Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  3 Sha'aban 1437 Na: PR16028
M.  Jumanne, 10 Mei 2016

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mwacheni Huru Naveed Butt
Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir Wilayah Pakistan Ilituma Ujumbe kwa Tume ya Haki za Binadamu Pakistan

(Imetafsiriwa)

Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir Wilayah Pakistan ilituma wajumbe kwa Tume ya Haki za Kibinadamu Afisi za Pakistan jijini Karachi, Lahore na Islamabad. Wajumbe hao waliwasilisha barua inayowataka wanaharakati wa haki za binadamu kuhamasisha kuachiliwa kwa watetezi wa Khilafah. Pia iliwasilisha maelezo ya kina ya baadhi ya kesi mashuhuri, ikiwa ni pamoja na ile ya Naveed Butt, Msemaji wa Hizb ut Tahrir ambaye amesalia kutekwa nyara tangu tarehe 11 Mei 2012, hadi sasa hajulikani aliko, pamoja na Saad Jagranvi, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano iliyekamatwa mnamo tarehe 22 Aprili 2015. Wengi wa wale waliokamatwa na kutekwa nyara nchini Pakistan wamepata mateso makali, ikiwa ni pamoja na kunyimwa usingizi, kupigwa bila huruma, kulazimishwa kula dawa za kubadilisha akili na kupigwa shoti ya umeme mikononi mwa vyombo vya usalama. Mamlaka mara kwa mara zimenyima haki muhimu za matibabu na kutembelewa kwa walio gerezani. Na familia, marafiki na watu wema wa waliofungwa pamoja na waliotekwa nyara wamekuwa wakitishiwa mara kwa mara na vyombo vya usalama vya Pakistan.

Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir Wilayah ya Pakistan inawataka Waislamu wanyofu nchini Pakistan, haswa kutoka kwa watu wenye ushawishi ndani ya idara ya mahakama ya Pakistan, wanasheria, vyombo vya usalama na vitengo vya haki za binadamu, kuzungumza sasa kwa niaba ya watetezi hao wa dhati wa Khilafah kwa njia ya Utume, ili kukomesha mateso makali wanayofanyiwa.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu