Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
H. 4 Rabi' I 1443 | Na: 1443/14 |
M. Jumatatu, 11 Oktoba 2021 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Baada ya Taarifa ya Naibu Waziri wa Kigeni wa Amerika, Asiyekuwa na Ruwaza Ndiye Pekee Atakayedumisha Muungano pamoja na Washington
(Imetafsiriwa)
Kwenye mahojiano na Jamshyd N. Godrej yaliyopeperushwa mnamo 7 Oktoba 2021, Naibu Waziri wa Kigeni wa Amerika, Wendy R Sherman, alitamka kwa kiburi, "Hatuioni tukijenga uhusiano mpana na Pakistan ... Lakini kile tunahitaji pekee ni kujua kinachoendelea nchini Afghanistan ... Sisi sote tunahitaji kuhakikisha kuwa tuna uwezo tunao hitaji kuhakikisha usalama wa kila mtu, ukiwemo wa India.” Licha ya taarifa hii ya kudhalilisha, uongozi wa jeshi na kisiasa ulimpokea kwa taadhima, ukapokea maagizo mapya kwa makini na kuanza kuyatekeleza kwa haraka. Mnamo tarehe 9 Oktoba 2021, siku moja tu baada ya kumalizika kwa ziara ya Wendy Sherman, Waziri Mkuu wa Pakistan, Imran Khan, aliamuru kuanzishwa kwa seli maalum ya kuboresha masuala ya Afghanistan, kwa mujibu wa miongozo ya Amerika. Kitendo hiki cha utiifu wa kitumwa kiliwasilishwa kama uratibu wa mashirika ya serikali juu ya suala la "misaada ya kibinadamu." Kwa kweli, watawala waliofilisika kifikra wa Pakistan hawajali kujithamini wao wenyewe wala masilahi ya Pakistan!
Sio mara ya kwanza kwa Amerika kuitishia, kuikemea na kuidhalilisha Pakistan, huku ikiidunisha Pakistan kutoka kwa hadhi ya mshirika wake. Kama ilivyofanya kwa zaidi ya miaka ishirini, licha ya ukandamizaji mkali wa watawala wa Pakistan, Hizb ut Tahrir Wilayah Pakistan aliwaonya Watu wanaomiliki Nguvu wa Pakistan juu ya ubwege wa muungano na Amerika, katika taarifa kwa vyombo vya habari mnamo 2 Oktoba 2021, ikisema, "Mkutano wa Quad wa 24 Septemba unazindua juu ya ukweli kwamba Amerika imeifanya India kuwa mshirika wa kimkakati dhidi ya China, huku ikiitupa Pakistan kama karatasi chafu iliyotumiwa. Baada ya kutumia nguvu ya kimkakati, kiuchumi na kitamaduni ya Pakistan kutimiza masilahi yake, Amerika sasa itatumia tishio la vikwazo, ili Pakistan itoe mwanya wa kuibuka kwa India, kama kiongozi wa eneo hili. Enyi Watu mnaomiliki Nguvu wa Pakistan! Achaneni na Amerika sasa, kwa haraka kama ilivyoiacha Pakistan." Ni wazi watawala wa Pakistan sio wajinga, hivyo basi je wakati haujawadia wa kumaliza usaliti dhidi ya Pakistan, Umma na Uislamu?
Enyi Watu mnaomiliki Mamlaka na Nguvu! Kwa zaidi ya miongo saba, watawala wa Pakistan wamekuwa wakifuata masilahi ya Amerika, wakitaraji kuwa Pakistan itakuwa salama na kufanikiwa kupitia ukarimu wa Amerika. Ingawa Amerika iliruhusu uimarishaji mdogo wa Pakistan hapo awali, hii ilikuwa tu wakati India haikuwa katika duara la ushawishi wa Amerika, bali la Uingereza, na ili tu kutiaa shinikizo kwa kipote cha watawala wa India kuachana na London kwa kuipendelea Washington. Lakini, hayo yote yalibadilika baada ya maridhiano kati ya Vajpayee na Clinton mnamo 2000, wakati BJP ilipoweka mafungamano makubwa na Amerika na kwa hivyo Amerika iliitupa Pakistan mara moja kama karatasi chafu iliyotumiwa.
Kwa hivyo, ni vipi, baada ya miongo miwili, mtu yeyote mwenye macho na busara atarajie kwamba Washington sasa ghafla itaichukua tena Pakistan kutoka kwenye jaa la taka la historia ya Amerika? Utegemeaji dola kuu ya kigeni umeifanya Pakistan kuwa mtumwa kwa masilahi ya kigeni, kwa gharama kubwa kwa usalama na ustawi wake wenyewe. Kuondoka kutoka utegemezi wa Washington hadi wa Moscow au Beijing hubadilisha tu bwana-mtumwa, au huongeza mabwana wapya wa watumwa. Pakistan itakuwa salama na kufanikiwa tu kupitia kukomesha kutegemea dola za kigeni, na kuifanya Tawwakul kwa Mwenyezi Mungu (swt) na kuchangamkia rasilimali kubwa ambazo yeye (swt) ametupatia, kama vile Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alivytuonyesha, kama kiigizo bora. Kusimamishwa kwa Khilafah kuunganisha Pakistan, Afghanistan na Asia ya Kati, kama dola moja yenye nguvu, kutarudisha Eurasia katika hali yake sahihi, ya karne nyingi, ya kihistoria, kwa utawala wa Uislamu na kushindwa kwa dola za makafiri. Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Sitisheni kuwa kwetu tu poni kwenye bodi ya chesi ya Eurasia. Wang'oeni watawala wa sasa wasio na maono na muwabadilishe kwa kuipa Nussrah Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume, ili Umma wa Kiislamu kwa mara nyengine tena uwaelekeze wabinadamu kwa mwongozo angavu wa Uislamu. Mwenyezi Mungu (swt) asema,
(أَتَخْشَوْنَهُمْ فَاللّهُ أَحَقُّ أَن تَخْشَوْهُ إِن كُنتُم مُّؤُمِنِينَ)
“Je, mnawaogopa? Basi Mwenyezi Mungu anastahiki zaidi mumwogope, ikiwa nyinyi ni Waumini.” [Surah At-Tauba 9:13].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Pakistan |
Address & Website Tel: https://bit.ly/3hNz70q |