Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  25 Rajab 1437 Na: PR16025
M.  Alhamisi, 28 Aprili 2016

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Simulizi za Seymour Hersh
Naveed Butt Alitekwa Nyara baada ya Kuwafichua Wasaliti katika Uongozi wa Jeshi Juu ya Shambulizi la Amerika la Abbotabad

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 27 Aprili 2016, dondoo za kitabu kimoja cha mwandishi wa habari maarufu wa Marekani, Seymour Hersh, zilichapishwa katika gazeti la Kiingereza la Dawn, ambamo alisema kwamba amekinai sana zaidi kuliko hapo awali kwamba Pakistan iliisaidia Marekani kumpata Osama. Seymour Hersh alitangaza katika kitabu chake kipya cha 'The Killing of Osama Bin Laden', aliandika kwamba, "Marekani na Pakistan kisha zilifikia makubaliano: Marekani ingevamia boma la Bin Laden lakini ikaifanya ionekane kana kwamba Pakistan haikujua."

Ushahidi wa Seymour Hersh hauhitajiki kuthibitisha kwamba shambulizi la Abbotabad mnamo tarehe 2 Mei 2011 lilifanyika kwa usaidizi na uungwaji mkono kamili na wasaliti katika uongozi wa jeshi. Mtu yeyote mwenye akili timamu anayefahamu historia ya jeshi la Marekani anajua vyema kwamba Marekani haina uwezo wa kufanya mashambulizi ndani ya nchi yenye nguvu kama Pakistan, isipokuwa ikiwa imehakikishiwa kuwa hakutakuwa na upinzani au jibu. Kwa hiyo, baada ya shambulizi hili Naveed Butt, Msemaji wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Pakistan, mara moja alifichua khiyana ya wasaliti katika uongozi wa kisiasa na kijeshi kupitia taarifa zake kwa vyombo vya habari. Mnamo tarehe 2 Mei 2011, Naveed Butt alisema, "Operesheni ya Abbotabad inawakilisha shambulizi la kujitoa mhanga lililowekwa na watawala wasaliti dhidi ya uhuru wa Pakistan... Ili kuepusha aibu, huku wakikanusha rasmi kuhusika na shambulizi hilo, watawala walivujisha ripoti zinazothibitisha hilo. shughuli hazingeweza kamwe kufanyika bila mashirika ya kijasusi ya Pakistan” (Nambari ya Taarifa kwa Vyombo vya Habari: pk11021pr). Vile vile Naveed Butt alikosoa vikali kauli ya Jenerali Kayani iliyotolewa ili kutuliza hasira na chuki dhidi ya Marekani iliyoelekezwa dhidi ya uongozi wa kijeshi wakati huo, ambapo aliwataka Waamerika kupunguza idadi ya wanajeshi wao nchini Pakistan. Naveed Butt mnamo tarehe 6 Mei 2011 alisema, "Kamanda wa jeshi kubwa zaidi la kijeshi katika Ulimwengu wa Kiislamu anaomba kutoka Amerika kupunguza uwepo wa wanajeshi wake nchini Pakistan...

Hatupaswi kusahau kwamba Kayani aliyekuwa mkuu wa ISI wakati watoto wasio na hatia walipochinjwa katika Jam’ia Hafsa katika tukio la Lal Masjid. Kayani kwa amri ya Marekani ndiye iliyeanzisha operesheni katika Swat, Shirika la Bajour, Waziristan Kusini na Shirika la Orakzai, na kuua maelfu ya Waislamu..... Kwa hiyo, hakuna shaka kwamba Kiyani na uongozi wa sasa wa kijeshi sio tofauti na Musharraf, kwa kweli wako hatua chache mbele” (Nambari ya Taarifa kwa Vyombo vya Habari: pk11023pr).

Baada ya kufichua usaliti wa wasaliti katika uongozi wa kijeshi, Naveed Butt alitekwa nyara na majambazi wa Jenerali Kayani na Shuja Pasha. Hata baada ya kuondoka kwa Jenerali Kayani, Jenerali Raheel Sharif hajamwasilisha Naveed Butt katika mahakama yoyote, wala kumwachia huru na anabaki kuwa "mtu aliyepotea" karibu miaka minne baadaye. Iwapo Jenerali Raheel angekuwa na ikhlasi kwa Pakistan basi angewakamata Musharaf na Kayani na kumwachilia huru Naveed Butt, ambaye alilinda maslahi ya Uislamu na Pakistan kwa kufichua usaliti wa wasaliti katika uongozi wa kijeshi.

Hizb ut Tahrir Wilayah Pakistan inatoa wito kwa maafisa wanyofu katika vikosi vya jeshi kuwakamata wasaliti katika uongozi wao na kutoa Nussrah kwa ajili ya kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Ni Khilafah pekee ndiyo itakayokomesha utumwa wa Pakistan kwa Amerika na udhalilifu mikononi mwake.

 [إِنَّ اللَّهَ لاَ يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُواْ مَا بِأَنْفُسِهِمْ]

“Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo nafsini mwao.” [Ar-Rad: 11]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu