Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  20 Safar 1446 Na: BN/S 1446 / 05
M.  Jumapili, 25 Agosti 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mamlaka ya Palestina Iliyofungamana na Maadui wa Mwenyezi Mungu Yakamilisha Dori ya Ghadhabu katika Kuwatesa Watu wa Palestina na Kuwakamata Watetezi wa Haki
(Imetafsiriwa)

Siku chache zilizopita, vikosi vya usalama vya Mamlaka ya Ndani ya Palestina (PA) viliwakamata Sheikh Aws Abu Arqoub na Sheikh Muhammad Manasrah, wanachama wa Hizb ut Tahrir. Kwa kuwakamata wale wanaosema ukweli, PA na vikosi vyake vinasisitiza kuwa kiongozi wa Mayahudi, wakidunga visu watu wote wa Palestina. Hali ya sasa inaakisi vitendo vya Mamlaka hiyo; umbile halifu linalokalia kwa mabavu lilimkamata Dkt. Musab Abu Arqoub, mjumbe wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina, zaidi ya miezi sita iliyopita. Leo hii, PA na vyombo vyake vinamkamata kaka yake Aws Abu Arqoub, kama kusema kwamba wanajumuisha chuki ya Mayahudi dhidi yetu. Adui anakichoanzisha, PA inakamilisha, na hili sio jipya katika misimamo ya Mamlaka ya Palestina. Ni Mamlaka hiyo hiyo inayoua, kuwaandama, na kuwakamata Mujahidina huko Jenin, Tulkarm, Nablus, Bethlehem, na kwengineko, ikitoa njia pamoja na usaliti wake kwa adui kuua, kukamata, na kuharibu.

Kwa vitendo hivi vya uhalifu, PA inaongeza jeraha jengine kwa watu wa Palestina, ambao tayari wameumizwa sana na adui yao, na huongeza mateso yao. Watu tayari wanakabiliwa na mauaji, kufukuzwa, njaa, kuzingirwa na kubomolewa kwa nyumba mjini Gaza na Ukingo wa Magharibi. Jela zao zimejaa Mujahidina, wazee, watoto, wanawake na wasema ukweli, wakiwemo Mashababu wa Hizb ut Tahrir, ambao ni sehemu ya watu wa Palestina na ni watetezi wa ukombozi wa Ummah wa Palestina na afueni ya Gaza na watu wake mchana na usiku. Wito huu humvuruga adui, husumbua usingizi wao, na huvuruga maisha yao kama vile Mujahidina wa Gaza wanavyofanya.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa, kama vile watu wa Palestina, wako imara kama mti mzuri uliokita mizizi ardhini. Kinyume chake, PA ni kama mti muovu, usio na uthabiti, unaokaribia kung'olewa na upepo kutoka kwa watu wa Palestina, na kutupwa mahali penye kina kirefu pamoja na Mubarak, Gaddafi, Ben Ali, na wale waliokuwa kabla yao waliomfanyia khiyana Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kuudhulumu Umma. Kama PA ingekuwa na akili yoyote, ingekata mafungamano yake na maadui wa watu wa Palestina kabla ya kukabiliwa na adhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu au mikononi mwa watu wa Palestina na Umma mzima.

[إِنَّ الَّذِينَ ‌يُؤْذُونَ اللهَ وَرَسُولَهُ لَعَنَهُمُ اللهُ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَأَعَدَّ لَهُمْ عَذَاباً مُهِيناً * وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ بِغَيْرِ مَا اكْتَسَبُوا فَقَدِ احْتَمَلُوا بُهْتَاناً وَإِثْماً مُبِيناً]

“Hakika wanao muudhi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Mwenyezi Mungu amewalaani duniani na Akhera, na amewaandalia adhabu ya kufedhehi. Na wale wanao waudhi Waumini wanaume na wanawake pasina wao kufanya kosa lolote, bila ya shaka wamebeba dhulma kubwa na dhambi zilio dhaahiri.” [Surat Al-Ahzab:57-8]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 0598819100
www.pal-tahrir.info
E-Mail: info@pal-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu