Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  27 Shawwal 1445 Na: HTS 1445 / 35
M.  Jumatatu, 06 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Yakutana na Viongozi wa Harakati ya Islamic Action
(Imetafsiriwa)

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Sudan, ukiongozwa na Ustadh Nasser Ridha, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan, na wanachama Ustadh Abdullah Hussein, Mratibu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano, na Ustadh Muhammad Mukhtar, Mwanachama wa Hizb ut Tahrir, alikutana na idadi ya viongozi wa Harakati ya Islamic Action katika afisi ya Hizb mjini Port Sudan, Jumapili, 26 Shawwal 1445 H sawia na 05/05/2024. Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi wa harakati hiyo ya Kiislamu:

1- Dkt. Abdullah Al-Ardab

2- Sheikh Yasser Bashir

3- Sheikh Al-Khair Al-Obaid

4- Dkt. Zuhair Abdel Rahman

5- Dkt. Zuhair Salah El-Din.

Mkutano huo ulijadili wasiwasi jumla nchini humu, mzozo wa kijeshi unaoendelea nchini Sudan, na uingiliaji kati wa dola za nje na usimamizi wao wa vita hivi, ili kuwezesha mradi wa makafiri wa Magharibi wa kuifanya nchi hii kuwa ya kisekula, kuigawanya na kuivunja vunja. katika vidola dhaifu. Pande hizo mbili ziliafikiana jinsi ya kukabiliana na njama hizi kupitia juhudi za pamoja za wabebaji da’wah, kupitia kueneza ufahamu miongoni mwa umati wa uhalisia wa mpango wa nchi za kikoloni, na ufahamu wa mradi wa kuunganisha Umma unaowakilishwa na kusimamisha chombo kinachounganisha Ummah chini ya Dola ya Khilafah, na kwamba Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan iko katika mchakato wa kufanya kongamano la kujadili masuala ya nchi, na kwamba suluhisho linatoka ndani ya Aqidah (itikadi) ya Kiislamu na sio kwa kuomba masuluhisho ya nje kutoka kwa nchi za kikoloni zenye ulafi katika nchi yetu.

Kwa upande wao viongozi wa Islamic Action wamesisitiza kuwa, suluhisho linapaswa kuegemezwa kwenye Aqida tukufu ya Uislamu, na kufanya kazi ya kuwa kitu kimoja kukabiliana na mipango muovu wa kikoloni, na kwamba wako tayari kufanya kazi katika mwelekeo huu.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

2024 05 06 Sudan OS 1 Pic

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu