Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  14 Rabi' II 1445 Na: 1445 / 17
M.  Jumapili, 29 Oktoba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Wilayah of Pakistan Kampeni ya Kulihamasisha Jeshi la Pakistan Army kwenda Al-Masjid Al-Aqsa

(Imetafsiriwa)

[Amali kutoka Wilayah Pakistan Zikitoa Wito kwa Majeshi ya Waislami Kuukomboa Msikiti wa Al-Aqsa - 27/10/2023 M]

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan inaendelea kufanya kampeni ya kuhamasishwa mara moja kwa jeshi la sita kwa ukubwa duniani, lenye uwezo wa nyuklia, Jeshi la Pakistan, ili kuliangamiza umbile la Kiyahudi. Kwa kupuuza vitisho vya utawala huu katili, muoga, Mashababu wanawahutubia Waislamu wa Pakistan katika maeneo ya umma, kote nchini. Wanawataka Maulamaa, hususan, na Waislamu kwa jumla, kuunga mkono kampeni yake, bila ya kuwaogopa watawala wahalifu, waovu. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[فَاللهُ ‌أَحَقُّ أَنْ تَخْشَوْهُ إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ]

“Basi Mwenyezi Mungu anastahiki zaidi mumwogope, ikiwa nyinyi ni Waumini.” [Surah At-Tawbah 9:13]. Hakika Umma umeamka kwa kusudio lake hapa Duniani na kamwe hautarudi kulala kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt). Hebu na usonge mbele sasa kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu (swt), kuwaongoza wanadamu wote kwenye haki, kama ilivyokuwa kwa karne nyingi nyuma.

Hizb ut Tahrir/Wilayah Pakistan inalaani wito wa watawala kwa kile kinachoitwa "jumuiya ya kimataifa," inayoongozwa na dola za Magharibi. Ni dola za kikoloni za Magharibi, ambazo zilianzisha ukaliaji kimabavu wa Mayahudi hapo mwanzo. Wakoloni wa Kimagharibi hivi sasa wanawapatia magaidi hao wa Kizayuni silaha na ufadhili, huku wakiwazika watoto wa Gaza wakiwa hai, chini ya nyumba zao. Wanatoa wito wa kukomeshwa kwa miungano yote na dola za Magharibi, na kukataa mfumo wao wa dhulma wa kilimwengu. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[إِنَّمَا يَنْهَاكُمُ اللهُ عَنِ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَى إِخْرَاجِكُمْ أَنْ تَوَلَّوْهُمْ وَمَنْ يَتَوَلَّهُمْ فَأُولَئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ]

“Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu.” [Surah Al-Mumtahana 60: 9].

Hizb ut Tahrir/Wilayah Pakistan inawalaani watawala wote wa Waislamu ambao wamethibitisha, kwa kuyazuia majeshi ya Waislamu, kwamba wao ni walinzi wa umbile la Kiyahudi. Ilhali, watawala hao hutuma majeshi kote ulimwenguni, wakati wowote mabwana zao wa Magharibi wanapowaamuru kufanya hivyo. Ni khiyana yao ya mwisho kabla Umma haujawakamata na kuutabikisha Uislamu, inshaaAllah. Hakika Mtume (saw) alitoa bishara njema ya kuregea Khilafah kwa Njia ya Utume, baada ya utawala wa kidhalimu. Mtume (saw) amesema,

«ثُمَّ تَكُونُ مُلْكًا جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»

“Kisha utakuweko utawala wa kutenza nguvu, na utakuweko katika muda apendao Mwenyezi Mungu uweko kisha atauondoa apendapo kuuondoa. Kisha itakuweko Khilafah kwa njia ya Utume.” [Ahmad]

Hizb ut Tahrir/Wilayah Pakistan inawaita maafisa wa jeshi kuhamasika kwa ajili ya ukombozi wa al-Masjid Al-Aqsa. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]

“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia” [Al-Surah Al-Anfal 8:72]. Inamkumbusha kila afisa kwamba hawako peke yao. Mwenyezi Mungu (swt) yuko pamoja nao kama Msaidizi wao, na Ummah wote wa Kiislamu utawaunga mkono. Hebu na wachukue heshima ya kuwa wa kwanza kuingia vitani, wakiondoa kizuizi chochote kinachowazuia. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[إِنْ يَنْصُرْكُمُ اللهُ ‌فَلَا ‌غَالِبَ ‌لَكُمْ وَإِنْ يَخْذُلْكُمْ فَمَنْ ذَا الَّذِي يَنْصُرُكُمْ مِنْ بَعْدِهِ وَعَلَى اللهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ]

“Akikunusuruni Mwenyezi Mungu hapana wa kukushindeni, na akikutupeni ni nani, basi, baada yake Yeye ataye kunusuruni? Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu.” [Surah Aal-i-Imran 3:160].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu