Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  6 Jumada II 1443 Na: HTS 1443 / 15
M.  Jumapili, 09 Januari 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Sudan Volker Perthes
Atafuta Kuvileta Pamoja Vyama vya Kisiasa nchini Sudan, kwa Njia ya Kiamerika

 (Imetafsiriwa)

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Volker Perthes, alizindua mpango ambao alisema ni wa kukusanya vyama vya Sudan ili kujiondoa katika mzozo wa sasa wa kisiasa kwa mashauriano na kile alichokiita washirika wa Sudan na wa kimataifa. Alisema mpango huo unalenga kusaidia wadau wa Sudan kufikia kujiondoa katika mzozo wa sasa wa kisiasa.

Mara tu baada ya Volker kutangaza mpango wake huo, vikosi vingi vya kisiasa viliukaribisha, kama ambavyo Amerika, Uingereza, Jumuiya ya Kiarabu, Saudi Arabia, Imarati, Misri na zingine ziliukaribisha. Je, mpango huu kweli unatatua matatizo ya Sudan, na kujenga utulivu mamlakani?!

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan tunathibitisha ukweli ufuatao:

Kwanza: Mzozo wa sasa wa viti vya madaraka kati ya jeshi na raia kwa kweli ni mzozo wa kimataifa, wahusika wakuu ndani yake ni Amerika na Uingereza. Wanajeshi na raia sio chochote isipokuwa ala tu za mzozo huu, na vijana wanaouawa kinyama ndio chachu ya mzozo huu. Kinachothibitisha kauli yetu hiyo ni uingiliaji wa waziwazi na vuguvugu la hila la Kiamerika kupitia ubalozi wake na wajumbe wake na yale ambayo Uingereza inayatekeleza pia kupitia balozi na wajumbe wake, na kila mmoja wao anaunga mkono upande mmoja dhidi ya mwingine kwa dhahiri au kwa siri. Marekani inatumia ala zake (Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, na Umoja wa Waarabu).

Pili: Wito wa Volker wa mpango huu ni katika njia ya Kiamerika ya kutatua mgogoro wa Sudan, kwa msingi wa suluhisho la maridhiano ambalo limeegemezwa kwenye itikadi ya kutenganisha dini na maisha. Ambapo kila upande hufanya maridhiano ili kufikia makubaliano ya muda ambayo hayatatui tatizo kwa njia kimsingi, kama ilivyotokea huko nyuma kupitia kile kiitwacho waraka wa katiba mnamo Agosti 2019, uliowaleta pamoja washirika wanaozozana.

Tatu: Marekani haitaacha kuidhibiti Sudan kupitia jeshi, na Uingereza inafahamu hili na itakubali sehemu ndogo ya mamlaka nchini Sudan hadi itakapopata fursa mwafaka ya kukwamisha miradi ya Marekani nchini Sudan. Ambayo ndiyo kazi Uingereza inayofanya sasa kwa kulishinikiza jeshi kupata mapato zaidi. Hivyo basi, tunaona inalazimika kukubaliana na mpango wa Volker licha ya kujua kuwa ni mpango wa Amerika.

Kwa kumalizia: Tunasema kwamba suluhisho la maridhiano ni ndoto isiyokuwepo katika uhalisi, na ni kuupumbaza mzozo wala sio suluhu yake. Suluhisho msingi la mgogoro liko katika kuwepo kwa fikra ya kisiasa iliyojengwa juu imani sahihi inayokinaisha akili na kuafikiana na umbile la mwanadamu (fitra), na kuujaza moyo utulivu. Fikra hii sahihi inapatikana tu katika ulimwengu wa leo katika Uislamu mtukufu na mfumo wake, ambao unachipuza kutokana na itikadi yake yenye hukmu kutoka kwa Al-Latif Al-Khabeer chini ya kivuli cha dola ya Uislamu; Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Enyi wanasiasa, na Enyi wanajeshi, nyote nyinyi ni Waislamu, na watoto wa Waislamu, basi mcheni Mwenyezi Mungu katika damu ya vijana wa Ummah huu, na ondoeni mikono yenu kutokana na mipango ya makafiri wakoloni ambao ni maadui wa Dini hii. Toeni Nusra (msaada wa kijeshi) kwa Hizb ut Tahrir ili kuregesha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume; ambayo kwayo Waislamu huwa na izza, na makafiri hudhalilika.

 [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa  Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu