Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
H. 4 Dhu al-Hijjah 1443 | Na: 1443 / 74 |
M. Jumapili, 03 Julai 2022 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mithili ya Demokrasia ya Kisekula, Mahakama za Kisekula ni Walinzi wa Riba, Zihakikisha Kesi ya Kutaka Kukomeshwa kwa Riba Inazungushwa Miduara. Kukomeshwa kwa Riba Kunawezekana tu chini ya Khilafah Pekee, kuanzia Siku ya Kusimamishwa Kwake
#KhilafahEndsRiba
(Imetafsiriwa)
Waislamu wameghadhabishwa kwamba uamuzi wa hivi karibuni wa Mahakama ya Sheria ya Majimbo wa kuondoa riba kutoka kwa uchumi wa Pakistan kwa mara nyingine tena umepingwa katika Mahakama ya Upeo, ambako kesi hiyo ilikuwa inasubiri uhakiki kwa miaka ishirini tayari. Kwa jumla miaka thelathini imepotea, licha ya amri dhahiri na ya kukatikiwa ya Mwenyezi Mungu (swt).
Aidha, huku akitoa maelezo wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo dhidi ya Riba, Jaji mmoja wa Mahakama hiyo ya Upeo, alisema kwamba wale wasiotaka kuchukua riba wasichukue, ilhali Mwenyezi Mungu (swt) atawauliza wale wanaoichukua. Jaji mwengine alisema kuwa hatuwezi kuwasihi watu kukataa riba, kupitia kufungua madrasa ya Kiislamu nje ya Mahakama ya Upeo. Hata hivyo, kamwe hatujawahi kusikia maoni kama haya kutoka kwa idara ya mahakama ya kisekula kuhusu kodi, kwa kusema "wale wanaotaka kulipa kodi walipe, ilhali wale ambao hawataki kulipa, Mwenyezi Mungu (swt) atawauliza, lakini hatuwezi kufungua madrasa ya Kiislamu nje ya Mahakama ya Upeo kuwahimiza watu kulipa kodi.” Mojawapo ya sababu zinazowafanya watu wa Pakistan kughadhabishwa, kutokana na rufaa dhidi ya uamuzi huo, ni kwamba wanafahamu hatua mbaya ambayo Mahakama ya Upeo itachukua kuhusiana na uamuzi huo. Haya ni maoni ya watu kuhusu idara ya mahakama ya kisekula ya Pakistan!
Kwa hakika, kuonesha kukerwa na uamuzi huo na kuzisusia baadhi ya benki zilizokata rufaa dhidi ya kuharamishwa kwa Riba ni dhihirisho la mapenzi ya Waislamu kwa Dini yao na hamu yao ya kuona inatabikishwa. Ndani ya ari hii, mambo yafuatayo yanawasilishwa ili kuorodhesha njia madhubuti ya harakati yetu:
1. Riba imeharamishwa kwa kukatikiwa katika Uislamu na maovu yake yako wazi kwa watu. Watawala wa Pakistan hujifanya kama wawezeshaji walioajiriwa wa IMF, wakinyonya damu ya watu wa Pakistan kwa malipo ya riba. Hata hivyo, deni la taifa linaongezeka kila uchao. Pakistan inalazimika kulipa Rupia 3,950 bilioni kama riba ifikapo Juni 2023, wakati bajeti yake ina lenga mapato ya Rupia bilioni 7,000. Hivyo, zaidi ya asilimia 56 ya mapato ya kodi yatatumika katika malipo ya riba. Deni la taifa lilikuwa Rupia 189 bilioni mwaka 1982, lakini Machi 2022 limefikia Rupia bilioni 44,366.
2. Kama ambavyo demokrasia ya kisekula ya Pakistan ni mlinzi wa mfumo wa kikoloni wa kirasilimali, idara hii ya mahakama ya kisekula ni sehemu ya mfumo huo huo na iko chini ya katiba ile ile ya kisekula. Idara hii ya Mahakama haioni kuwa ni wajibu wake kuondoa chembechembe zisizo za Kiislamu katika mfumo huu. Badala yake, ni idara ya mahakama ya mfumo huu ndio mlinzi wa mfumo huu wa kisekula uliojengwa juu ya riba. Kwa hivyo, ni ndoto ya mwendawazimu kutarajia utabikishaji wa Shariah kutoka katika idara hii ya mahakama. Mtume (saw) amesema,
«لَا يُلْدَغُ الْمُؤْمِنُ مِنْ جُحْرٍ مَرَّتَيْنِ» “Muumini hang’atwi mara mbili kutoka shimo moja.” (Ibn Majah amesimulia kutoka kwa Ibn Umar (ra)).
3. Uislamu ni mfumo uliokamilika, uliounganishwa, huku hukmu zake zikiwa zimeshikamana, zinazokamilishana na sio kugongana. Lazima zitabikishwe kikamilifu na kwa upekee kupitia Dola ya Khilafah kwa njia ya Utume. Sheria zilizoteremshwa kwa wahyi hazipaswi kuchanganywa na sheria zenye kasoro, zisizo kamilifu zilizotungwa na wanadamu. Kwa hivyo, haishangazi kwamba majaribio ya kuzitekeleza hukmu hizi, kivipande au hatua kwa hatua, ndani ya mfumo wa kisekula, yote yameshindwa, kote katika Ulimwengu wa Kiislamu, kwa miongo kadhaa. Katika Uislamu, utaratibu wa kuwekeza pesa katika biashara ni kuanzisha ushirika wa moja kwa moja, sio njia ya mfumo wa benki za "Kiislamu", huku viwanda vizito vikifadhiliwa pakubwa na hazina ya dola. Sarafu inaegemezwa kwa dhahabu na fedha, ambazo thamani yake haipungui kwa zama. Sarafu ya Kiislamu hulazimisha nidhamu ya fedha, ambayo inazuia nakisi ambayo hutatuliwa kupitia kuchapisha pesa au kwa kutoa mikopo yenye riba. Katika hali ya dharura, mikopo isiyo na riba inaweza kuchukuliwa kutoka kwa Ummah, huku ushuru wa dharura wa mara moja unaweza kutozwa kutoka kwa matajiri kwa ajili ya majukumu ya Shariah. Kwa vyovyote vile, Pakistan bado kwa kiasi kikubwa haina nakisi ya kifedha, lau kama si kwa malipo makubwa ya riba. Zaidi ya hayo, kutokana na sarafu iliyoegemezwa kwa dhahabu na fedha, biashara ya kimataifa hazifanyi kwa dolari, hivyo mikopo ya kigeni yenye riba haichukuliwi kufidia nakisi ya sasa ya akaunti kwa kukosekana dolari. Waislamu wataendelea kutoa mikopo bila riba kwa Waislamu wengine, wakitafuta malipo ya Mwenyezi Mungu (swt). Inapobidi, dola itatoa mikopo isiyo na riba kusaidia biashara. Kwa hivyo hakuna haja riba kupitia mfumo jumuishi kama huo. Hakuna wigo wa riba ndani ya uchumi wa Kiislamu.
4. Ni Khilafah pekee ndiyo itakayokomesha riba na kukataa malipo yote ya riba kuanzia pale Khilafah itaposimamishwa. Kuhusiana na malipo ya kiwango asili, bila ya kulipa riba, Khilafah itawawajibisha wale watawala na maafisa, waliochukua deni hilo. Hii ni kwa sababu walitajirika sana katika kipindi hicho. Kwa hivyo, kawango asili cha deni hilo kinapaswa kulipwa kutoka kwa pesa zao zinazozidi mahitaji yao ya kawaida, na kwa uwiano wa fedha zao za ziada.
5. Benki zinazokata rufaa dhidi ya riba zimekuwa zikiamiliana na riba hata kabla ya rufaa hii. Na zingali zinafanya hivyo. Ama benki ambazo hazikukata rufaa, wao vilevile wamenaswa ndani ya dhambi hili kubwa. Ama kuhusu benki ya nne inayokata rufaa, msimamizi wa benki hizi zote, ni Benki Kuu ya Pakistan (SBP). SBP ndiyo inayoweka viwango vya riba nchini na kutoa leseni kwa benki hizi. SBP inaendesha shughuli zake chini ya Kifungu cha Sheria ya Benki Kuu ya Pakistan, 1956, na Sheria ya Makampuni ya Benki, 1962, ambayo yameidhinishwa na dola hiyo ya Kidemokrasia. Kwa hiyo, kuupogoa mti huu wenye sumu, au kutupa matunda yake hatari, huku ukiubakisha mti wenyewe kama ulivyo, kamwe haitatatua tatizo hili. Maadamu mti huu upo, utaendelea kuzaa matunda hayo ya uharibifu.
6. Khilafah ndiyo itakayoing'oa demokrasia na idara hii ya mahakama ya sekula, na kuasisi mfumo wa Uislamu mahali pake. Uislamu hautasimamishwa kupitia kukata rufaa katika mahakama za kisekula, wala kwa ushawishi na hotuba Bungeni, baada ya kula kiapo juu ya katiba hii ya kisekula na kukubali sheria na kanuni zake. Badala yake, Khilafah itasimamishwa kupitia njia ile ile ya Utume ambayo kwayo kipenzi chetu Mtume Muhammad (saw) alisimamisha dola ya Kiislamu mjini Madina, baada ya kuasisi rai jumla mjini Madina, wakati machifu wakuu na makamanda wa kijeshi wa Madinah kama Saad bin Mu'adh. (ra), Usayd bin Hudhair (ra) na Saad bin Ubadah (ra) walipotoa Kiapo cha Pili cha Utiifu cha Aqabah, kutoa Nusrah yao kwa Mtume (saw). Hivyo njia ikafunguliwa kwa ajili ya kuusimamisha na kuutabikisha kikamilifu Uislamu. Hii ndiyo njia ambayo Waislamu ni lazima kuifuata leo. Ni lazima wawakinaishe kaka zao, watoto na jamaa zao, wanaohudumu katika jeshi la Pakistan, kutoa Nusrah kwa Hizb ut Tahrir. Hizb ut Tahrir ndiyo iliyofanya maandalizi kamili ili kuhakikisha utabikishaji wa Uislamu kama mfumo kamili. Imejitolea kwa utayari kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt). Imeikamata kamilifu mandhari ya kimataifa. Ndio chama kikubwa zaidi cha kisiasa ndani ya Ulimwengu wa Kiislamu. Ni chama kinachoongozwa na Maulamaa wa kimataifa, walio na ufahamu wa kisiasa ambao, kwa neema ya Mwenyezi Mungu (swt), wana uwezo wa kuunganisha Ulimwengu wa Kiislamu kama dola moja yenye nguvu. Sasa wakati umewadia wa kusimamisha Khilafah. Basi msiukose ujira huu mkubwa wa kuisimamisha.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Pakistan |
Address & Website Tel: https://bit.ly/3hNz70q |