungu (swt) na Nusra (Usaidizi wa Kinguvu) ya Dini hii ni faradhi juu yenu. Katika Uislamu hairuhusiwi kwenu kuchelewesha utoaji wa Nusra yenu hata kwa saa moja. Jueni kwamba Nusra ya Dini hii haitanguliwi na mapenzi ya maisha wala hofu ya kukandamizwa. Hivyo basi jitokezeni kutoa Nusra kwa Hizb ut Tahrir na Da'wah yake, mtoe Ahadi ya Utiifu (Bay'ah) kwake ili kusimamisha tena Dola ya Pili ya Uislamu, Dola ya Khilafah kwa Njia ya Utume. Hivyo kuweni Maanswari wa leo, kama ambavyo watu wa al-Madina walikuwa Maanswari wa jana. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

 [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا كُونوا أَنصَارَ اللَّهِ كَمَا قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ لِلْحَوَارِيِّينَ مَنْ أَنصَارِي إِلَى اللَّهِ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ نَحْنُ أَنصَارُ اللَّهِ]

“Enyi mlio amini! Kuweni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu, kama alivyo sema Isa bin Mariamu kuwaambia wanafunzi wake: Nani wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu? Wakasema wanafunzi: Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu!” [As-Saff 61:14].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu