Alhamisi, 24 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  15 Rabi' I 1444 Na: 1444 / 11
M.  Jumanne, 11 Oktoba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Waislamu wa Pakistan Wapinga Vikali Usalimishaji wa Kashmir kwa Dola ya Kibaniani. Uongozi wowote Mpya wa Kijeshi Lazima Utangaze Jihad kwa ajili ya Ukombozi wa Kashmir, Kuthibitisha Utiifu wake kwa Uislamu na Waislamu

(Imetafsiriwa)

Mkuu wa Wanajeshi ya Pakistan (COAS) Jenerali Qamar Javed Bajwa mnamo tarehe 8 Oktoba 2022, Jumamosi, alihutubia gwaride la kufuzu kwa Kozi ndefu ya 146 katika Chuo cha Kijeshi cha Pakistan. Hotuba hiyo hakika haikumstahiki mkuu wa jeshi ambalo ni la sita kwa ukubwa zaidi duniani, linalochukuliwa kuwa la tisa kwa nguvu zaidi, linalomiliki makombora ya nyuklia na balestiki.

Katika wakati ambapo mshiko wa Dola ya Kibaniani kwa Kashmir Iliyokaliwa unazidi kuwa na nguvu, ukatili wa Dola hiyo ya Kibaniani unaongezeka katika eneo hilo. Waislamu wanauawa kwa umati huko Kashmir na India na nyumba zao zinabomolewa na misikiti inauawa shahidi. Haya yote yanafanywa na dola ya Kibaniani kwa nguvu zake za kijeshi na serikali. Hata hivyo, Jenerali Bajwa anawasihi Waislamu na uongozi mpya wa kijeshi kuanzisha amani katika eneo hilo kwa vyovyote vile, kwa gharama yoyote ile. Kwa maana nyengine, Jenerali Bajwa anawahimiza Waislamu wa Pakistan kukubali ubwana wa dola ya Kibaniani katika eneo letu.

Jenerali Bajwa ametawala Pakistan kwa zaidi ya miaka sita, kwa hivyo alileta nini? Alileta ukosefu wa utulivu wa kisiasa na kiuchumi nchini, kama natija ya kupanua na kujaribu kuongeza muda wa madaraka yake. Ataingia kwenye orodha ya watawala waliotoa pigo kwa Uislamu na maslahi ya Waislamu. Kwa sababu hii, utawala wake utazingatiwa kuwa mbaya zaidi katika historia ya Pakistan. Jenerali Bajwa ana hadhi hii ya aibu katika historia ya Pakistan kwa sababu wakati wa uongozi wake dola ya Kibaniani iliiunganisha Kashmir, huku akikataa katakata kuinua silaha kujibu. Katika historia ya Pakistan, Jenerali Bajwa atakumbukwa kama Jenerali aliyeiuza Kashmir.

Enyi Majeshi ya Pakistan! Amani na dola ya Kibaniani si kwa maslahi ya Pakistan na Waislamu. Madhumuni ya amani hii ni kuipa India masharti, kwa amri za Marekani, ili iweze kutekeleza sera ya Marekani kuhusu China na Uislamu, bila ya kuwa na wasiwasi kuhusu Pakistan. Kashmir ilikuwa ndio mstari wetu mwekundu, lakini India ilipovuka mstari huu, uongozi wetu wa kisiasa na kijeshi ulikaa kimya. Badala yake, uliisaidia India kuiunganisha Kashmir, kupitia kujadidisha makubaliano ya amani na India juu ya Laini ya Udhibiti (LoC).

Enyi Majeshi ya Pakistan! Uongozi wa Pakistan uliisaliti Kashmir kwa sababu tu ya kimya chenu na kutochukua hatua. Kwa nini hamkuikamata mikono ya Jenerali Bajwa? Munakubali vipi sera ya kukataa sera ya Jihad juu ya Kashmir? Muliangukaje kwenye udanganyifu kwamba tunaweza tu ima kuiokoa Kashmir au kuuokoa uchumi? Kwa nini tusiokoe yote mawili kupitia Uislamu? Leo, kwa sababu ya kuachana na Jihad, tumepoteza Kashmir na uchumi wetu, ambao umo ndani ya magofu.

Enyi Majeshi ya Pakistan! Nyinyi ni warithi wa Muhammad bin Qasim, ambaye aliweka msingi wa utawala wa Uislamu katika Bara Dogo la Hindi. Mumeapa kuwalinda Waislamu. Watawala hawa hawana ikhlasi kwa Pakistan na Kashmir. Mstari wao mwekundu ni upanuzi wa madaraka yao na nyadhifa zao. Inatosha sasa! Songeni na muwakamate watawala hawa nyuma ya shingo zao. Toeni Nusrah kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah. Toeni ahadi ya utiifu kwa Khalifa, atakaye kuongozeni katika Jihad kwa ajili ya ukombozi wa Kashmir, ambaye atakuandaeni kwa ajili ya uvamizi wa India na ambaye atasimamisha tena hukmu ya Uislamu, juu ya bara dogo hili zima, kupitia nguvu zenu.

(وَعَدَ اللّٰهُ الَّذِيۡنَ اٰمَنُوۡا مِنۡكُمۡ وَ عَمِلُوا الصّٰلِحٰتِ لَـيَسۡتَخۡلِفَـنَّهُمۡ فِىۡ الۡاَرۡضِ كَمَا اسۡتَخۡلَفَ الَّذِيۡنَ مِنۡ قَبۡلِهِمۡ ص وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمۡ دِيۡنَهُمُ الَّذِىۡ ارۡتَضٰى لَهُمۡ وَلَـيُبَدِّلَــنَّهُمۡ مِّنۡۢ بَعۡدِ خَوۡفِهِمۡ اَمۡنًا‌)

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao.” [Al-Nur 24:55]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu