Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  29 Shawwal 1445 Na: HTS 1445 / 39
M.  Jumatano, 08 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mkutano baina ya Kiongozi wa Kabila la Al-Habab na Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir Wilayah ya Sudan
(Imetafsiriwa)

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir Wilayah Sudan ukiongozwa na Ustadh Suleiman Al-Dasees, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, na akiwemo Ustadh Abdullah Hussein, Mratibu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir Wilayah Sudan, Ustadh Montaser Karar, Mratibu wa Kamati ya Amali za Mawasiliano huko Kassala, Ustadh Yaqoub Ibrahim, Mwanachama wa Hizb ut Tahrir, na Ustadh Adel Mohammed, Mwanachama wa Hizb ut Tahrir, walimtembelea Sheikh Hamed Mahmoud Hussein Kantabai, Nazir (kiongozi wa kabila) la Al-Habab, akiandamana na naibu wake Sheikh Idris Mohamed Idris, kwenye makaazi yake mjini Port Sudan mnamo siku ya Jumanne, 28 Shawwal 1445 H, sawia na 07/05/2024 M.

Ujumbe huo ulieleza suala muhimu la Ummah na uliitambulisha Hizb ut Tahrir, ukieleza kwamba inatetea kuhuisha maisha kamili ya Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Walisisitiza ulazima wa kulifanyia kazi lengo hili, wakichukulia kuwa ni faradhi juu ya Waislamu kote duniani. Walibainisha kwamba katika kutokuwepo kwake, Umma umesambaratika, umekumbwa na majanga na maafa makubwa, yakiwemo uharibifu na vita vikali baina ya watu wa Umma wao kwa wao.

Kisha naibu wa kiongozi wa kabila, Idris Mohamed Idris, alizungumza, akikaribisha kile wajumbe walichowasilisha, akisema kwamba ni lengo kuu na zuri ambalo linahitaji juhudi kubwa na muhanga mkubwa. Alithibitisha kwamba hakuna Muislamu atakayepingana na jambo hili, akisema, "Kwa mara ya kwanza, tunakutana na chama cha kisiasa ambacho lengo lake ni kuinua neno la Mwenyezi Mungu, kuwaunganisha Waislamu, na sio kukimbizana na mamlaka ya muda mfupi."

Mkutano huo ulihitimishwa na Nazir Hamed Kantabai, kutoa shukrani kwa Hizb ut Tahrir kwa ziara hii ya kipekee. Alipendezwa na uwazi wa ruwaza yao, akisema, "Tunajivunia kwamba mmezingatia viongozi wa makabila. Sisi, kwa upande wetu, tutawajulisha watu wetu kuhusu jitihada hii kubwa." Alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuwasiliana na kubadilishana ziara.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu