Jumatatu, 04 Sha'aban 1446 | 2025/02/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  28 Jumada II 1446 Na: HTS 1446 / 38
M.  Jumatatu, 30 Disemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hotuba Inayohusu Bendera za Rayah na Liwaa za Mtume (saw)

Ilipambwa kwa Takbira na Machozi katika Soko Kuu la Port Sudan

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ilitoa hotuba yake ya kisiasa ya kila wiki, iliyokuwa na kichwa: “Je, Mtume (saw) alikuwa na bendera na Rayah?”, mnamo Jumatatu tarehe 28 Jumada al-Akhirah 1446 H sawia na 30/12/2024 M. Ustadh Muhammad Jami’ (Abu Ayman), Msaidizi wa Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan, alizungumza akisisitiza kuwa bendera ya Liwaa na Rayah katika Uislamu ni suala la dini, itikadi, mfumo na nembo ya Uislamu. Mtume (saw), ana benera (Liwaa) nyeupe kama bendera ya amiri jeshi, na bendera (Rayah) nyeusi kwa makamanda wa majeshi na vikosi, na inaitwa Uqab, zimeandikwa juu yazo “La Ilaha illa Allah Muhammad Rasulullah”, zikitolewa dalili nyingi, zikiwemo baadhi yake aliyopokea Al-Tirmidhi, Ahmad, na Ibn Majah, kutoka kwa Ibn Abbas, ambaye alisema: وَلِوَاؤُهُ أَبْيَضَ» كَانَتْ رَايَةُ رَسُولِ اللهِ ﷺ سَوْدَاءَ» “Bendera ya Rayah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ilikuwa nyeusi. Na bendera yake ya Liwaa ilikuwa ni nyeupe.”

Vile vile alitaja kuwa kinachothibitisha ulazima wa kunyanyua Rayah na Liwaa hizi ni kujitoa mhanga kwa Maswahaba na kuuawa kwao kishahidi katika kuihami. Na akabainisha,  kwamba Waislamu waliendelea kushikamana na hilo, wakinyanyua Rayah na Liwaa ya Mtume (saw) katika vita, na katika taasisi za Dola na nyumba zao, hadi maadui wa kikoloni walipoivunja Khilafah Uthmani na kuzigawanya nchi za Waislamu. Hivyo wakachora bendera za kitaifa zilizo sasa, kwa makubaliano ya Sykes na Picot, Mawaziri wawili wa Mambo ya Nje wa Ufaransa na Uingereza, na kuibadilisha Rayah ya Mtume (saw) kama walivyobadilisha hukmu za kisheria na kuziweka sheria za kibinadamu ikiwemo demokrasia, usekulari, serikali ya kiraia, serikali ya kijeshi ... nk.

Aliashiria kuwa wajibu wa Umma wa Kiislamu hivi leo ni kuregesha mfumo kamili wa Kiislamu; Khilafah Rashida kwa njia ya Utume inayoinua bendera (Rayah) hii, kusimamisha dini, kutabikisha Shariah, na kuunganisha umma wa Mtume (saw). Na katika kipindi cha maswali na michangio, hadhira ilitangamana kwa shangwe kwa kupiga takbira, tahlil, na kulia, na kunyanyua na kupeperusha bendera za Rayah na Liwaaa, pamoja na mashababu wa Hizb ut Tahrir, kwa kukumbatiana na salamu njema na dua za kheri.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu