Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 22 Jumada II 1446 | Na: HTS 1446 / 38 |
M. Jumanne, 24 Disemba 2024 |
Ripoti ya Habari
Maingiliano ya Ummah na Hotuba: “Khilafah Ndio Mfumo wa Utawala katika Uislamu”
(Imetafsiriwa)
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ilitoa hotuba ya kisiasa katikati mwa soko kuu la Port Sudan mnamo Jumatatu, 23 Disemba 2024, chini ya mada: “Khilafah Ndio Mfumo wa Utawala katika Uislamu.” Hotuba hiyo ilitolewa na Ustadh Yaqub Ibrahim mwanachama wa Hizb ut Tahrir ambaye alisisitiza kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amewawajibisha Waislamu kutabikisha hukmu za Uislamu na kupangilia nyanja zote za maisha yao kwa mujibu wake. Alieleza kwamba utabikishaji huu hutokea kupitia Bay’a halali kwa Khalifa ambaye anasimamisha Dini na kuifikisha kwa ulimwengu.
Aliangazia ufaradhi wa Khilafah na ulazima wa Ummah kufanya kazi kuelekea kusimamishwa tena, akiregelea maandiko kadhaa, yakiwemo maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَن يَفْتِنُوكَ عَن بَعْضِ مَا أَنزَلَ اللهُ إِلَيْكَ فَإِن تَوَلَّوْا فَاعْلَمْ أَنَّمَا يُرِيدُ اللهُ أَن يُصِيبَهُم بِبَعْضِ ذُنُوبِهِمْ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ لَفَاسِقُونَ]
“Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka, basi jua kwamba hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwasibu kwa baadhi ya dhambi zao. Na hakika wengi wa watu ni wapotofu.” [Al-Ma'ida:49]. Na pamoja na hadith iliyopokewa na Al-Bukhari kutoka kwa Abdullah ibn Umar (ra), ambayo Mtume Muhammad (saw) amesema: «وَمَنْ مَاتَ وَلَيْسَ فِي عُنُقِهِ بَيْعَةٌ مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً» “Na yeyote anayekufa na hana katika shingo yake ahadi ya utiifu (kwa Amiri) amekufa kifo cha Kijahiliya.”
Pia aliangazia jinsi mifumo ya utawala ya leo, iwe ya kidemokrasia, ya kiraia, au ya kijeshi, inagongana na Uislamu. Alifafanua kuwa mifumo yote hiyo ni mazao ya yaliyopitwa na wakati ya dola za kikoloni.
Hatimaye, aliwataka wale waliokuwepo, pamoja na Ummah wote wa Kiislamu, kufanya kazi kuelekea kusimamisha faradhi hii kubwa: Khilafah Rashida wa pili kwa njia ya Utume.
Hadhira iliitikia kwa maingiliano thabiti na mazuri, ikionyesha furaha, matumaini, na nyimbo za kusifu na takbira. Wengine hata waliomba mwishoni hotuba iendelee na isimalizike, kwa kuzingatia manufaa ya mazungumzo hayo.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |