Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 18 Rajab 1446 | Na: HTS 1446 / 42 |
M. Jumamosi, 18 Januari 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Machafuko na Ghasia nchini Sudan Kusini Zinasisitiza Haja ya Umma kuwa na Kiongozi mwenye Kuwalinda
(Imetafsiriwa)
Ulimwengu umefuatilia machafuko ya Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini, ambayo yalilenga watu waliokimbia makaazi yao na wakaazi kutoka Sudan Kaskazini. Matukio haya yalichochewa na ripoti zinazowatuhumu wanajeshi wa Sudan kwa kuwaua watu kutoka Sudan Kusini huko Wad Madani baada ya jeshi kuutwaa tena mji huo. Kulingana na gazeti la ‘Sudan Tribune’, Wasudan watatu waliuawa mjini Juba, na wengine saba kujeruhiwa.
Afisi ya Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir Mayardit, kupitia kwa katibu wake wa vyombo vya habari Martin Manyiel, ilitoa wito wa utulivu na kuhimiza kuepukwa kwa vitendo ambavyo vinaweza kuzidisha uhasama kati ya nchi hizo mbili. Mamlaka mjini Juba zilituma vikosi vya kijeshi kwenye masoko na kuwahamisha raia wa Sudan hadi maeneo salama mnamo siku ya Ijumaa.
Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imeeleza wasiwasi wake mkubwa na kuwataka raia wa Sudan walioko Sudan Kusini kuwa waangalifu na makini. Kwa kuzingatia hali hii, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan inawasilisha nukta zifuatazo:
1- Dola lazima ihakikishe kuwa vikosi vya jeshi vinafanya kazi ndani ya mipaka ya sheria za Kiislamu, kujiepusha na kuwalenga raia wasio na silaha ambao hawashiriki katika mapigano. Kulipiza kisasi kwa msingi wa shutuma, shaka, au tuhuma ni haramu. Kanuni ya kisheria ni kwamba watu wanachukuliwa kuwa hawana hatia hadi ithibitishwe kuwa na hatia katika mahakama ya sheria. Utesaji bila shaka umeharamishwa, na yeyote anayejihusisha nayo lazima awajibike.
2- Kuwahukumu au kuamiliana na watu kwa msingi wa rangi ya ngozi, jamii, au kabila zao ni haramu. Vitendo hivyo ni mabaki ya ujinga (Jahiliyyah) yanayochukiza na yanalaaniwa katika Uislamu. Mtume Muhammad (saw) amesema, «دَعُوهَا فَإِنَّهَا مُنْتِنَةٌ» “Uacheni kwa maana ni uvundo”. Pia amesema, «مَنْ تَعَزَّى بِعَزَاءِ الْجَاهِلِيَّةِ فَأَعِضُّوهُ وَلَا تَكْنُوا» “Yeyote anayejinasibisha (katika nasaba) kwa sifa ya Jahiliyyah na mwambieni aiume dhakari ya babake mzazi na wala msiseme kwa mafumbo.”
3- Dola inawajibu wa kuwalinda raia wake na kuwahakikishia usalama na amani yao. Hili ni jukumu ambalo kila kiongozi atahisabiwa. Mtume Muhammad (saw) amesema, «الْإِمَامُ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ» “Mtawala ni mlinzi wa raia wake na atauliza kuhusu raia wake.”
4- Sudan imekuwa jukwaa la mivutano la dola za kimataifa. Mzozo kati ya watu wa kaskazini na kusini mwa Sudan bila shaka unachochewa na wale wanaotaka kuitumia kwa malengo yao ya kisiasa, hata kwa gharama ya maisha ya watu. Vitendo kama hivyo ni vya kukemewa. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,
[فَأَمَّا الزَّبَدُ فَيَذْهَبُ جُفَاءً وَأَمَّا مَا يَنفَعُ النَّاسَ فَيَمْكُثُ فِي الْأَرْضِ]
“Basi lile povu linapita kama takataka tu basi. Ama kinacho wafaa watu hubakia kwenye ardhi.” [Surat Ar-Ra’d:17].
Mizizi ya ufisadi huu itatokomezwa kutoka Sudan wakati Uislamu safi utakapoasisiwa kama mfumo tawala chini ya Khilafah.
Matukio ya Sudan Kusini, pamoja na uharibifu uliosababishwa na vita hivi tangu Aprili 15, 2023, yanasisitiza udharura wa kusimamishwa Khilafah ambayo ni ngao ya ulinzi, kama Mtume Muhammad (saw) alivyosema, «إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ» “Mtawala wa Kiislamu ni ngao.”
Bila ya Khilafah, Ummah wa Kiislamu utakabiliwa na balaa moja baada ya jengine, huku serikali hizi zisizo na ufanisi zinabakia hazina nguvu ya kuzizuia au kuzishughulikia. Ni wajibu wa watu wa Ummah huu kufanya kazi kuelekea kusimamisha Khilafah ili kulinda maisha yao, heshima, na mali zao, na zaidi ya yote, kumridhisha Mwenyezi Mungu, na hivyo kupata furaha hapa duniani na kesho Akhera.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |