Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  26 Shawwal 1445 Na: HTS 1445 / 34
M.  Jumapili, 05 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Yakutana na Mjumbe wa Kamati ya Wanazuoni wa Jimbo la Bahari Nyekundu
(Imetafsiriwa)

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, ukiongozwa na Sheikh Nasser Ridha, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, na akiwemo Abdullah Hussein, Mratibu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano, na Mohammed Mukhtar, Mwanachama wa Hizb ut Tahrir, ulikutana na Sheikh Othman Arefa, mjumbe wa Kamati ya Wanazuoni wa Jimbo la Bahari Nyekundu na Imam wa Msikiti wa Ibn Masoud, mnamo siku ya Jumamosi, 25 Shawwal 1445 H sawia na 4 Mei 2024 M, katika Afisi ya Hizb ut Tahrir Wilayah ya Sudan. katika mji wa Port Sudan.

Mkutano huo ulizungumzia hatari ya matamshi ya chuki na uchochezi ya ukabila yanayopelekea kumwaga damu zisizo na hatia, fujo na machafuko miongoni mwa watu wa Sudan, mambo ambayo ni vitangulizi vya kuisambaratisha nchi na kuziwezesha nchi za kikoloni kuingilia Umma wetu.Njia ya kukabiliana na hili ni kupitia tu njia ya mahubiri inayobeba mradi wa kisiasa unaotokana na Aqidah (itikadi) tukufu ya Kiislamu, yenye kuimarisha udugu wa Kiislamu, na kuhitimisha kwa kusimamishwa dola iliojengwa juu ya msingi wa Uislamu. Hizb ut Tahrir iko kwenye mchakato wa kufanya kongamano la kuwasilisha ufumbuzi wa masuala ya nchi yanayotokana ndani yake na kukomesha uingiliaji wa nje.

Sheikh Othman Arefa alikaribisha ufumbuzi uliotolewa na Hizb ut Tahrir kwa matatizo yanayogusa uhalisia, akisema, "Tuko pamoja nanyi kwa moyo wote na kikamilifu." Pande zote mbili zilithibitisha dhamira yao ya kuendeleza mikutano kama hii.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu