Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  10 Rabi' II 1446 Na: BN/S 1446 / 09
M.  Jumapili, 13 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tubas ni Shahidi wa Upendeleo wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina dhidi ya Maadui wa Palestina na Watu wake
(Imetafsiriwa)

Kwa kuzingatia mandhari ya Ukanda wa Gaza na kaskazini mwake, na kitendo cha jinai cha Kiyahudi kufanya upya mashambulizi ya mabomu baada ya mabomu, mauaji baada ya mauaji, na kuhamishwa makaazi baada ya makazi, na kwa kuzingatia mandhari ya mauaji yanayoendelea katika Ukingo wa Magharibi; sio mwisho kabisa ni kuuawa kwa vijana wanne kutoka Nablus kwa mikono ya wale ambao ghadhabu ya Mwenyezi Mungu iko juu yao, kinyama, katika eneo lililo chini ya mamlaka ya Mamlaka ya Palestina (PA) kama inavyodai, na ikiwa ina hata chembe ya hadhi, mandhari hiyo ingetosha kwake kumaliza uhusiano wake nao.

Mamlaka hiyo ambayo haiondoi uchokozi wa jeshi la umbile halifu la Kiyahudi au magenge yake ya walowezi kutoka kwa watu wa Palestina, bali inashirikiana nalo na kutii amri zake, na matokeo yake inazidisha udhalilifu wake kwa kuizingatia Ramallah kuwa ni sehemu ya kazi ya gavana wa jeshi. Ni mamlaka hiyo ambayo mradi wake unaodaiwa wa kijidola ulioegemezwa juu ya uhaini na kutelekezwa kwa ardhi ya Isra na Mi'raj ulikanyagwa na umbile la Kiyahudi kwa miguu yake, lakini uhaini wake unabakia.

Ni zaidi ya uhaini, kwamba Mamlaka ya Ndani ya Palestina inatangaza uadui wake kwa watu wa Palestina, kama inavyotokea kwa kuwasaka Mujahidina wa Tubas, kuwakamata na kuwapiga risasi, kuwatawanya watu huko kwa gesi ya machozi, kuwaua Mujahidina na kuwatia nguvuni kama wafanyavyo Mayahudi, sawa kwa sawa, na kutenda kwa niaba yake kwa kujaza pengo wakati inashughulika na uvamizi wake dhidi ya Gaza na Lebanon.

Hatushangazwi na haya kutoka kwa mamlaka iliyozoeleka kumfanyia khiyana Mwenyezi Mungu, Mtume wake na watu wa Palestina, tangu ilipoanza safari yake na PLO, iliyofanya kila dhambi popote ilipokwenda, mpaka ikafikia dhambi kubwa zaidi kwa kuisalimisha Palestina. Hatushangazwi na hili kutoka kwa yule aliyeasisiwa kwa wazo la kuishi chini ya viatu vya uvamizi na kutukuza ushirikiano nao (uratibu wa usalama); msemo huo ni wa mapambo ili kulinda umbile la Kiyahudi na kupigana na yeyote anayetishia usalama wake.

Tunachokiona cha ajabu ni matendo ya wana wa vyombo vya usalama vya Mamlaka ya Ndani ya Palestina, ni vipi walikuwa na uwezo wa kuwaua ndugu zao na watu wao, kuchora picha mbaya zaidi ya mtoto muasi aliyeiasi familia yake na kuwafuata wahalifu, na alikubali kuwa silaha ya adui ya kuwashambulia ndugu zake?! Labda wanafikiria kuwa PA itaangamia, ikiwa sio leo basi kesho, iwe kabla au kwa ukaliaji kimabavu. Viongozi wake watajaribu kung’ang’ania upepo ili waepuke mwisho wao mbaya, nao watawaacha bila kuwajali wala kujali hatima yao.

Enyi Wana wa Huduma za Usalama za Mamlaka ya Palestina: Tunakunasihini mtubu kwa Mwenyezi Mungu na muachane na ndugu zenu, labda wakati bado haujapita, na muwe upande wa watu wenu. Mkifanya hivyo ni bora kwenu, na msipofanya hivyo mtakuwa mmechagua kusimama na maadui zao, na hayo yana madhara katika dunia hii na kesho Akhera, kwa yeyote mwenye moyo wa kuzingatia na akatega sikio linalosikiliza.

Kinachoumiza zaidi ni kwamba Ummah pamoja na watu wake na askari wake wamewaacha watu wa Palestina kwa adui aliye na udhibiti juu yao, na kwa mamlaka ambayo inawakunja na kufanya uratibu pamoja na adui yao. Hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, kumtegemea kwetu Mwenyezi Mungu na ahadi yake havina mpaka.

[‌وَلَا ‌تَحْسَبَنَّ اللهَ غَافِلاً عَمَّا يَعْمَلُ الظَّالِمُونَ]

“Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayo yafanya madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatapo kodoka macho yao.” [Ibrahim: 42]

[إِنَّ اللهَ ‌بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْراً]

“Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake.” [At-Talaq: 3]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu