Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  23 Shawwal 1440 Na: 1440 /63
M.  Jumatano, 26 Juni 2019

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali ya Bajwa-Imran Yashindwa Kutii Agizo la Kumleta Naveed Butt katika Kesi ya Watu Waliopotea, lakini Huchangamka Kuchukua Hatua kwa Kila Matakwa ya Mabwana zake Wakoloni

(Imetafsiriwa)

Msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Pakistan, Naveed Butt, anaendelea kutekwa nyara tangu tarehe 11 Mei 2012, wakati majambazi kutoka kwa mashirika ya serikali walipomteka nyara kwa nguvu nje ya nyumba yake jijini Lahore, mbele ya watoto wake na majirani waliojaa hofu. Kwa miaka sita, Tume ya Watu Waliopotea imeendesha vikao katika kesi ya Naveed. Mnamo 27 Disemba 2017, tume hiyo ilitoa agizo la utolewaji ambalo lilithibitisha ukweli kwamba Naveed anazuiliwa na mashirika ya ujasusi. Lilitolewa kwa mamlaka husika za serikali lakini Naveed Butt bado hajapelekwa katika mahakama yoyote ya sheria. Familia yake kisha ililazimika kusajili shtaka jengine katika Mahakama Kuu ya Lahore kuitaka serikali ya Bajwa-Imran itii agizo la utoaji la Tume ya Watu Waliopotea. Kesi ya Naveed Butt inathibitisha kwamba mfumo wa sasa ni kipofu linapokuja suala la haki kwa Waislamu, na uko hai tu kuwatumikia wakoloni.

Enyi Waislamu wa Pakistan!

Watawala wa Pakistan walimrudisha haraka haraka rubani mshambulizi wa Kihindi Abhinandan kwa "familia yake" kwa "huruma," lakini wananyima Naveed bila ya huruma hata simu moja ili kuwahakikishia familia yake usalama wake, katika zaidi ya miaka saba. Watawala wa Pakistan wanadai kwamba wanataka "kuziimarisha taasisi" lakini kwa kiburi wanapuuza agizo la kumtoa Naveed Butt, kwa sababu tu ya kushikamana kwao na vita vya wakoloni dhidi ya Uislamu na kutawala kwa Uislamu. Watawala wanamzuia Naveed Butt katika utekaji huu ili kuwafurahisha wale ambao hofu yao ya kurudi kwa Khilafah huwafanya wakeshe vitanda mwao, bila ya kuzingatia onyo la Mwenyezi Mungu (swt),

(إِنَّ الَّذِينَ فَتَنُوا الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ثُمَّ لَمْ يَتُوبُوا فَلَهُمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمْ عَذَابُ الْحَرِيقِ)

“Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua.” [Surah Al Buruj 85:10.] Kwa hivyo, watawala hawa waovu hawana huruma katika msimamo wao kwa Muislam mnyoofu anayelingania hukmu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt), ingawa katika Hadith Qudsi, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«إِنَّ اللَّهَ قَالَ مَنْ عَادَى لِي وَلِيًّا فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالْحَرْبِ» “Hakika Mwenyezi Mungu amesema, yeyote anayemdhuru Walii wangu basi nimekwisha tangaza vita naye” [Bukhari]. Hivyo basi, Je! Waislamu walio na nia njema hawatajitenga na dhambi hili baya la watawala hawa, kwa kupaza sauti zao kutaka kutolewa kwa Naveed Butt?

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Pakistan

#FreeNaveedButt

#MwacheniHuruNaveedButt

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu