Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
H. 12 Muharram 1446 | Na: 1446 / 01 |
M. Alhamisi, 18 Julai 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Waislamu wa Pakistan Wanashikiliwa Mateka na Watawala kwenye Mpango Angamivu wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa
(Imetafsiriwa)
Mnamo tarehe 13 Julai, 2024, Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) ulithibitisha katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kwamba Pakistan na IMF wamefikia makubaliano ya kifurushi cha mkopo wa msaada wa dolari bilioni 7, wakidai kuwa “Programu hiyo mpya inalenga kuunga mkono juhudi za mamlaka za kuimarisha utulivu wa uchumi mkuu.” Mpango huo wa IMF bado haujapokea kibali chake cha mwisho kutoka kwa Bodi ya Utendaji ya IMF. Huu ni mpango wa ishirini na nne wa IMF wa Pakistan, ambao Waziri Mkuu Shehbaz Sharif alidai, “Ni wakati wa kuhakikisha kuwa huu ni mpango wetu wa mwisho wa IMF.” Hata hivyo, Waziri Mkuu anawahadaa tu Waislamu kwa niaba ya mabwana zake wa kigeni. Kwa hakika, zaidi ya mwaka mmoja uliopita, mnamo tarehe 30 Juni, 2023, siku ya Makubaliano ya Ngazi ya Wafanyikazi kwa mpango wa 23 wa IMF, Shahbaz Sharif alidai vivyo hivyo. Wakati huo pia ilisemwa kwamba mpango huu wa dolari bilioni 3 ungekuwa mpango wa mwisho wa IMF wa Pakistan. Kabla ya hapo, kaka yake mkubwa na kiongozi, Nawaz Sharif, alikuwa ametangaza kukata mzunguko wa deni wakati wa uongozi wake. Kwa hivyo mtu yeyote anawezaje bado kuzipa umuhimu wowote kwa kauli za vibaraka hawa wa ukoloni?
Je! Waziri Mkuu angependa kuwa wazi kwa watu ni kwa umbo gani watu watalazimika kubeba gharama ya kifurushi hiki kipya? Ni “utulivu gani wa uchumi mkuu” unaotekelezwa kwa kuongeza kodi kwa 40%, ndani ya kipindi cha mwaka mmoja tu? Kodi mpya zimetozwa kwa kila kitu kuanzia unga wa maziwa ya watoto hadi madawa, dengu hadi sukari, viatu hadi nguo, elimu hadi afya, chakula cha mifugo hadi petroli na umeme hadi gesi. Viwango vya ushuru vimeongezwa, au bei zao halisi zimeongezwa. Ongezeko la ushuru kwenye mapato ya watu ni kando na mizigo yote hii. Katika nchi ambayo kiwango cha umaskini ni 40% kulingana na ripoti ya Benki ya Dunia ya 2023, sera za IMF za kupunguza matumizi, kupunguza mahitaji na kuondoa ruzuku zitasababisha njaa zaidi, madeni na watu kujiua. Je, maridhiano kuhusu madeni, umaskini na mahitaji ya msingi yatatoka kwa umbo gani sasa? Hakika watawala na mabwana zao wakoloni wanafahamu vyema. Hata hivyo, watawala hawa “wanacheza huku Roma ikiteketea,” kwa sababu wamejiwekea bajeti, wakiongeza matumizi ya serikali kwa karibu asilimia mia moja kwa miaka miwili.
Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) ni taasisi ya kikoloni. Inadumisha utawala wa dolari ya Kimarekani kote ulimwenguni, kupitia sera za uchumi wa uliberali mamboleo. Inatumia zana za mfumo wa ulimwengu kuzuia nchi zinazoendelea kutokana na maendeleo, na kupitisha sera huru za kiuchumi. Inazifanya dola ndogo ndogo kuwa vitengo vya uzalishaji tu katika misururu ya ugavi duniani, ili kunufaisha uchumi wa dola kubwa zenye nguvu duniani. Inafanya hivyo hata kama hii itasababisha uharibifu wa kiuchumi na utumwa wa kisiasa wa watu wa nchi hiyo. Hili ndilo lengo halisi la IMF. Utulivu wa uchumi mkuu ambao haukutokana na programu 23 za IMF za hapo awali hautatoka kwenye mpango wa 24 wa IMF pia. Njia pekee ya kusonga mbele kwa Waislamu ni kuunganishwa kwa Ulimwengu wa Kiislamu kupitia kuanzishwa kwa Khilafah kwa Njia ya Utume. Hatua hii pekee ndiyo itakayotufanya kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi mkubwa duniani na kuhakikisha uhuru wetu. Rasilimali za Ulimwengu wa Kiislamu zinatuwezesha kupinga dola kubwa, na kuchukua nafasi muhimu katika kuunda siasa za kimataifa na uchumi wa dunia. Kwa hivyo Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Acheni kuwa watazamaji wa kuuangalia Ummah katika dhiki, unyonge na kukata tamaa. Jitokezeni na muchukue hatua kuelekea kwenye mabadiliko ya kina katika hali ya Ummah kwa kutoa Nussrah kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume. Amesema Mwenyezi Mungu (swt),
[وَمَنْ أَعْرَضَ عَنْ ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنْكاً]
“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki.” [Surat Taha 20:124].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Pakistan |
Address & Website Tel: +(92)333-561-3813 http://www.hizb-pakistan.com/ |
Fax: +(92)21-520-6479 E-Mail: htmediapak@gmail.com |