Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  2 Dhu al-Hijjah 1445 Na: BN/S 1445 / 15
M.  Jumamosi, 08 Juni 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Damu Safi ya Waislamu haina Umuhimu kwa Watawala wao...

Hivyo Adui Wao Muovu Anaimwaga kwa Wingi!

 (Imetafsiriwa)

Mamia ya mashahidi na waliojeruhiwa ni matokeo ya operesheni ya kihalifu na mauaji ya kinyama yaliyotekelezwa na umbile la Kiyahudi leo, Jumamosi, tarehe 8/6/2024 katika kambi ya Nuseirat katika Ukanda wa Gaza. Idadi kubwa ya vikosi na vifaa vyake vilitumwa, chini ya kifuniko kikubwa cha uhalifu na umwagaji damu, ili kuwaacha huru wafungwa wake wanne.

Operesheni hiyo ya kihalifu ilifanywa kwa ushiriki wa moja kwa moja wa Marekani, mfadhili anayeunga mkono umbile hilo la kihalifu na uhalifu wake na wakati huo huo ikisimamia mazungumzo ya "usitishaji mapigano", ambayo inathibitisha kwamba damu ya watu wa Gaza na watoto wao iko nje ya mahesabu na mazingatio yake, ujanja wake na mipango yake.

Kukombolewa kwa wafungwa wanne wa adui huyo baada ya miezi minane ya vita hakutarudisha ari ya adui iliyoporomoka, wala haitaregesha heshima yake, ambayo imefunikwa na vumbi, wala haitarudisha kizuizi chake kilichoanguka. Haitaipa umbile hilo ushindi wa udanganyifu na usiowezekana ambao viongozi wake wahalifu wanatafuta. Ni kutoa tu visingizio vya uhalifu wake dhidi ya raia na watoto, na ukubwa wa umwagaji damu, ili kuficha kushindwa kwake na udhaifu na aibu yake, ambayo ilifichuliwa mikononi mwa Mujahidina mashujaa.

Jukumu la kila nafsi isiyo na hatia iliyopotea katika mauaji ya leo, na kila siku, na kila damu isiyo na hatia iliyomwagika, liko kwenye shingo za watawala wahalifu wa Waislamu kabla ya wengine. Hao ndio waliowakabidhi watu wa Palestina na watoto wao, damu zao na shingo zao, kwa Marekani na umbile la Kiyahudi, ili wawaue wapendavyo. Umbile ya Kiyahudi na mfadhili wake, Marekani, si chochote ila ni adui. Tumekuwa tukijua kuhusu chuki na uhalifu wao, na mbwa mwitu huyo si wa kulaumiwa kwa uvamizi wake. Kwa nini wasiwaue watu wa Palestina wakati watawala wahalifu wanatafuta kufikia usalama wa umbile hilo, na kuliahidi kwa kuhalalisha mahusiano badala ya kulipiza kisasi, badala yake wanakula njama nao.

Kinachoumiza moyo ni kwamba tukio hilo linaitwa "Ukombozi wa Mateka Wanne," sio mauaji yaliyosababisha mamia ya mashahidi na majeruhi. Kinachoumiza moyo vile vile ni kwamba adui yetu anarusha nguvu na silaha zake zote katika vita vyake ili kuwakomboa mateka wake, wakati hakuna hata risasi moja iliyopigwa kwa ajili ya damu nyingi za watu wa Gaza, na hakuna chochote kilichofanywa na watawala wa Waislamu katika kujibu isipokuwa udhalilifu, na udhalilifu zaidi, na shutuma za uwongo za nje huku ndani kukiwa na njama na usaliti. Hii ni kwa sababu Waislamu na roho zao sio muhimu kwa watawala wao wahalifu. Inatia uchungu kuwaona makafiri wahalifu wakishindana wao kwa wao, licha ya tofauti zao, ili kusaidiana wao kwa wao na kuliunga mkono umbile hilo katika batili yake, huku Waislamu wa Palestina wakiachwa bila msaada kutoka kwa wale ambao Mwenyezi Mungu amewapa wajibu wa kuwanusuru, watu wenye nguvu na silaha miongoni mwa Waislamu!

Kadhalika, jukumu la nafsi zisizo na hatia na damu safi liko juu ya mabega ya kila mtu aliye na nguvu wa kuleta mabadiliko, miongoni mwa vikosi na majeshi, na hachukui hatua ya kuwapindua watawala hao wasaliti, kuwanusuru ndugu zake na kulipiza kisasi cha damu yao. Yaliyotokea Nuseirat, pamoja na uzito wake, si mapya ya aina yake, bali yamekuwa yakiendelea kwa muda wa miezi minane, na kushindwa kwa watawala na kudharau damu na roho za Waislamu pia si jambo geni. Badala yake, imekuwa ikitokea kwa miongo kadhaa, na watawala hawa wasipoondolewa kwenye viti vyao vya enzi, umwagaji damu huu utaendelea, na kushindwa na usaliti kutaendelea pamoja nayo.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انفِرُوا فِي سَبِيلِ اللهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ أَرَضِيتُم بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ]

“Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache.” [At-Tawba: 38]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu