Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  9 Rajab 1436 Na: PR15041
M.  Jumatano, 27 Mei 2015

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mwacheni Huru Naveed Butt
Huku akiwa Dhaifu mbele ya Shinikizo Kubwa la Kuachiliwa Huru kwa Naveed Butt, Serikali "Mtekaji nyara" Inageukia Urongo Duni.

(Imetafsiriwa)

Miezi minane baada ya kesi kusikilizwa kwa mara ya mwisho, usikilizaji katika kikao cha Tume ya Uchunguzi juu ya Kupotezwa kwa Nguvu ulifanyika jana, 26 Mei 2015, kuhusu kutekwa nyara kwa Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir nchini Pakistan, Naveed Butt, ambaye alitekwa nyara na majambazi wa taasisi mnamo tarehe 11 Mei 2012. Jaji alilaani taasisi hizo kwa hadithi yao ya urongo kwamba Naveed aliuawa katika shambulizi la droni katika maeneo ya makabila ambayo ilibebwa katika kipande cha gazeti linaloegemea taasisi hiyo mnamo Julai 2013. Hizb ut Tahrir inalaani mbinu hii duni ya utawala wa Raheel-Nawaz kuendelea kujificha nyuma ya urongo, ili kuepusha shinikizo kubwa juu yake kuachiliwa huru kwa Naveed Butt.

Inajulikana kuwa Naveed alitekwa nyara mbele ya mashahidi na majambazi wa serikali, nje ya nyumba yake, baada ya kurudi huko na watoto wake kutoka shuleni kwao. Hii ilikuwa ni baada ya miezi kadhaa ya vyombo hivyo kumuwinda huku na kule, kumdadisi na kutoa vitisho kupitia chaneli yoyote inayopatikana kwao. Baada ya kutekwa nyara kwake, kama uthibitisho zaidi, baadhi ya watu wenye ikhlasi kutoka miongoni mwa watu wenye mamlaka walithibitisha kuwepo kwa Naveed kwenye jela za vyombo hivyo. Zaidi ya hayo, inajulikana pia kwamba Mashababu kadhaa wa Hizb ut Tahrir wametekwa nyara kwa miezi kadhaa kwa wakati mmoja, ikidaiwa na maafisa wa vyombo hivyo kwamba hawakuwachukua, lakini baadaye wakaachiliwa na vyombo hivyo hivyo. Maafisa hawa wa chombo hicho bila aibu walikiuka viapo vyao kwa Mwenyezi Mungu (swt) mbele ya mahakama kwa kusema urongo waziwazi.

Ikikabiliwa na shinikizo kubwa la kuachiliwa huru kwa Naveed kutoka kila pembe na ngazi za Pakistan, na vile vile kutoka kwa Waislamu kote duniani, serikali "mtekaji nyara" umetabanni mbinu duni kukengeusha shinikizo hilo. Ni dhahiri zaidi kwamba serikali hii imechagua njia ya watekaji nyara warongo kwa sababu haina Neno hata moja la Ukweli la kujihami kutokana na ulinganizi mkali wa Hizb ut Tahrir wa kumuondoa Raj wa Kiamerika na kusimamisha Khilafah pahali pake.

Serikali hii "mtekaji nyara" hivi karibuni itajua kosa lake katika kuchagua njia ya ukandamizaji Uislamu kwa nguvu. Inasogeza tu karibu kuanguka kwake kwenyewe. Mahakama za Khilafah inayokuja hivi karibuni, inshaaAllah, zitawatoa wale wote waliohusika na utekaji nyara, ambao uko chini ya jinai kubwa ya kueneza ufisadi ardhini. Mahakama hizi zitawahukumu wale waliotoa amri kutoka kwa makhaini katika uongozi wa kisiasa na kijeshi, pamoja na wale majambazi waliotekeleza amri zao za uovu na kuwaadhibu kwa kumpiga kwao vita Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[إنَّمَا جَزَاءُ الَّذِينَ يُحَارِبُونَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَيَسْعَوْنَ فِي الْأَرْضِ فَسَادًا أَنْ يُقَتَّلُوا أَوْ يُصَلَّبُوا أَوْ تُقَطَّعَ أَيْدِيهِمْ وَأَرْجُلُهُمْ مِنْ خِلَافٍ أَوْ يُنْفَوْا مِنَ الْأَرْضِ ذَلِكَ لَهُمْ خِزْيٌ فِي الدُّنْيَا وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ - إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا مِنْ قَبْلِ أَنْ تَقْدِرُوا عَلَيْهِمْ فَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ]

“Basi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi katika nchi, ni kuuwawa, au kusalibiwa, au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kutolewa nchi. Hii ndiyo hizaya yao katika dunia; na katika Akhera watapata adhabu kubwa. Isipo kuwa wale walio tubu kabla hamjawatia nguvuni. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira na Mwenye kurehemu.” [Surah Al-Maida 33-34]

Fauka ya yote, wale wanaowatesa Waumini wenye ikhlasi, wanakaribisha maangamivu yao wenyewe mikononi mwa Mwenyezi Mungu (swt), Mwenyezi Mungu (swt) amesema katika Hadith Qudsi:

«مَنْ عَادَى لِي وَلِيًّا فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالْحَرْبِ»

“Yeyote anayemfanyia uadui Walii wangu nimekwisha tangaza vita dhidi yake.” [Bukhari]. Bila ya shaka, majuto na kukata tamaa katika siku ambayo hakuna hata mmoja aliyewekwa kwa ajili ya kuwaokoa madhalimu wenyewe wanaowatesa walinganizi wa Uislamu badala ya kuzingatia wito wao. Mwenyezi Mungu (swt) asema

 [إِنَّ الَّذِينَ فَتَنُوا الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ثُمَّ لَمْ يَتُوبُوا فَلَهُمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمْ عَذَابُ الْحَرِيقِ]

“Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua.” [Surah Al-Buruj 85:10].

Na majuto na kukata tamaa vyote viwili ni kwa wale wanaotoa amri za ukandamizaji, na vile vile wale majambazi ambao ndio miguu yao, macho na masikio yao katika kutekeleza amri hizo, wakiwatii kwa upofu wale wanaomuasi Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw). Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

 [وَقَالُوا رَبَّنَا إِنَّا أَطَعْنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَاءَنَا فَأَضَلُّونَا السَّبِيلَ]

“Na watasema: Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tuliwat'ii bwana zetu na wakubwa wetu; nao ndio walio tupoteza njia.” [Surah Al-Ahzab 33:67]

Hatimaye, Hizb ut Tahrir inazidi kuwahakikishia Waislamu kwamba kampeni yake ya kiulimwengu ya "Mwacheni Huru Naveed Butt" itaendelea, ikishajiishwa na msimamo dhaifu wa serikali ilioilazimisha kupotoa shinikizo kupitia mbinu duni thamani, hadi ndugu yetu mpendwa arudishwe kwetu akiwa salama na mzima inshaallah.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu