Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  21 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: 1445 / 46
M.  Jumatano, 29 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Baada ya Shambulizi la Kinyama la Mabomu la Kambi za Wakimbizi mjini Rafah, Ni Dhahiri kwamba Ummah na Majeshi Yake Lazima Wawang'oe Watawala na Kusimamisha Tena Khilafah Rashida

(Imetafsiriwa)

Mnamo usiku wa tarehe 26 Mei 2024, umbile la Kiyahudi lililenga kambi ya wakimbizi mjini Rafah, na makombora yakilipua miili ya wanawake na watoto hadi vipande vipande. Vichwa vya watoto vilitenganishwa na miili yao midogo, huku watu kadhaa wakiteketezwa hadi kufa. Hii ni baada ya Mayahudi wenyewe kuwapeleka watu wa Rafah kwenye mahema ya wakimbizi ili kuepuka mashambulizi ya mabomu. Mauaji haya yalifanyika baada ya amri ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kwa 'Israel' kusitisha mara moja mashambulizi yake ya kijeshi huko Rafah. Siku zimepita tangu shambulizi hilo la kutisha, lakini watawala wa Pakistan wameridhika na msimamo dhaifu uleule waliouchukua mbele ya adui yeyote wa Waislamu. Mnamo tarehe 27 Mei 2024, Waziri wa Mambo ya Nje alisema, "Pakistan inalaani vikali mashambulizi ya 'Israel' na kulenga kambi ya wakimbizi huko Rafah katika Ukanda wa Gaza ambayo imesababisha hasara nyingi." Machoni mwa watawala wa Waislamu, hakuna thamani kwa utakatifu wa Al-Masjid Al-Aqsa, Ardhi Iliyobarikiwa, na damu ya Waislamu. Hawajachukua hatua kwa zaidi ya miezi saba, ingawa Ummah una mamilioni ya askari walio tayari na wenye uwezo.

Enyi Waislamu wa Pakistan na Majeshi yao! Uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan ni wasaidizi wa Marekani na kambi yake ya kijeshi katika moyo wa Ummah, umbile la Kiyahudi. Watawala wa Waislamu ni sehemu ya kambi ya maadui zetu, na sasa hakuna nafasi ya mjadala zaidi, baada ya miezi saba ya kutotenda kwa khiyana. Basi ni nani ataendelea kutii uongozi huu wa kisiasa na kijeshi unaoshirikiana na wale wanaopigana na Mwenyezi Mungu (swt), Mtume wake (saw) na waumini? Ni nani atakayetubia na kujiondolea dhambi, kupitia utiifu kwa Mwenyezi Mungu (swt), Mtume wake (saw) na waumini? Kuwatii watawala hawa kunakaribisha kufufuliwa pamoja nao Siku ya Kiyama, na kushiriki katika adhabu yao kali. Utiifu huo utakuwa chanzo cha majuto makubwa na sababu ya hasara kubwa. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «لَا طَاعَةَ لِمَخْلُوقٍ فِي مَعْصِيَةِ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ» “Hakuna utiifu kwa viumbe, katika kumuasi Mwenyezi Mungu Mtukufu.” (Bukhari).

Enyi Waislamu wa Jeshi la Pakistan! Hebu kila mwana wa Salahudin na ajue kwamba saa ya maamuzi imewajia. Kusitasita na kutochukua hatua kunarefusha tu wakati kwa wasaidizi wa makruseda na Mayahudi. Ni wakati sasa wa kuchukua hatua. Dada zetu, kaka, watoto na wazee wetu wanaodhulumiwa wanauawa kishahidi kwa mabomu, mizinga na makombora ya Mayahudi, lakini wanabaki imara kwenye Dini yetu, wakingojea kusonga kwenu. Al-Masjid Al-Aqsa inakungojeni na Gaza inakuiteni. Sauti za wanaodhulumiwa huko Rafah zimepazwa kwa Mwenyezi Mungu (swt) na zinasubiri majibu yake. Mwenyezi Mungu (swt) amewajibisha kuinusuru Gaza juu yenu, kwa kusema:

 [وَاِنِ اسۡتَـنۡصَرُوۡكُمۡ فِى الدِّيۡنِ فَعَلَيۡكُمُ النَّصۡرُ]

“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia.” [Surah Al-Anfal 8:72]. Zingatieni mfano mzuri wa kaka yenu mheshimiwa, Abdullah Ramadhan, mwanajeshi wa Misri, ambaye alikubali kifo cha kishahidi, alipokuwa akipigana na Mayahudi huko Rafah, mnamo tarehe 27 Mei 2024. Alikuwa amechapisha hapo awali mnamo tarehe 7 Februari 2024, “Moyo unahuzunika. Macho yanatoa machozi. Nina huzuni kwa kuwa karibu na mateso yako, Ewe Gaza. Gaza iko karibu, ilhali dunia ni kiziwi, bubu na kipofu, imeshindwa kuonyesha uanaume. Kutochukua hatua ndio kilele cha kushindwa.” Kwa hivyo, je, hakuna mtu miongoni mwenu mwenye akili, ambaye atasimama kutafuta ushindi na shahada?!

Enyi Waislamu wa Jeshi la Pakistan! Watawala wa Waislamu wameyazuia majeshi ya Waislamu dhidi ya udhalimu wa mfumo wa kilimwengu wa Marekani, makruseda na Mayahudi. Mayahudi wameanzisha mashambulizi ya makombora dhidi ya Waislamu mbele ya kamera, wakatoa picha za droni za mujahidina wakiuawa shahidi, kuwanyima chakula Waislamu na kutangaza katika televisheni maiti za watoto kwenye matangazo ya moja kwa moja. Mayahudi wamewabaka wanawake wa Kiislamu, wamefunga mikono na miguu ya Waislamu, na kuwapiga risasi, na wengine walizikwa wakiwa hai, na wengine walisagwasagwa chini ya vifaru. Mayahudi hawaoni hata haja ya kuficha uhalifu wao, kwa sababu ya watawala wa Waislamu. Mayahudi wanayachukulia majeshi ya Waislamu si zaidi ya wadudu, kwa sababu ya watawala wa Waislamu. Kwa hiyo waondoe watawala hawa wanafiki na wafisadi, ambao wamekudhoofisheni mbele ya watu waoga kuliko watu wote, Mayahudi. Hizb ut Tahrir ndio jukwaa pekee linalokulinganieni nyinyi kutoa Nussrah yenu kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume. Ni Khilafah ndiyo itakuwa sababu ya kifo cha umbile la Kiyahudi na itapiga pigo la mwisho kwa mfumo wa kilimwengu unaoporomoka wa Marekani, ambao unafichuliwa katika dhulma zake duniani kote. Kwa hivyo Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Chukueni hatua sasa ili Mwenyezi Mungu (swt) akupe heshima kubwa ya kuviamrisha vikosi na askari watakaoikomboa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina na Al-Masjid Al-Aqsa.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu