Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  22 Rajab 1436 Na: PR15034
M.  Jumatatu, 11 Mei 2015

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Miaka Mitatu Imepita Tangu Kutekwa nyara kwa Naveed Butt Ukandamizaji wa Utawala wa Raheel-Nawaz wa Wanaharakati wa Kiislamu Hautasitisha Kusimamishwa kwa Khilafah

 (Imetafsiriwa)

Huu ni ‘ushujaa’ wa watawala na majambazi wao. Hata baada ya miaka mitatu kupita, hawako tayari kumwachilia huru wala hawana ujasiri wa kumfikisha mbele ya mahakama. Ushujaa wao umefungika kwa Waislamu wasio na hatia lakini pindi makafiri wanapoutukana Uislamu, Muhammad (saw) na Waislamu, wanakuwa watumwa watiifu, wakipokea medali na magwaride ya heshima – utambuzi wa khiyana zao dhidi ya Uislamu na Waislamu. India na Amerika zinapoua wanajeshi wetu na raia, mngurumo wao kama wa simba unakuwa mlio wa paka. Wanatosheka na kutoa kauli tupu za kupinga halafu hawafanyi chochote.

Utawala wa Raheel-Nawaz unajua na umeona kwa macho yake kwamba kumweka Naveed Butt kwenye shimo lao kwa muda wa miaka mitatu na kutekwa nyara na kukamatwa kwa makumi ya Mashababu wa Hizb katika kipindi hiki hakujaitisha au kuinyamazisha Hizb na Mashababu wake. Mbinu hizo za uoga hazijapunguza ulinganizi wa Khilafah kufika kila pembe ya jamii. Lau wangekuwa na Imani yoyote wangejua kwamba huu ni ulinganizi wa Mwenyezi Mungu (swt) na hata kama ulimwengu wote ungekusanyika kusimamisha ulinganizi huu, wangeshindwa. Lau wangekuwa na akili yoyote wangechukua funzo kutokana na mfano wa Uzbekistan ambapo Karimov aliwafunga zaidi ya Mashababu elfu nane wa Hizb kwa muda wa miaka saba hadi kumi na tano na kuwaua makumi yao gerezani lakini pamoja na hayo alishindwa kuiondoa Hizb au ulinganizi wake kutoka Uzbekistan. Badala yake, ilienea hata zaidi.

Tunatoa wito kwa utawala wa Raheel-Nawaz, ikiwa tu kwa madai yao ya kuwa ni Waislamu, kwamba ikiwa wana imani hata chembe kwamba watawasilishwa mbele ya Mwenyezi Mungu (swt) basi watubu kutokana na matendo yao na kumwachilia mara moja Naveed Butt na kukoma kuweka vikwazo dhidi ya ulinganizi huu. Mnapaswa kutubu kabla milango ya toba haijafungwa. Bila kujali, Hizb na Mashababu wake wameridhika na qadhaa ya Mwenyezi Mungu (swt) na wana matumaini kamili kwamba Muumba wa ulimwengu atawapa Jannat-ul-Firdaws kwa ajili ya taabu zao hapa duniani. Jueni kwamba ikiwa mumetoa ahadi ya kuwatumikia mabwana zenu wa Kiamerika hata liwalo na liwe, basi sisi pia tunamuomba Bwana wetu Mwenyezi Mungu (swt), atujaalie azma na uthabiti wa kujitolea muhanga wa mkubwa kabisa na kukikumbatia kifo bila kusita endapo itahitajika katika kutafuta radhi zake peke yake. Hakika huu ni mpango bora zaidi kwa Muumini. Kwa hivyo chaguo ni lako, ewe utawala wa Raheel-Nawaz: utiifu kwa Marekani au utiifu kwa Mwenyezi Mungu (swt).

[وَلاَ تَحْسَبَنَّ ٱللَّهَ غَافِلاً عَمَّا يَعْمَلُ ٱلظَّالِمُونَ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمْ لِيَوْمٍ تَشْخَصُ فِيهِ ٱلأَبْصَارُط مُهْطِعِينَ مُقْنِعِى رُءُوسِهِمْ لاَ يَرْتَدُّ إِلَيْهِمْ طَرْفُهُمْ وَأَفْئِدَتُهُمْ هَوَآءٌ]

“Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayo yafanya madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatapo kodoka macho yao. Nao wako mbioni, vichwa juu, na macho hayapepesi, na nyoyo zao tupu.” [Ibrahim:42-43]

Zingatio: Kwa mnasaba huu Hizb ut Tahrir imetoa taarifa za video za familia ya Naveed Butt, zinaweza kutazamwa katika link hii: pk.tl/1iMQ

Shahzad Shaikh
Naibu Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu