Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  6 Sha'aban 1444 Na: BN/S 1444 / 11
M.  Jumapili, 26 Februari 2023

 Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
(مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُواْ مَا عَاهَدُواْ اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُواْ تَبْدِيلاً)

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab 33:23]
(Imetafsiriwa)

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina inamuomboleza mmoja wa Mashababu wa Hizb, marehemu mbebaji dawah, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt):

Ustaadh Ahmad Helmi Musa (Abu Abdullah)

ambaye alifariki kwenda kwa rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu katika mji wake wa Qaryut, Nablus, mnamo Jumamosi, tarehe 25/2/2023, baada ya kupambana na maradhi aliyompata Mwenyezi Mungu, alikuwa mkakamavu, mwenye subira, na mnyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu.

Ustadh Ahmad Helmy alikuwa mmoja wa Mashababu wachamungu na safi wa Hizb. Alitumia maisha marefu katika safu za Hizb, akiwa muendelevu na imara, akifanya kazi ngumu ya kiidara. Hakuchoka wala hakupuuza, na alimuonesha Mwenyezi Mungu wema kutoka kwake.

Abu Abdullah anashuhudiwa kwa uadilifu wake, uchamungu, na tabia zake zilizonyooka, na hata baada ya Mwenyezi Mungu kumsibu na maradhi ambayo yalikuwa yamezidi hivi karibuni, hakumuonyesha Mwenyezi Mungu ila kuridhika na utambuzi wa Qadhaa yake, na kimbilio jema na dua Kwake.

Mwenyezi Mungu amrehemu maiti wetu, na amjaalie katika Jannah yake pana pamoja na Manabii, wakweli, mashahidi na watu wema. Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake sote tutarejea. Mwenyezi Mungu awamiminie subra na faraja familia na jamaa zake, na sisi hatusemi ila yale tu yanayomridhisha Mwenyezi Mungu. Ni cha Mwenyezi Mungu kile alichotoa, na ni chake kile anachokichukua, na amekadiria kila kitu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Kalima ya Mhandisi Baher Salah katika mazishi ya mbebaji dawa Ustadh Ahmad Helmi Musa (Abu Abdullah)

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu