Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  15 Muharram 1444 Na: 01 / 1444
M.  Jumamosi, 13 Agosti 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mafuriko na Mvua ni Doa kwenye Bapa la Uso la Serikali za Kirasilimali ambazo Hazisimamii Mambo
(Imetafsiriwa)

Mamlaka za Sudan zilitangaza vifo vya watu 51 na wengine 24 kujeruhiwa kutokana na mvua na mafuriko katika majimbo ya Mto Nile na White Nile, kulingana na idhaa ya Al Jazeera mnamo 13/8/2022. Serikali ya jimbo la Mto Nile ilisema mafuriko hayo yalisababisha mmomonyoko wa barabara kuu zinazounganisha jimbo hilo na miji mingine. Kwa upande wake, msemaji wa Baraza la Kitaifa la Ulinzi wa Raia nchini Sudan, Brigedia Jenerali Abdel Jalil Abdel Rahim, alisema kuwa mafuriko yalisababisha kuporomoka kabisa kwa nyumba 5345, kuanguka sehemu kwa nyumba 2845, na kuporomoka kwa vituo 16 vya umma.

Licha ya kujua kwa hakika wakati wa msimu wa vuli, hiyo haibadilishi, habari za kuanguka kwa nyumba juu ya vichwa vya wakaazi wake kutokana na mvua na mafuriko, kuongoza habari kila mwaka. Serikali haisongi kukabiliana nayo, au kufanya chochote kinachobadilisha au kupunguza uharibifu kutokana na hilo. Au hata kutoa msaada na uangalizi mchache ili kupunguza kiwango cha uharibifu, na idadi ya wahasiriwa wanaopoteza maisha, na ambao wanabaki bila makaazi, chakula, au uangalizi kwa masiku kadhaa, hata wiki na miezi!

Hakuna sera za makaazi salama, na idadi ndogo ya familia vijijini zina uwezo mdogo wa kupata vifaa vya ujenzi vinavyostahimili mvua na mafuriko, wengi hawana usalama wa maisha yao wenyewe, kwa hivyo familia hizi zinaishi katika nyumba dhaifu zinazo yaweka maisha yao hatarini. Maeneo haya yanakumbwa na mvua na mafuriko kila mara. Kuna barabara mbovu za msimu pekee, ambazo zinazidisha hali ambapo waathiriwa wa mafuriko wanabaki hoi. Miundombinu hii iliyochakaa katika maeneo yote ya Sudan, ambayo inadhihirisha kutokuwa na uwezo wa serikali kuchunga mambo ya watu, ni doa kwenye bapa la uso lililorithiwa na serikali za kitaifa tangu uhuru unaodaiwa. Hali ya watu itabaki kuwa hivi, pasi na uangalizi, badala yake itazidi kuwa mbaya chini ya mifumo ya sasa ya kirasilimali iliyotungwa na mwanadamu, ambapo maslahi pekee ya wanasiasa ni kung’ang’ania madaraka, na kusukuma mipango inayoimarisha mamlaka ya upande mmoja kwa gharama ya mwengine. Mwanadamu chini ya mfumo huu hupoteza mali yake na huenda akapoteza nafsi yake, hivyo watawala wanastahili ghadhabu na laana ya Mwenyezi Mungu. Imepokewa katika dondoo ya Abu Awana, kwamba Harmala alisema: “Na nilimsikia Ayyash bin Abbas akisema: Mtume (saw) amesema:

«مَنْ وَلِيَ مِنْ أَمْرِ أُمَّتِي شَيْئاً، فَرَفَقَ بِهِمْ فَرَفَقَ اللَّهُ بِهِ، وَمَنْ وَلِيَ مِنْهُمْ شَيْئاً، فَشَقَّ عَلَيْهِمْ فَعَلَيْهِ بَهْلَةُ اللَّهِ، قَالُوا: يَا  رَسُولَ اللَّهِ، وَمَا بَهْلَةُ اللَّهِ؟ قَالَ: لَعْنَةُ اللَّهِ»

Yeyote anayetawalishiwa chochote katika mambo ya Umma wangu, akawa mpole kwao, Mwenyezi Mungu atakuwa mpole naye. Na yeyote atakaye tawalishiwa chochote kwao, akawa mkali kwao, atapata Bahla ya Mwenyezi Mungu. Wakauliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, Bahla ya Mwenyezi Mungu ni nini? Akasema: laana ya Mwenyezi Mungu.”

Makhalifa wa Kiislamu waliweka mifano ya ajabu sana ya kujitolea katika kuchunga mambo ya watu, hadi kufikia kiwango ambacho bwana wetu Omar Ibn Al-Khattab alisema: “Wallahi, lau nyumbu atajikwaa katika njia za Iraq, mimi nachelea kuwa Mwenyezi Mungu ataniuliza kwa nini sikumsawazishia barabara?” Kukabiliana na majanga kama vile mafuriko na mvua, na kuchunga mambo yote ya watu, ni moja ya hatua muhimu zaidi za serikali. Uislamu umelifanya jukumu la kuangalia mambo ya umma juu ya dola. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«الإِمَامُ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ»

“Imam ni mchungaji na atakwenda kuulizwa kuhusu raia wake.”

Hili linaweza kutokea tu chini ya Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume pekee. Kwa mfano wa hili, na wafanye kazi wenye kufanya kazi.

Msemaji Rasmi wa Kitengo cha Wanawake katika Hizb ut Tahrir

Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu