Alhamisi, 24 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  26 Dhu al-Hijjah 1443 Na: HTS 1443 / 45
M.  Jumatatu, 25 Julai 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mabadiliko Msingi Yanaweza Kutokea tu kupitia Khilafah kwa Njia ya Utume Pekee

(Imetafsiriwa)

Ilitangazwa jijini Khartoum kuzaliwa kwa muungano mpya wa kisiasa chini ya jina la Muungano wa Majeshi ya Mabadiliko Msingi, na kwamba haja yake kuu ni kukamilisha matakwa ya mapinduzi ya Disemba chini ya kauli mbiu "Kuelekea kwenye mabadiliko ya kitaifa na ya kimsingi yanayoongozwa na raia". Ilisemekana kuwa mpango huu wa mabadiliko msingi unajengwa juu ya kufikia haki ya kijamii katika sekta na kanda, kumaliza vita, kudumisha amani, bila kutoathiri ubwana na rasilimali za nchi, haja ya kufikia uhamisho wa amani wa mamlaka, na kuunda dola ya kiraia na ya kidemokrasia.

Mwenye kuuchunguza mpango wa muungano huu, uliosemekana kuwa ni kwa ajili ya kuleta mabadiliko msingi, ataona kwamba hauhusiani na mabadiliko hayo msingi, bali ni mabadiliko rasmi ndani ya nidhamu ya mifumo iliyotungwa na mwanadamu iliyopo tangu wakati wa ukoloni hadi sasa, na hakuna jipya ndani yake, si katika msingi yaliyoegemezwa juu yake, wala katika masuluhisho yake, yameegemezwa kwenye mfumo ule ule wa kirasilimali; Itikadi ya kutenganisha dini na dola, na masuluhisho yale yale yaliyofeli ambayo yamekuwa yakitekelezwa katika nchi yetu kwa miongo mingi hadi yakatufikisha ukingoni mwa shimo.

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan tunawasilisha mradi wa mabadiliko msingi ambayo yataiokoa Sudan kutokana na ukandamizaji wake, na hata kuuokoa ulimwengu mzima, kama ifuatavyo:

Kwanza: Kuifanya itikadi ya Kiislamu kuwa ndio msingi wa dola, na wakati huo huo kuwa msingi wa katiba na sheria, kwa kuzingatia kuwa hukmu za Shariah zinatoka kwa Muumba wa wanadamu wote, anayejua yanayowanufaisha na yanayowadhuru.

[أَلَا يَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ]

“Asijue aliye umba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye khabari?” [Al-Mulk:14]

Pili: Ubwana kamili ni kwa sheria, na mamlaka ni kwa Ummah, kwani ndio unaochagua miongoni mwa watu wake mwenye sifa ya kutawala, hivyo kumpa kiapo cha utiifu kwake kuwa Khalifa wake ambamo ndani yake inatekeleza Shariah ya Mwenyezi Mungu, na Uislamu kubeba ujumbe wa uongofu na nuru kwa ulimwengu uliopotea.

Tatu: Ni haramu kabisa kwa Makafiri wa kikoloni kuingilia kati mambo ya nchi na watu, kwa sababu uingiliaji wao unawafanya wawe na mamlaka juu yetu, na Uislamu umeharamisha hilo. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[وَلَنْ يَجْعَلَ اللَّهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلاً]

“Wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.” [An-Nisaa:141].

Nne: Dola ya Khilafah husimamia rasilimali za nchi, haswa zile zinazojumuishwa katika milki ya umma wa dhahabu, mafuta, gesi na nyinginezo kwa manufaa ya watu. Dola hudhamini ushibishaji mahitaji ya kimsingi ya chakula, mavazi na nyumba kwa kila raia. Vile vile inadhamini elimu, matibabu na usalama kwa watu wote, hivyo mizozo huisha kwa dhulma au kutokana na ardhi au mali, na kila mwenye haki huchukua haki yake kwa mujibu wa hukmu za Shariah, hivyo jamii yenye utoshelevu, uadilifu na usalama. hupatikana; Ili dola iweze kujishughulisha na kazi yake kuu ya kuuleta Uislamu duniani kwa njia ya dawah na jihad.

Haya ndio mabadiliko msingi yanayong'oa ushawishi wa kikafiri mkoloni, yanatengeneza maisha ya staha, na kumaliza machafuko haya yanayoikumba nchi, na tunatoka katika ukimbizi wa mifumo dhalimu iliyoegemezwa juu ya mfumo wa kilafi wa kirasilimali.

 

Enyi watu wa Sudan, nyote! Vyama na makundi, Hizb ut Tahrir, huku ikiwa imebeba rasimu ya katiba yenye vifungu 191 vilivyotolewa kutoka katika Quran, Sunnah, Ijma ya Maswahaba na qiyas ya kisheria, inawalinganieni kufanya kazi nayo kwa ajili ya kuleta mabadiliko msingi halisi kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ambayo kwayo mutapata izza na kupata radhi za Mola wenu Mlezi.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24]

 

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu