Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  18 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: 1445 / 45
M.  Jumatano, 26 Juni 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ubinafsishaji Tayari Umeharibu Sekta ya Kawi, Ilhali Watawala Wangali Wanafuata Maagizo ya Angamivu ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF)

(Imetafsiriwa)

Watawala wa Pakistan wako kwenye harakati za kuvutia wawekezaji kwa ajili ya ubinafsishaji kwa sababu ya maagizo ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa. Mnamo tarehe 23 Mei 2024, Mfuko wa Fedha wa Kimataifa ulisisitiza kwamba mamlaka za Pakistan lazima, "zilinde ufanisi wa sekta ya kawi, ikiwa ni pamoja na mageuzi ya kupunguza gharama ya juu ya kawi ... kuboresha utoaji wa huduma za umma kupitia urekebishaji na ubinafsishaji wa mashirika yanayomilikiwa na serikali (SOE); na kukuza maendeleo ya sekta binafsi, kwa kuweka uwanja sawa wa uwekezaji na utawala imara.” Siku iliyofuata, mnamo tarehe 24 Mei 2024, Waziri wa Shirikisho wa Biashara wa Pakistan alikutana na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Pakistan. Kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari ya Idara ya Habari, Waziri “alitoa mwaliko wazi kwa makampuni ya Korea, na kuwataka kuvinjari na kuwekeza katika miradi ya kibiashara na ya kimkakati ya Pakistan. Sekta muhimu zilizoangaziwa kwa uwezekano wa uwekezaji ni pamoja na kawi.” Mashirika ambayo yanalengwa kubinafsishwa ni pamoja na miradi mikubwa ya kawi yenye faida, kama vile kiwanda cha RLNG na kampuni za usambazaji umeme za Genco 1, 2, 3 na 4.

Katika utumwa wa kipofu kwa wakoloni, serikali inaleta ufukuziaji utajiri usiojali juu ya sekta ya kawi ya Pakistan, ambayo ni uti wa mgongo wa viwanda, ikiwemo viwanda vya kimkakati vya kijeshi. Kanuni za kibepari za kikoloni za "kupunguza mzigo wa taasisi za umma kwenye hazina ya taifa" na "sio kazi ya serikali kufanya biashara" zimekuwa ndio matamshi ya watawala na wahanga wa uchumi wa IMF waliofunzwa na nchi za Magharibi. Watawala hawajali kwamba umma kwa jumla unalipia gharama ya agizo hili la uharibifu la baada ya itifaki ya Washington kwa njia ya umaskini, shida, deni na kujiua. Marekebisho haya mabaya na ubinafsishaji wa sekta ya kawi ambayo yameharibu sekta ya kawi, yalianza katika miaka ya tisiini ya karne iliyopita, kwa matakwa ya taasisi za kikoloni, zikiwemo Mfuko wa Fedha Kimataifa na Benki ya Dunia. Kwa mwaka wa 2024-25, serikali itatumia rupia bilioni 2200 kwa malipo ya umeme, kati ya jumla ya matumizi ya umeme ya bilioni 4000. Itatumia malipo ya umeme, hata kama wazalishaji hawa wa kujitegemea (IPP) hawatazalisha nyuzi hata moja ya umeme.

Marekebisho ya sekta ya kawi yamejaza mifuko ya wawekezaji wa ndani, wawekezaji wa kigeni na wamiliki wa benki. Marekebisho hayo yamehakikisha wizi wa mchana wa akiba na mapato ya watu waliyochuma kwa taabu. Hata hivyo, watawala wanabinafsisha miradi yenye faida ya sekta ya kawi. Wanadai kuwa, "baada ya ubinafsishaji, taasisi zitajisimamia zenyewe." Hata hivyo, hawawezi kujibu swali hili, “Kwa nini taasisi 130 kati ya 160 za kwanza zilizobinafsishwa, zilifungwa?” Wanadai kwamba "Sio kazi ya serikali kufanya biashara." Bado hawawezi kujibu swali, "Ni nani aliyeufanya utoaji wa mahitaji msingi na huduma kwa watu kuwa ni biashara hapo mwanzoni?" Wanadai kwamba "Tutalipa deni la nje kwa mapato ya ubinafsishaji." Bado hawawezi kujibu swali, "Kwa nini deni la Pakistan linaendelea kuongezeka baada ya ubinafsishaji wa makumi na makumi ya taasisi?" Ubepari hulimbikizia mali mikononi mwa wachache tu, na kuwanyima raia sehemu yao katika utajiri wa taifa.

Ujamaa pamoja na ubepari zinashindwa kuelewa ni rasilimali zipi zinapaswa kumilikiwa na umma na zipi zimilikiwe na sekta binafsi na serikali. Hii ni kwa sababu kina cha mada ya umilikaji wa mali kiko nje ya udiriki wa hekima iliyo na kikomo ya mwanadamu. Mwenyezi Mungu (swt) amewapa wanadamu Rehema zake kwa kulitatua suala la umiliki kwa Hekima yake isiyo na kikomo. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«الْمُسْلِمُونَ شُرَكَاءُ فِي ثَلاَثٍ: الْمَاءِ وَالْكَلإِ وَالنَّارِ»

“Watu ni washirika katika vitu vitatu: maji, chakula na moto (chochote kinachotoa moto).” (Ahmed). Katika Uislamu, nishati na madini huwa chini ya ufafanuzi wa umiliki wa umma. Rasilimali hizi ni hitaji la kawaida la umma, matumizi yake yakiwa ya lazima. Ima iwe ni za bei nafuu au za gharama kubwa, watu hawawezi kuishi bila yake. Serikali inasimamia mali ya umma, kama vile mafuta, gesi, maji, ardhi ya malisho, umeme na maji, kwa ajili ya matumizi ya umma. Khalifa wa Waislamu haruhusiwi kuhamisha mali hizi zinazomilikiwa na umma kuwa umiliki wa kibinafsi, kwa njia ya ubinafsishaji.

Katika Khilafah, chanzo kikubwa cha utajiri katika uchumi, nishati, kinagawiwa watu, kwa pamoja. Kutokana na mtazamo wake wa kipekee wa umiliki, Uislamu unahakikisha mzunguko wa mali katika jamii. Uislamu unazuia mali kujilimbikiza mikononi mwa wawekezaji wachache. Zaidi ya hayo, kutokana na hukmu za kiuchumi za Uislamu, umeme, mafuta na gesi hupatikana kwa watu kwa bei nafuu. Ni Khilafah kwa Njia ya Utume ndiyo itakayokomesha unyonyaji wa mali ya umma, kama vile nishati na mafuta, kwa njia ya ubinafsishaji. Itahakikisha utoaji wa mafuta na nishati kwa bei nzuri, na kuzalisha mapinduzi ya viwanda. Waislamu lazima waupe mfumo unaoporomoka wa kikoloni msukumo wa mwisho, ili waweze kujiondolea mzigo wake. Waislamu lazima wawatake maafisa wa kijeshi wa Ummah watoe Nusrah kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume ili Ummah kwa mara nyengine tena uweze kufaidika kikamilifu na utajiri mkubwa ambao Mwenyezi Mungu (swt) ameupa ardhi za Waislamu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu