Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  20 Rabi' II 1443 Na: HTS 1443 / 10
M.  Alhamisi, 25 Novemba 2021

 Majibu kwa Vyombo vya Habari
(Imetafsiriwa)

Mpendwa Ndugu Ustadh Mohammed Abdullah Ya’qub

Assalam Alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatuh,,,

Tumesoma maoni yenu juu ya toleo la Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan lenye kichwa: "Makubaliano ya Burhan na Hamdok... Nchi Yetu Itakuwa Uwanja wa Mizozo ya Kimataifa Mpaka Lini?!", katika safu yenu ya makala Safar Al-Qawafi, katika Gazeti la Al-Ahram Al-Yawm, mnamo Alhamisi, 25/11/2021. Tutashukuru iwapo mtaturuhusu kujibu maoni yenu.

Kwanza: Shukrani zetu za dhati na kuridhika kikamilifu na gazeti lenu, na kwa mkuu wenu, ambaye daima azoea kuchapisha kupitia safu yake machapisho ya Hizb ut Tahrir, wakati ambapo wanahabari wengi na vyombo vya habari wanapuuza wanayoyapokea kutoka kwa machapisho ya Hizb; matoleo yake, taarifa zake nk zinazohusu kadhia zinazowaka moto na muhimu katika medani ya siasa za Sudan au kwingineko, kwani hawayataji ima kwa ubaya au kwa uzuri, au hata suala la habari, ambalo haliendani na ukweli wa kitaaluma na kudai kutokuwa na mapendeleo.

Pili: Madai yenu ya kwamba Hizb ut Tahrir inamuunga mkono Al-Burhan kwa kusema: “Sasa Hizb ut Tahrir imedhihirisha mapenzi yake kwa Al-Burhan bila ya ubishani...” ni kauli inayopingana na ukweli. Njia ya Hizb ut-Tahrir ina uangavu wa hali ya juu kama vile jua ling'aavyo katikati ya mbingu, kwani inataka kuregelea maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Inafanya kazi na Ummah kuifanya kadhia hii kuwa nyeti kwake, na inawataka watu wenye nguvu na ulinzi kukabidhi mamlaka kwa Ummah, kuinusuru Hizb ut Tahrir kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, na kutoa kiapo cha utiifu kwa Khalifa atakayesimamisha miongoni mwao Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Sunnah za Mtume Wake (saw). Ama Al-Burhan na watawala wengine wa Waislamu katika sehemu za dunia, kwa mtazamo wetu wote ni vibaraka, wanatawala kinyume na yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, na wanatekeleza njama za mkoloni Kafiri katika nchi za Waislamu. Vilevile, yako wapi hayo mapenzi katika taarifa iliyoonyesha kuwa yanayojiri nchini Sudan ni mzozo wa Amerika (inayowakilishwa na Al-Burhan na walio pamoja naye), na wa Uingereza (inayowakilishwa na Hamdok na kundi lake)?!

Tatu: Mazungumzo yenu na madai yenu ya Hizb ut-Tahrir kupanua mgawanyiko, na maono yanayotofautiana katika majimbo mia moja (kama mlivyotaja)... Tunasema kwamba kugawanyika kulianzishwa na Kafiri wa mkoloni, kwani yeye ndiye aliyeuchana Umma huu vipande vipande kwa kuivunja Khilafah mnamo Rajab 1342 Hijria sawia na Machi 3, 1924, alipozigawanya nchi za Kiislamu katika vijidola vidogo vya kikatuni vya kitaifa ambavyo kazi yake ni kuwatumikia Makafiri wa kikoloni. haviwatumikii Ummah wala mwamko wake, na yale ambayo Hizb ut Tahrir inayafanya ndiyo njia pekee ya mwamko na umoja wa Ummah. Khilafah, kama mjuavyo, ndiyo pekee inayounganisha Ummah ndani ya chombo kimoja cha kisiasa kinachokata mkono wa mkoloni wa Kikafiri aliyehujumu uwezo na rasilimali za nchi yetu kupitia watawala vibaraka wake na baadhi ya wanasiasa na wanahabari.

Kwa kumalizia, tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atujaalie sisi na nyinyi kuwa watetezi wa haki, waaminifu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, wanaojitahidi kuhukumu sheria za Mwenyezi Mungu ardhini kupitia Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu