Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  2 Dhu al-Hijjah 1439 Na: 1439/52
M.  Jumatatu, 13 Agosti 2018

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
#MwacheniHuruDktRoshan:
Kumteka Nyara Mwanamke kwa Ajili tu ya Kulingania Hukmu kwa yale yote Yaliyoteremshwa na Allah (swt) ni Kushuka Daraja ya Maquraysh

Katika ugandamizaji wao wa nguvu kwa ulinganizi wa kisiasa wa Uislamu kama mfumo kamili wa maisha, watawala wa Pakistan wametupilia mbali hadhi kuu ambayo Uislamu umeipatia heshima ya mwanamke wa Kiislamu. Katika usiku wa mapema wa Jumatatu 13 Agosti 2018, wafanyikazi wa asasi za usalama walivamia nyumba ya Dkt Romana Roshan na kumteka nyara yeye pamoja na mumewe. Dkt Roshan mlinganizi anayeheshimika mno na mashuhuri sana wa Khilafah kwa njia ya Utume jijini Karachi.

Kwa miaka mingi, alifanya kazi pasi na kuchoka kuendeleza ulinganizi wa utawala wa Kiislamu, akitoa darasa za kawaida kote jijini Karachi, ili wanawake wetu waheshimika wa Kiislamu washiriki kikamilifu katika kupata malipo ya kufanya kazi ya kuregesha maisha kamili ya Kiislamu. Na utekaji nyara huu unajiri wiki mbili tu baada ya Dada Romana kutekwa nyara kwa nguvu, baada ya fasihi za Hizb ut Tahrir kupatikana nyumbani kwake.

Enyi Waislamu wa Pakistan! Vipi utekaji nyara kwa nguvu unatumika dhidi ya mwanamke wa Kiislamu anayelingania Uislamu kama mfumo kamili wa maisha, ndani ya dola iliyoasisiwa kwa jina la Uislamu?

Ni vipi, wakati Ummah wa Muhammad (saw) umepigania heshima ya mwanamke wa Kiislamu katika zama zote za Uislamu? Ni vipi, wakati RasulAllah (saw) alilimaliza kabila zima katika Dola ya Madina, Bani Qaynuqa’a, pindi mmoja wao alipofanya ufidhuli wa kumvunjia heshima mwanamke mmoja wa Kiislamu? Hakika, kulindwa mwanamke wa Kiislamu ndio kunakotufafanua sisi kama Ummah na kututofautisha na mataifa ya kikafiri na uasi. Hivyo basi, tunakumbuka kwa fahari jinsi Khalifah Mua’tasim alivyoivunja ngome madhubuti ya Umairiyah kujibu kilio cha mwanamke mmoja wa Kiislamu, aliye dhulumiwa. 

Na tunakumbuka kwa taadhima kubwa jinsi ardhi zetu zilivyofunguliwa kwa Uislamu, baada ya jeshi la Muhammad bin Qassim kunyunyizia maji mchanga wetu kwa damu zake, kujibu mateso ya Waislamu wanaume na wanawake mikononi mwa dhalimu Raja Dahir. Kwa hivyo, nyanyueni upinzani wenu katika kila kikao mulichoko, ili mwanamke wa Kiislamu amuabudu Allah (swt) kwa kujisalimisha kikamilifu, bila ya hofu ya kuadhibiwa.

Enyi Waislamu katika Jeshi la Pakistan na Asasi za Usalama! Je, hali hii haishangazi? Kwa miaka, wanaume na wanawake wa Hizb ut Tahrir wameshutumu mashambulizi ya kinyama kwa majeshi yetu, wanawake na watoto wetu, huku wakifichua kichwa cha nyoka, mtandao mkubwa wa kigaidi wa Kiamerika wa Raymond Davis. Hizb ut Tahrir imekuwa ikiwalingania kutumia mamlaka na nguvu zenu kuhakikisha usalama wetu, kupitia kukata laini za usambazaji za Amerika za NATO, kufunga balozi zake na kuwafurusha wanajeshi na ujasusi wake wa kisiri. Licha ya hayo, majasusi wa Amerika na wauwaji wake wangali huru kuzurura kwa mapana na marefu biladi yetu, huku mwanamke mukhlisa wa Kiislamu, atekelezaye jukumu lake la kusimamisha tena Uislamu kama mfumo kamili wa maisha, akikamatwa kwa nguvu. Hivyo basi, fanyeni bidii katika kumtii Allah (swt), kwa kuitikia kilio cha mwanamke aliyedhulumiwa na kumkamata aliyemdhulumu. 

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu