Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  19 Dhu al-Qi'dah 1439 Na: 1439/50
M.  Jumatano, 01 Agosti 2018

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

#MuachilieniHuruDadaYetuRomana:

Ni Mpango wa Marekani wa kumvamia usiku na kumteka nyara Mwanamke Muumini nyumbani kwake, kwa sababu ya Kutamka kuwa Mola wake ni Allah (swt)

Saa za mapema mnamo 30 Julai 2018 wafanyikazi kutoka idara ya ujasusi ilimteka nyara Dada Romana Hussain, mwalimu wa Kiislamu mwenye kuheshimika na mama wa watoto wanne. Amehitimu shahada ya masuala ya kiakili na falsafa kutoka chuo maarufu cha ST.Joseph na shahada ya uzamili katika masomo ya Uislamu. Baada ya kuipata thaqafa ya Hizb ut Tahrir nyumbani kwao Karachi, majambazi hawa walimteka bila kujali utukufu wa nyumba au kuwanyima watoto usimamizi wao. Kitendo hicho cha kutamausha dhidi ya Dada Romana ni kutoka katika mfano wa madhalimu wa Quraysh, ambao hawakujali hadhi ya wanawake kwa kumtesa na kumuua Sumayah (ra) kama shahidi wa kwanza katika Ummah wa RasulAllah (saw). Vitendo hivyo dhidi ya Dada Romana ni kwa mujibu wa maagizo ya Marekani, bwana wa kweli wa serikali wanaokuja na kuondoka Pakistan kupitia uchaguzi, mapinduzi na mapinduzi hafifu. Na vitendo hivi vinadhibitisha kwamba hatutakuwepo na “Pakistan Mpya” na hakutakuwa na “Serikali ya Madina” baada ya uchaguzi. Hakika ni wazi kwamba Pakistan imebakia kuwa Kibaraka wa Marekani, wakati ambapo mwanamke aliyejihifadhi na muumini haifadhiwi na Dini yake.

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan inawashitaki watawala walioko mamlakani na wale wanaochukua hatamu za uongozi kwa neno la Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw) ili waweze kutafakari. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

إِنَّ الَّذِينَ فَتَنُوا الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ثُمَّ لَمْ يَتُوبُوا فَلَهُمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمْ عَذَابُ الْحَرِيقِ﴿

Hakika waliofitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakhutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua.” [Al-Buruj: 10].

 RasulAllah (saaw) said, «ومن عادى أولياء الله فقد بارز الله بالمحاربة»“Na anaye onyesha uadui dhidi ya Awliya (walio karibu na Allah) wa Mwenyezi Mungu watashindana na Mwenyezi Mungu katika mzozano.” (imesimuliwa na Hakim kama Sahih kutoka kwa Mu'aadh bin Jabal. Na katika Hadith Quds imesimuliwa,

قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّ اللَّهَ قَالَ مَنْ عَادَى لِي وَلِيًّا فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالْحَرْبِ»

“Mtume (saw) alisema kwamba, “yeyote anayemddhuru Wali wangu nitamtangazia vita dhidi yake…” [Bukhari]. Hivyo basi, Hizb ut Tahrir inawataka watawala wapya kumuogopa Mwenyezi Mungu (swt), kurekebisha kosa hilo kubwa na kumuachilia mara moja akiwa salama Dada Romana Hussain kwa wanawe, wakimruhusu kuendelea na ulinganizi wake wa Amani wa kusimamisha Uislamu kama mwenendo wa maisha, kupitia kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume. Na lau watawala hao wapya watalazimisha kuendelea na utumwa wao kwa mabwana zao Amerika, wafahamu kwamba wamejidunisha wenyewe kwa kutojifunza kutokana nay ale yaliyowafika madhalimu kabla yao. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

أفَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنْظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ كَانُوا أَكْثَرَ مِنْهُمْ وَأَشَدَّ قُوَّةً وَآثَارًا فِي الْأَرْضِ فَمَا أَغْنَىٰ عَنْهُمْ مَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿

“Kwani hawatembei katika ardhi wakaona ulikuwaje mwisho wa walio kuwa kabla yao? Wao walikuwa wengi kuliko hawa, na wamewashinda kwa nguvu na athari katika nchi. Wala hayakuwafaa hayo waliyo kuwa wakiyachuma. [Ghafir: 82].

Afisi ya Hizb ut Tahrir Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu