Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 12 Dhu al-Qi'dah 1443 | Na: 04 / 1443 |
M. Jumamosi, 11 Juni 2022 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Urasilimali Husababisha Njaa na Kuwauwa Wenye Njaa
(Imetafsiriwa)
Mamlaka huko Darfur Kaskazini zilianzisha uchunguzi kuhusu kifo cha watoto wawili kutokana na njaa katika moja ya wilaya za El Fasher, mji mkuu wa jimbo hilo, siku mbili zilizopita. Katika taarifa ya shirika la ‘Save the Children’ mnamo siku ya Jumatano ilidai "inatoa wito wa haraka kwa jumuiya ya kimataifa kuupa kipaumbele mwitiko wa kibinadamu nchini Sudan na kutoa chakula kinachohitajika mno, pamoja na usaidizi wa kimaendeleo wa muda mrefu kwa watoto na familia zao zilizoathiriwa na janga hilo" Nabd, 10/6/2022). Kwa nini haya yanatokea katika nchi inayoitwa kapu la chakula duniani, na neema zake ni nyingi, zinazoonekana na zilizofichika.
Tatizo liko katika kutabanni mfumo wa kirasilimali, ambao waundaji wake hawakutafuta kukidhi mahitaji ya watu, mmoja baada ya mwengine, ili kuwatosheleza kwa mfumo unaohakikisha hili. Badala yake, walitafuta bidhaa na huduma kuhusiana na mahitaji; walisema kwamba ni tatizo la mwanadamu, yaani, idadi isiyotosheleza ya bidhaa na huduma kwa mahitaji yasiyo na kikomo ya mwanadamu, na kwamba hilo ndilo tatizo la kiuchumi la jamii. Kwao, tatizo lilikuwa ni uhaba wa mahitaji. Matokeo yasiyo epukika ni kwamba mtu hatakidhi mahitaji yake, au kuyatosheleza baadhi, kwa hivyo mkate ima utaliwa na mimi au wewe!
Mfumo wa kirasilimali uliolazimishwa na taasisi za kimataifa ni mfumo usio wa kibinadamu unaokosa njia ya kugawanya mali miongoni mwa watu, mmoja baada ya mwengine, na matokeo yake wakaifanya bei kuwa ndio mdhibiti katika ugavi wa mali, yaani, mwenye kumudu bei ndiye anayepata fursa kumiliki vigezo vya uzalishaji mali na kufikia bei yake, atapata mali na atatimiza mahitaji yake, na ambaye hakumudu bei hatapata mali. Hivyo umaskini, njaa na ukosefu wa ajira yalikuwa ndio matokeo yasiyoepukika ya mfumo wa kirasilimali unaotawala dunia leo, ukiongozwa na Marekani.
Jukumu lipo kwa watawala wanaotabikisha sera za kibepari, kwa kuzingatia maamuzi ya Benki ya Dunia na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, zana mbili kuu za ubepari za kuwaua maskini kwa njaa na wasiwasi. Watawala wameshindwa kutoa usalama na ufanisi kwa watu kote duniani. Dunia ilipandwa umaskini, maradhi, vita, njaa na uharibifu.
Uislamu unatatua tatizo hili kimsingi kwa sera yenye thamani ya kiuchumi, kwa kuwawezesha watu wote, kila mtu binafsi kukidhi mahitaji yao ya kimsingi. Huwafungulia njia ya kutosheleza mahitaji yao ya ziada. Uislamu katika mfumo wake wa kiuchumi unazingatia ugavi wa rasilimali na mali kwa namna ambayo hudhamini kushibisha mahitaji ya kimsingi ya wanajamii mmoja baada ya mwengine. Haishangazi kuwakuta miongoni mwa Makhalifa na watawala wa Waislamu wale walioapa kuua umasikini ili kuwahuisha maskini.
Uislamu ulipambana na njaa, na kwa hakika uliimaliza ilipokuwa ukitawala na kutabikishwa. Unamhimiza mtu binafsi kuchuma, kutafuta na kujitahidi kupata riziki, na umeweka uangalizi wa mahitaji (nafaqa) kwa warithi wake endapo atakuwa hawezi, na kisha juu ya Bait Al-Mal (Hazina ya Dola). Urasilimali husababisha njaa na wenye njaa, huku Uislamu unashughulikia tatizo la umasikini na kuwalinda maskini.
Msemaji Rasmi wa Kike wa Kitengo cha Wanawake
katika Hizb ut Tahrir Wilayah Sudan
بالخلافة_نقتلع_نفوذ_الكافر#
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: |