Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  7 Rajab 1443 Na: 1443 / 39
M.  Jumanne, 08 Februari 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kupitishwa kwa Mswada wa Marekebisho wa SBP Kunabainisha kuwa Vyama vyote vya Kidemokrasia Vinalinda Maslahi ya Wakoloni.

(Imetafsiriwa)

Iwe ni kupitishwa kwa Mswada wa Marekebisho wa SBP, bajeti ndogo iliyoagizwa na IMF, sheria inayoendeshwa na FATF au sheria inayotoa haki ya kukata rufaa kwa Kulbhushan Jadhav, sasa ni wazi kwamba uongozi wote wa kidemokrasia, iwe katika kutawala au katika upinzani, wako kwenye ukurasa mmoja kuhusiana na kutimiza matakwa ya ukoloni wa kimataifa. Licha ya tofauti kuhusu ubwana wa kiraia na kijeshi, PTI, PPP na PML-N zote zinatii matakwa ya mfumo wa kiulimwengu wa kikoloni, kuhakikisha kwamba Pakistan inasalia kunyonywa na mataifa ya kigeni. Hivyo basi, Enyi Watu Wenye Nguvu na Uwezo, mtaruhusu utumwa huu muovu kudumu mpaka lini? Je, wakati haujawadia sasa wa kuigeukia Hizb ut Tahrir, pamoja na mradi wake wa Khilafah kwa Njia ya Utume, ili kuepuka mtego huu wa sasa?

Je, kuna chama chengine chochote cha kisiasa mbali na Hizb ut Tahrir, ambacho kinaweza kukomesha utumwa wa mfumo wa kikoloni wa Kimagharibi? Hizb ut Tahrir pekee hivi sasa ndiyo inayolingania ukombozi wa Waislamu kutoka katika minyororo ya mgawanyiko kwa msingi wa dola ya kitaifa. Niyo pekee inayolingania kuunganishwa kwa Pakistan, Afghanistan, Asia ya Kati, Mashariki ya Kati na Ulimwengu wote wa Kiislamu, kama Dola moja ya Khilafah. Je, kuna chama chochote cha kisiasa zaidi ya Hizb ut Tahrir, ambacho kinatoa mpango kamili wa kivitendo wa kutukomboa kutoka katika minyororo ya mfumo wa uchumi wa kiulimwengu unaotawaliwa na dola, na kutukomboa kutoka kwenye makucha ya IMF kwa kutoa sarafu inayoegemezwa kwa dhahabu na fedha? Ni nani kando na Hizb ut Tahrir, anayetaka kuhamasishwa kwa majeshi ya Ummah kwa ajili ya ukombozi wa Kashmir Iliyokaliwa kwa mabavu na Al-Masjid al-Aqsa, chini ya Khalifah Muongofu, na kupindua njama za makafiri? Khilafah pekee ndiyo itakayomwadhibu Kulbhushan Jadhav na washirika wake, ambao wanaeneza moto wa uchochezi huko Baluchistan na maeneo mengine, wakati vyama vya kidemokrasia vyote vimejisalimisha kwa mahakama za kimataifa za wakoloni. Ni Khilafah pekee ndiyo itakayotuondoa kutoka idara ya mahakama za kikafiri ya zama za wakoloni ambayo imeyafanya maisha ya watu kuwa duni, huku vyama vyote vya kidemokrasia vikijitolea kikamilifu kwa sheria ya Raj Uingereza, pamoja na marekebisho madogo. Enyi Watu wenye Nguvu na Uwezo, ni nani anayesema tumeishiwa na machaguo? Vipi, wakati Khilafah na Hizb ut Tahrir ni njia iliyo wazi ya ukombozi kutoka kwa ukoloni? Je hatutazingatia angalau?!

Khalifah Muongofu, ‘Umar al-Farooq (ra) alisema, نحن قوم أعزَّنا الله بالإسلام فمهما ابتغينا العزَّة في غيره أذلَّنا الله “Sisi ni watu ambao Mwenyezi Mungu amewatukuza kupitia Uislamu. Pindi tutakapotafuta utukufu kwengine kusikokuwa katika Uislamu, Mwenyezi Mungu atatudhalilisha.” Tangu kuondolewa kwa Khilafah tarehe 28 Rajab 1342 H, 3 Machi 1924 M, tabaka la kisiasa lenye ushawishi wa Magharibi linatafuta heshima kutoka kwa mfumo wa kimataifa wa wakoloni, sheria za mahakama, hali za kiuchumi na mifumo ya utawala. Ni kujisalimisha huku kwa sheria na kanuni za wakoloni ambako kumehakikisha tunazidi kuwa watumwa, muongo baada ya muongo. Baada ya zaidi ya karne moja hijria ya giza, taabu na fedheha, ni wakati muafaka wa kuung'oa mfumo wa ukafiri. Enyi majeshi ya Pakistan, sheria na sera za mfumo wa sasa ndizo zinazohakikisha kuwa sisi ni mawindo rahisi ya ukoloni wa Kikafiri. Jitokeni na mutoe Nussrah yenu kwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume, itakayovunja minyororo ya utumwa kwa mkoloni Magharibi. Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

 [وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.”[Surah Ar-Rum 30: 4-5].

#YenidenHilafet         #ReturnTheKhilafah             #الخلافة_101      #أقيموا_الخلافة

#TurudisheniKhilafah

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu