Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  9 Dhu al-Hijjah 1445 Na: 1445 / 47
M.  Jumamosi, 15 Juni 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Watawala wa Pakistan wanatekeleza Ukamataji ili Kuzuia Hizb ut Tahrir Kutaka Kuhamasishwa kwa Jeshi la Pakistan Kuinusuru Gaza. Badala ya Kushambulia umbile la Kiyahudi, Watawala Wanawashambulia Waislamu

(Imetafsiriwa)

Huku Mayahudi wa Kizayuni wakivuka mipaka yote katika ukatili wao, wito wa kampeni ya kisiasa ya Hizb #ArmiesToAqsa umefika kila barabara na kila kona, kwa Fadhila za Mwenyezi Mungu (swt). Wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali, viongozi wa kisiasa, wanaharakati wa mitandao ya kijamii na umma kwa jumla sasa wote wanazidi kuimba, “Enyi Majeshi ya Waislamu, nendeni Palestina, nendeni Palestina.” Matakwa ya kuhamasishwa majeshi kuinusuru Gaza yamezua shinikizo kubwa kwa watawala. Yamefichua kuwezesha kwao Marekani na umbile la Kiyahudi, kupuuza kwao Waislamu na uadui wao dhidi ya Uislamu. Bila hata hoja moja ya Kiislamu au dalili inayowaunga mkono, watawala wanalipiza kisasi cha kikatili kwa Hizb ut Tahrir. Wameanzisha msako dhidi ya Mashababu wa Hizb ut Tahrir. Nyumba za Mashababu wa Hizb zinavamiwa. Familia zao zinanyanyaswa. Mashababu wametupwa kwenye seli za jela. Watawala wamefanya hivyo kana kwamba matakwa ya kuhamasishwa majeshi ni dhambi kubwa. Wamefanya hivyo kana kwamba kuwanusuru Waislamu wanaodhulumiwa sio faradhi kubwa, iliyowekwa na Mwenyezi Mungu (swt) juu ya watawala na majeshi!

Kesi za mashtaka ya "ugaidi" zinasajiliwa dhidi ya Mashababu wa Hizb ut Tahrir. Wengine wangali wamepotezwa kwa nguvu. Wengine wanadhalilishwa katika vituo vya polisi na mahakama. Watawala hawa bado hawajapata funzo kwamba mapambano ya kisiasa ya kuhamasishwa majeshi hayatakoma chini ya ukandamizaji wowote. Ni nishani ya heshima kwa Mashababu wa Hizb ut Tahrir kwamba wamedhulumiwa kwa sababu walitoa wito wa kuangamizwa kwa umbile la Kiyahudi na kukombolewa kwa Al-Masjid Al-Aqsa. Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt), Mashababu hao wataendelea na matembezi yao, kwa mujibu wa Hadith ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ambaye amesema:

«أَلَا لَا يَمْنَعَنَّ أَحَدَكُمْ رَهْبَةُ النَّاسِ أَنْ يَقُولَ بِحَقٍّ إِذَا رَآهُ أَوْ شَهِدَهُ فَإِنَّهُ لَا يُقَرِّبُ مِنْ أَجَلٍ وَلَا يُبَاعِدُ مِنْ رِزْقٍ»

“Asiwaogope mmoja wenu watu kutokana na kusema Ukweli, pindi anapouona au kuushuhudia, kwani hakika yake kufanya hivyo haifupishi uhai (Ajal) wala haiweki mbali riziki (Rizq).” [Ahmad]. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) aikubali mihanga hii kama udhuru wa Mashababu hao Siku ya Kiyama. Tunaomba mihanga hii ichume Nasr ya Mwenyezi Mungu (swt), ambayo itamaliza udhalilifu uliotuzonga leo.

Ama watawala hawa, wanakataa kuyahamasisha majeshi yetu dhidi ya Mayahudi, na badala yake wanafanya msako wa kikatili dhidi ya Hizb ut Tahrir! Watawala hawa ni panya mbele ya maadui wa Mwenyezi Mungu (swt), na simba wakali dhidi ya Waislamu. Watawala hawa wanabeba misimamo ya kikatili dhidi ya walinganizi wanyoofu wa Uislamu, licha ya kuwa Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[إِنَّ الَّذِينَ فَتَنُوا الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ثُمَّ لَمْ يَتُوبُوا فَلَهُمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمْ عَذَابُ الْحَرِيقِ]

“Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua.” [Surah Al-Buruj 85:10] Wanajitahidi kuwanyamazisha waja watiifu wa Mwenyezi Mungu (swt) licha ya kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«ومن عادى أولياء الله فقد بارز الله بالمحاربة»

“Yeyote atakayewafanyia uadui Awliya (vipenzi) wa Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu amekwisha tangaza vita na Mwenyezi Mungu.” [Hakim ameisimulia kama Sahihkutoka kwa Mu'aadh bin Jabal.]! Hivyo, Enyi Vikosi vya Usalama! Musipate ghadhabu na adhabu ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa kuwatii watawala hawa. Hamtakuwa na udhuru wowote mbele ya Mwenyezi Mungu (swt) Siku ya Kiyama pindi Mashababu wa Hizb ut Tahrir watakapotoa malalamiko yao dhidi yenu.

Enyi Waislamu wa Vikosi vya Usalama! Hapana shaka kwamba serikali za madhara katika nchi za Kiislamu zinaogopa mlipuko wa Ummah, wakiwemo watu wenye nguvu miongoni mwa majeshi. Kwa hivyo unazipata huduma zote za usalama ziko kwenye tahadhari katika nchi mbalimbali za Kiislamu. Wanajua vizuri sana, kama vile mabwana zao wanavyojua, kwamba Hizb ut Tahrir ndio tishio halisi na la pekee kwa ushawishi wao muovu duniani. Hakika, Mwenyezi Mungu (swt) ni Mbora wa wapangaji. Dola hizi zilizofeli zinawaandama Mashababu kwa sababu hii, kama vile dola ya Kiyahudi inavyowaandama Mashababu. Dola ya Kiyahudi imewakamata Mashababe wengi wanachangamfu, ambao wanajulikana vyema kwa kutoa wito kwa majeshi ya Waislamu kuinusuru Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina. Watawala na Mayahudi wote ni vibaraka wa nchi za kikoloni zilizoivunja Khilafah, zikagawanya Ummah, na kuasisi umbile la Kiyahudi lenye saratani katika moyo wa Ummah. Kila mtu anayepambana na Magharibi na kufanya kazi kwa bidii ili kuregesha utukufu wa Ummah anakandamizwa na kutupwa magerezani. Kwa hivyo, enyi Waislamu wa Vikosi vya Usalama! Achaneni na watawala hawa na muwe upande wa Umma wa Kiislamu.

Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Tayari mumechelewa kuitikia wito wa Hizb ut Tahrir. Kwa nini? Hizb ut Tahrir ni uongozi wenye ufahamu ambao umewasilisha msimamo wa wazi kwenu katika kila tukio na kila mada, kwa miongo kadhaa. Hizb ut Tahrir ni uongozi shupavu na wa kweli usioogopa kudhulumiwa na dhalimu yeyote. Hizb ut Tahrir inajitahidi kwa mujibu maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw) na maslahi ya Ummah. Leo, Hizb ut Tahrir inawataka waziwazi kwamba muung'oe uongozi huu kibaraka na mumpe Nusrah Amir wa Hizb ut Tahrir, Sheikh Ata Bin Khalil Al-Rashtah, ili kusimamisha Khilafah Rashida ya Pili. Ni Khalifa Rashid ndiye atakayekupeni heshima ya kupigana mstari wa mbele kwa ajili ya ukombozi wa Al-Masjid Al-Aqsa na ardhi iliyobarikiwa. Chini ya amri yake, mutapigana na Mayahudi. Kisha mutakuwa na heshima ya kuwa mlinzi wa dada zenu na watoto wenu. Baada ya jeshi la Salah al-Din Ayyubi, mtapata fursa ya kuswali katika Msikiti wa Al-Masjid Al-Aqsa kama washindi. Basi je, hamtasonga kupata Jannah ambayo upana wake ni kama mbingu na ardhi?

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu