Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  8 Muharram 1446 Na: BN/S 1446 / 02
M.  Jumapili, 14 Julai 2024

Tangazo kwa Vyombo vya Habari
Kusitisha Majukumu ya Ndugu Alaa Abu Saleh katika Afisi ya Habari

(Imetafsiriwa)

Bismillahi Ar-Rahman Ar-Rahim

Alhamdulilah, rehma na amani zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw),

Kwanza, napenda kutoa shukrani zangu kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Mwenyezi Mungu amhifadhi, kwa amana na fursa aliyonipa kufanya kazi ndani ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina katika kipindi cha miaka iliyopita. Nimemuomba Mwenyezi Mungu (swt) aifanye juhudi yangu ya unyenyekevu kuwa mchango katika mradi wa mwamko wa Ummah na kuifanya kuwa ya ikhlasi kwa ajili ya kazi Yake tukufu. Namuomba (swt) awape Waislamu ushindi na tamkini kwa kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Khilafah ambayo itaikomboa Masra, wafungwa wa kivita na kuwaletea ushindi watu wa Gaza na Palestina, na kulipiza kisasi kwa wakoloni wote waliosubutu kuwashambulia Waislamu, kuikalia kwa mabavu ardhi yao, na kuinajisi Masra ya Mtume wao (saw).

Zaidi ya hayo, natangaza kusitisha kazi yangu katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina, ili kutoa nafasi kwa nguvu changa zinazoingiza uchangamfu na mng'aro, na kuiingiza kazi hii damu mpya na mbinu mbalimbali. Namuomba Mwenyezi Mungu (swt) kwa ajili ya ndugu zangu katika Afisi ya Habari mafanikio na ustawi, na kwamba daima wawe ni sauti kubwa ya kutangaza haki, na kwamba kheri itiririke mikononi mwao. Kutokana na haya, hii ni taarifa kwa vyombo vya habari inayosema kwamba sina tena uwezo rasmi wa kuzungumza na vyombo vya habari.

Salamu za dhati,

Alaa Abu Saleh

Kwa upande wetu sisi katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina, tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) azikubali juhudi za Ustadh Alaa Abu Saleh na amlipe malipo tele kwa kazi zote alizozifanya katika miaka aliyohudumu katika Afisi hii ya Habari.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu